MM,
Insha Allah nitajitahidi:
"TAA mjini Lindi ilikuwa chini ya uongoziwa Suleiman Masudi Mnonji aliyekuwa Rais na Katibu wake alikuwa Mohamed Waziri.Mnonji alikuwa fundi cherahani na Waziri alikuwa mchoraji wa ramani za nyumba.TAA ilichelewa kuanza mjini Lindi. TAA ilianzishwa Lindi mwaka 1953 wakatiuongozi wa TAA mjini Dar es Salaam si tu ulikuwa unaigeuza TAA kuwa chama chasiasa bali ulikuwa ukifanya mipango kumpeleka mjumbe wake Umoja wa Mataifakudai uhuru. Masudi Mnonji alikuwa na uzoefu wa kutosha katika siasa. Baada yaVita Kuu ya Pili alikuwa amejaribu kuanzisha vyama vya wafanyakazi katikamashamba mbalimbali ya mkonge kusini mwa Tanganyika. Vilevile aliwakusanyawapishi na madobi mjini Lindi waanzishe umoja wao. Ilikuwa kupitia juhudi zakebinafsi TAA ijapokuwa ilichelewa, ilikuja kuanzishwa mjini Lindi na Mnonjialijitolea nyumba yake katika mtaa wa Makonde kama ofisi ya chama. Mnonji kwakutambua umuhimu wa kuwa na uongozi ulioelimika vizuri, alimleta NangwandaSijaona kutoka Nachingwea aje aishauri TAA jinsi ya kufanya mambo kwa utaalamu.Wakati huo mjini Lindi kulikuwa na chamacha wafanyakazi bandarini Dockworkersí Union chini ya uongozi wa Mussa AthumaniLukundu, chama ambacho kwa kiasi chake kilianzisha vuguvugu la siasa za vyamavya wafanyakazi. Ingawa vyama hivi viwili, yaani TAA na Dockworkersí Unionvilikuwepo katika mji mmoja, siasa za hiki chama cha pili cha wafanyakazibandarini hazikupitia TAA kama ilivyokuwa mjini Dar es Salaam. Hii kidogoilidhoofisha mwamamko wa siasa kwa wananchi. Jimbo la Kusini lilikuwa katikausingizi mzito wakati sehemu nyingine Tanganyika zilikuwa zikipiga hatua kwendambele zikiandaa vita dhidi ya utawala wa kikoloni. Chanzo cha usingizi huumzito huko kusini ulikuwa na asili yake katika historia ya Tanganyika.Vita vya Maji Maji vilipoanza kusini yaTanganyika mwaka 1905 kwa nia ya kuwafukuza Wajerumani kutoka Tanganyika, zilesehemu zenye Wakristo wengi zilikataa kujiunga na vita na badala yakewakajiunga na majeshi ya Wajerumani na kupigana bega kwa bega na dhidi yawazalendo. Hii ilitokana na sababu ya kuwa uasi dhidi ya dhulma wa Wajerumaniulianza katika maeneo yenye Waislam wengi na vita vikachukua sura ya vita vyaKiislamu dhidi ya Wazungu ambao dini yao ni Ukristo. Kwa kuwa wamishonariwalikuwa washirika wa wakoloni, walichukuliwa kama maadui na hivyo ikawa vituovyao vinashambuliwa na wapiganaji wa Maji Maji. Kutokana mashambulizi haya,Wakristo walivichukua Vita Vya Maji Maji kama vita dhidi ya Ukristo. Harakatiza Maji Maji zilishindwa na Wajerumani walifanya fisadi kubwa dhidi ya wananchina viongozi wao. Jambo hili liliacha kovu kubwa katika fikra za wananchi na kwaupande wa Wakristo ambao walinusurika na ghadhabu ya Wajerumani, wengi waowakajiweka mbali na aina yoyote ya kupinga ukoloni. Kufuatia historia hii Waafrika waliokuwakusini ya Tanganyika sasa wakiwa chini ya utawala wa Waingereza na kuwa chiniya himaya ya wamishonari walipupazwa kiasi kiasi kwamba waliogopa siasa. Baadaya Waafrika kushindwa vita kwa silaha kali za Wazungu sasa Kanisa likaona ndaniya fadhaa ile fursa yao kutawala sehemu hiyo kwa kutoa vishawishi kama vileshule na hospitali. Kwa hiyo Wamishionari na Waingereza walionekana kamamabwana wema wenye kuwajali raia zao kinyume na serikali katili na ya kidhalimu ya Wajerumani. Vuguvugu lasiasa kama ilivyokuwa Vita vya Maji Maji, lilianza katika maeneo ya Waislamkufuatia mfumo ule ule kama ilivyokuwa katika upinzani wa ukoloni waWajerumani. Wakristo katika Jimbo la Kusini waliiona TANU kama walivyovionaVita Vya Maji Maji, kama harakati nyingine za Waislam zilizowa zinakuja tenakwa mara ya pili kuvuruga amani na utulivu. TANU ilipoanza ikawa inavuma kuwasafari hii Waislam walikuwa wamemua kuanzisha vita dhidi ya Waingereza kamawalivyoanzisha vita na Wajerumani. TANU ilipoanzishwa mjini Dar es Salaam nahisia za utaifa zilipokuwa zikipandapole pole katika fikra za wananchi katika sehemu nyingi za Tanganyika, Jimbo laKusini lilikuwa bado usingizini likiishi katika zama za kale. Mnonji na Waziri, kwa sababu ya utu uzima wao, darajayao katika jamii na hasa kutokana na kuhusika kwao katika siasa za pale mjini,walikuwa na nguvu kubwa katika TAA. Wakati TANU imeshachukua nafasi ya TAA,uongozi wa TAA Lindi haukutaka kufungua tawi la TANU. Mtu wa kwanzakuutanabaisha uongozi wa TAA mjini Lindi juu ya mageuzi yaliyokuwa yakitokeaTanganyika na kuanzishwa kwa chama kipya cha siasa mjini Dar es Salaam alikuwaAbdallah Juma Makopa, kijana kutoka Tanga akifanya kazi ya ukarani Posta yaLindi. Makopa aliwaendea Mnonji na Waziri na kuwajulisha kuhusu kuanzishwa kwaTANUmjini Dar es Salaam na aliwashauri waanzishe TANU pale Lindi. Jambo hilolilipingwa moja kwa moja na Mnonji, Waziri, Said Nassoro, Abdallah Mhuji nawanachama wengine wa TAA.Chama cha Waafrika ambacho kilianzishwasiku nyingi mjini Lindi na kwa hakika ndicho kilikuwa chama cha pekeekushughulikia maslahi ya Waafrika sehemu za kusini kilikuwa African WelfrareAssociation ambacho mlezi wake alikuwa John Nevi, Mjaluo kutoka Kenya na katibuwake alikuwa Casian Njunde, Mngoni wa Songea. Makopa aliposhindwa kukishawishikile kikundi cha wazee wa TAA aliwaendea Yusufu Chembera na Rashid SalumMpunga. Chembera alikuwa na umri wa miaka thelathini na nne na Mpunga alikuwakijana wa miaka ishirini na saba. Chambera alikuwa amesoma hadi shule ya msingina Mpunga alikuwa amemaliza madras. Chembera alikuwa akifanya kazi katikakantini ya Lindi Welfare Centre, wakati Mpunga alikuwa dereva wa lorialiyeajiriwa na mfanyabishara wa Kihindi. Makopa aliwashauri Chembera na Mpungajuu ya uwezekano wa kuwahamasisha wananchi wawaunge mkono ili tawi la TANUlifunguliwe pale mjini. Aliwaambia alitaka sana kufanya hivyo yeye mwenyewelakini asingeweza kwa sababu yeye alikuwa mtumishi wa serikali na hakuwaakifahamika sana mjini. Uongozi kama wao ndiyo ungeweza kuaminiwa na wananchina usingetiliwa mashaka. Makopa, Chembera na Mpunga walikubaliana kuwa kabla yakuanza kufanya kampeni waziwazi kwa ajili ya TANU, lazima wawaandikishewanachama wachache kama waasisi wa chama. Mpunga na Chembera walimwandikishakijana mmoja akiitwa Abdallah Faraj na katika muda mfupi waliweza kuwapatatakriban wanachama kumi na tano walioridhia kujiandikisha kama wanachamawaasisi wa TANU.Baada ya kuandikisha wanachama waasisimkutano wa siri uliitishwa katika Welfare Centre ambako ndiko alikokuwaakifanya kazi Chembera. Chembera aliwaeleza kwa ufupi wale wanachama wa mwanzokuhusu malengo na madhumuni ya chama hicho kipya cha siasa. Mkutano huoulichagua kamati ya watu watatu yaani, Makopa, Chembera na Faraj ili kuwakabiliMnonji na Waziri kuwaleza kuwa TAA haipo tena nchini Tanganyika. Lengo lilikuwakuwasadikishia kuwa ilikuwa kazi bure na kupoteza wakati kujaribu kuihuisha TAAmjini Lindi wakati ambapo Tanganyika nzima ilikuwa ikisonga mbele na TANU.Baada ya mjadala mrefu sana na mkali wa wale vijana watatu na ule uongozi waTAA wa wazee, walikubaliana TANU lazima isajiliwe mjini Lindi.Uchaguzi ulifanyika na Shaaban Msangi,kijana wa Kipare akifanya kazi kwa Smith Mc Kenzie, alichaguliwa rais na AhmedSeif, katibu. Mpunga, Chembera, Mnonji na Idd Toto walichaguliwa wajumbe wakamati. Ahmed Seif alikuwa kijana ambaye ndiyo kwanza amemaliza shule, yeyealikabidhiwa kuendesha ofisi kwa niaba ya uongozi. TANU mjini Lindi ilimwajiri ili kukiandaachama kiweza kufanya kazi zake kwa ufanisi. Hassan Mohamed Kinyozi aliajiriwakama mhudumu wa ofisi. Hawa wawili walikuwa ndiyo wafanyakazi wa kwanza wa TANUwaliokuwa wakilipwa mshahara katika Jimbo la Kusini na wakawa miongoni mwawafanyakazi wachache sana walioajiriwa na TANU kwa wakati ule. Mnonji alitoanyumba yake katika mtaa wa Makonde kuwa ofisi ya kwanza ya TANU Jimbo laKusini. Baada tu ya kuanzishwa kwa TANU, Athumani Mussa Lukundu, kiongozi waLindi Dockworkersí Union, aliunganisha chama chake na TANU. Jambo hili, kwaTANU lilikuwa la kuitia moyo sana kwa sababu Dockworkersí Union ilikuwa nawananchama wengi na hatua ile iliongezea TANU nguvu.Baada ya muda mfupi tu toka kufunguliwakwa TANU Mkutano Mkuu wa Kwanza wa TANU wa mwaka 1955 ulifuatia. Tawi la Lindililikuwa tayari lina uhusiano na makao makuu ya TANU mjini Dar es Salaam, nalilikuwa likitarajia kuhudhuria mkutano huo na kukutana na Julius Nyerere nauongozi mzima wa TANU pale makao makuu Dar es Salaam. Mpunga, mwanachamamuasisi wa TANU, na Ali Ibrahim Mnjale waliteuliwa kuhudhuria mkutano huo kamawajumbe kutoka Jimbo la Kusini. Halmashauri ya TANU ya Lindi iliwaelekezawajumbe hawa wafikishe ombi rasmi kwa makao makuu ili Julius Nyerere ajekufanya ziara kusini kwanza, kukutana na wananchi na kufanya kampeni kwa ajiliya TANU na pili aje kupambana na propaganda dhidi ya TANU zilizokuwazikitawanywa na Yustino Mponda. [1]Mponda akitumia uhusiano wake na serikali ya kikoloni na nafasi yake kamamjumbe wa Baraza la Kutunga Sheria kutoka Newala; na vilevile akitumia ushirikianowake wa muda mrefu na kanisa ambao bila shaka yoyote lilikuwa serikali ndani yaserikali kule kusini, alikuwa ameanza kampeni yake ya kuipinga TANU. Hilililikuwa likiathiri msukumo wa uanachama. Mponda alikuwa mmoja wa wajumbewaliotumwa na Gavana Twining kwenda Umoja wa Mataifa Februari, 1955 kwa niabaya serikali ya kikoloni kwenda kuipinga. Uongozi wa TANU huko Lindi ulitakaNyerere aende kupambana na Mponda akiwa katika uwanja wake mwenyewe, ndanikabisa ya ngome ya Ukristo wa Kikatoliki katika Tanganyika.Mkutano mkuu wa mwaka wa TANU ulifanyikakatika ukumbi wa Hindu Mandal mjini Dar es Salaam. Siku kabla ya mkutano TANUilimwalika Gavana Edward Twining kwenye tafrija katika Ukumbi wa Arnatouglolakini alikataa kistaarabu na akamtuma Chief Secretary, Bruce Hutt,kumwakilisha. Baada ya mkutano, wakati wajumbe wengine wanaondoka kurudi kwenyemajimbo yao, Mpunga na Mnjawale walibakia nyuma kukutana na uongozi wa makaomakuu wa Julius Nyerere, Sheikh Suleiman Takadir, John Rupia, Ali Mwinyi Tambwe,Said Chamwenyewe, Oscar Kambona na wengineo. Mpunga na Mnjawale waliwafahamishaviongozi wa makao makuu kuhusu hali mbaya ya siasa Jimbo la Kusini. Mbali nakampeni za kuipinga TANU za Mponda, katika ziara yake Lindi Gavana Twiningaliwatahadharisha Waafriika wa Tanganyika wasijihusishe na ëwafaanya fujowanaotaka kuzusha vuruguí. Twining alikuwa akitoa onyo hili akiikusudia TANUambayo ilikuwa imeanzishwa mwaka uliopita. Hotuba hii ya Gavana iliwatishawananchi kujiunga na TANU. Mpunga na Mnjawale walisisitiza kuwa kuja kwaNyerere mjini Lindi kulitakiwa haraka sana kukabiliana na vyote viwili, kwanzaile hotuba ya gavana na pili zile kampeni za kupinga TANU zilizokuwazikiendeshwa na Liwali Yustino Mponda. Wakati huo Abeid Amani Karumealiyehudhuria ule mkutano alimwalika Nyerere afanye ziara Zanzibar. Kitu chakustaajabbisha ni kuwa, Nyerere alionekana kuiafiki zaidi ziara ya Zanzibarkuliko ile safari ya kwenda kusini kuiimarisha TANU. Mpunga alimsisitiziaNyerere umuhimu wa yeye kwenda Lindi ambako kunaweza kuwa ndiyo chanzo cha TANUkupata ufanisi Newala, Songea, Tunduru na Masasi ambako kulikuwa na upinzanimkubwa dhidi ya TANU. Kanisa lilikuwa likiwazuia Wakristo kujiunga na TANU.Sheikh Suleiman Takadir, Said Chamwenye, John Rupia, Ali Mwinyi Tambwe wotewaliunga mkono ule ujumbe wa Lindi juu ya suala hili. Baada ya kufikiamakubaliano, Mpunga na Mnjawale walipewa barua ya kuthibitisha safari yaNyerere. Ziara ya Nyerere ilikuwa ianzemuda mfupi kutokea hapo kwa kuwa ilikuwa ndiyo siku za mwisho za kiangazi.Barabara sehemu ya kusini ya Tanganyika zilikuwa hazipitiki wakati wa masika,zikiitenga kabisa kusini toka sehemu zilizobaki za nchi. Ali Mwinyi Tambwe naRajab Diwani walifuatana na Nyerere kwenda Jimbo la Kusini kuondoa wasiwasi nawoga uliozushwa na Gavana Twining na kibaraka Yustino Mponda.Nyerere na msafara wake ulipokelewa nauongozi wa TANU wa Lindi huko Mbanji, kijiji kidogo nje ya mji. Msafara waNyerere ulipowasili Mbanji ilikuwa kiasi cha saa moja jioni hivi na gizalilikuwa linaanza kutanda. Mbali na Mpunga na wale wajumbe wawili waliokutanana Nyerere mjini Dar es Salaam mwezi uliopita, hakuna hata mtu kati ya umma uleuliokuja kupokea ujumbe kutoka makao makuu ya TANU aliyekuwa anajua Nyerereanafanana vipi. Mpunga, dereva wa lori, alijibagua kutoka kwa lile kundi lawatu akawa amesimama pembeni ili Nyerere apate kumuona. Baada ya Nyerere kumtiaMpunga machoni, Mpunga alimwendeakumsalimu Nyerere, Tambwe na Diwani; kisha aliligeukia lile kundi la watukumtambulisha Nyerere kwa wananchi akilitaja jina lake kwa sauti kubwa. Baadaya hapo aliutambulisha ule ujumbe wa Nyerere. Nyerere na ujumbe wakeulisindikizwa kwa shangwe na kundi la watu hadi ofisi ya TANU kwenye nyumba yaMnonji. Kupakana na ofisi ya TANU ilikuwepo nyumba ya seremala mmoja, Issa binAli Naliwanda. Hii ndiyo nyumba iliyochaguliwa alale Nyerere na ujumbe wake, sikwa sababu ilikuwa nzuri kupita zote. Ilichaguliwa na kupewa heshima hii kwasababu ilikuwa karibu sana na ofisi ya TANU na hivyo basi ilirahisishia TANU kaziya ulinzi wa Nyerere. Siku iliyofuata ilikuwa Jumapili na Nyerere aliwaombawenyeji wake apelekwe kanisani kwa ajili ya ibada.Kanisa Katoliki mjini Lindi ni jengo lafahari lililoko ufukweni katika Bahari ya Hindi. Lindi ulikuwa mji wa Waislam.Mbali na mlio wa kengele za kanisa hakuna mtu pale mjini aliyekuwaakishughulishwa na kile kilichokuwa kikifanyika kwenye viwanja vya kanisa. Watuwachache waliokuwa wakienda kusali kanisani walikuwa Wakristo waliokuja Lindikutoka sehemu nyingine za Tanganyika kufanya kazi katika ofisi za serikali.Ghafla mahala hapa palipokuwa pweke, palipopuuzwa kwa miaka na Waislam wamjini, pakawa muhimu kwa sababu rais wa TANU ambae alikuwa Mkatoliki alikuwa nahaja ya kuhudhuria ibada pale kanisani. Hakuna mtu katika uongozi wa TANU waLindi aliyejua ndani ya kanisa lile kulikuwa vipi wala hapakuwa na yoyote katiyao aliyewahi kuingia ndani ya kanisa, si Lindi wala mahali popote pale.Uongozi wa TANU wa Waislam mjini Lindi haukumwamini Mkristo yoyote kumsindikizaNyerere kanisani ili kumpa ulinzi. Baada ya kujadili suala hilo kwa urefuhatimaye iliamuliwa kuwa Mpunga nawanachama wachache Waislam wenye kuaminika lazima wamsindikize Nyerere kanisanina wengine wabakie nje kulinda mlango.Jumapili hiyo Nyerere aliingia ndani yakanisa Katoliki mjini Lindi akifuatwa nyuma na walinzi wake Waislam wakiongozwana Salum Mpunga, dereva wa lori shupavu. Misa hii ëmaalumí ilidumu katika fikra za wale Wakristowaliokuwepo pale kanisani kwa miaka mingi kwa kuwa tukio hilo liliwagusa sanaWakristo walioshuhudia mkasa ule ndani ya kanisa la Lindi. Hii huenda ilikuwamara ya kwanza na ya mwisho kwa Nyerere kumsalia Mungu wake huku akiwaamesimamiwa na Waislam.DC mkoloni alikataa kutoa kibali kwa TANUkufanya mkutano wa hadhara. Akiwa amekasirika sana, Shabaan Msangi aliitishamkutano wa dharura wa tawi uliohudhuriwa na Nyerere na Tambwe. Baada ya mkutanohuo Tambwe alikwenda kumwona DC. Ruhusa ilitolewa, na adhuhuri hiyo siku yaJumapili, katika kiwanja ambacho Wazungu walikuwa wakicheza gofu, ambako mwakammoja uliopita Gavana Edward Francis Twining alitoa hotuba iliyowavunja moyoWaafrika, Nyerere alihutubia mkutano wa hadhara. Kamwe haijapata kutokea kablaya siku ile katika historia nzima ya Jimbo la Kusini, watu wengi kiasi hichokujumuika mahali pamoja. Wazungu na Wahindi pamoja na askari, watu wakiwawamekaa na wengine wamesimama katika yajua kali walikuja kumsikiliza Nyerere akihutubia. Ili kuhakikisha amani nausalama pale mkutanoni serikali iliweka askari waliouzunguka uwanja mzima wamkutano. Nyerere aliwafikishia watu ule ujumbe wa TANU wa kuwa, kutawaliwa nifedheha, na Waafrika wa Tanganyika lazima wadai uhuru wao. Uingereza ilikuwaikiitawala Tanganyika chini ya udhamini kwa niaba ya Umoja wa Mataifa, nawakati ukiwa muafaka inabidi Uingereza ikabidhi nchi kwa wananchi wenyewe. TANUilikuwa imewasili Jimbo la Kusini."
Mohamed