Historia ya Uhuru isimuliwavyo na Mohammed Said yakosolewa

Historia ya Uhuru isimuliwavyo na Mohammed Said yakosolewa

Nguruvi3,

Huo ndiyo ukweli kuwa Wamanyema, Wazulu na Wanubi waliingia Tanganyika kutoka nje na walikuwa watumishi wa Wajerumani na walipigana dhidi ya wazalendo wa nchi hii.

Hilo ni wazi kabisa.

Mabadiliko yalikuja kuletwa na watoto wao ambao walizaliwa katika utawala wa Waingereza. Naweka tena kwa faida ya wanaukumbi:
Nadhani "mnakasha' umefika pazuri sasa. Utaona kwamba hata wale waliomuua Gaddaffi wenyewe pia hawakuwa na lengo moja mara tuu walipompata. Hata wakristo na waislamu wapo wema na wabaya. Huwezi kwa ujumla ukasema wakristo walikuwa na lengo la kudhulumu waislamu haki yao ya kuanzisha mapambano dhidi ya wakoloni.

Hoja yangu hapa ni kwamba Uislam au Ukristo siyo utakatifu wa kuhalalisha nafasi ya mtu kwenye jamii yetu. Kama tukiwa wakweli wakati huo wa kupigania uhuru bila watu wa kanda ya ziwa kukubali kuiunga mkono TANU leo hii ingewezekana kabisa historia ya nchi hii isingekuwa hivi.
 
Mgalanjuka,

Kweli nashindwa kupata "gist" ya swali lako.
Niwie radhi.

Mohamed

Sawa MS, haina tabu. Ila kwa faida ya wasomaji wengine kuna maswali mawili katika aya hiyo na yana alama ya kuuliza (?) Hivyo mwingine atakaye yaona kwa upeo tofauti basi si vibaya kuyaweka bayana ili twende sawa.
 
Ahsante ndugu yangu nadhani tunaelekea ukingoni mwa mnakasha.

Mohamed

Naam, maana naona mengine tunarudi kule kule tu. NItafurahi sana kama inshallah siku moja tuweze kujadiliana kwa kina kitabu chako cha Sykes. Itakuwa ni heshma kubwa kwangu.
 
Kinachofutwa ni kile kilichoandikwa. Mbona hamtuambii ni nani aliyeandika hiyo historia na nani aliifuta na kwa maagizo ya nani na maagizo hayo yalitolewa lini?

Kigarama rudi nyuma katika Mjadala huo na mwengine wa Miaka 50 ya uhuru wa Tanganyika utaona nani amefuta historia ya Tanzania na kwa faida ya nani. Hatuna muda wa kurudia rudia kauli unatupotezea muda . By the way ushauona ushahidi wa Mkwawa aliyewachachafya wajerumani alikuwa mwislamu?
 
Nimeona nitumie njia hii kwani tangu mwanzo nimejitahidi kwa kila hali kuuliza hili swali lakini kila mara unalikwepa. Nakumbuka mara ya mwisho ulidai huwezi kunijibu kwa sababu eti niliwatukana wazee wako. Niwie radhi kama kweli uliona nimewatukana wazee wako. Lakini swali langu lipo palepale. Wewe ni MMANYEMA??
 
Hivi mtu kuandika kwa Irabu za Kiarabu ni Uislamu miye nilikuwa sijui. Wakristo wa Misri wanatumia Irabu gani kuandikia Biblia yao... wanatumia Irabu ya Kiarabu bila shaka!!?? Mkwawa kundika kwa Irabu za Kiarabu. Nimo njiani kuwasiliana na mtunza historia za kina Mkwawa siyo Chifu Abdul bali ni wazee wake.

Mkuu nashukuru kwa hoja yako.

Binafsi nimepata kufanya kazi na waarabu, miongoni mwao walikuwa waarabu wa kutoka misri na mmoja wao alikuwa ni mkristo.

Ukweli ni kwamba alikuwa anaandika kwa irabu za kiarabu. Alikuwa anasali kwa kiarabu. Kwahiyo hoja ya mtu kuandika ama kusoma irabu za kiarabu haimfanyi kuwa muislamu moja kwa moja.
 
Kigarama rudi nyuma katika Mjadala huo na mwengine wa Miaka 50 ya uhuru wa Tanganyika utaona nani amefuta historia ya Tanzania na kwa faida ya nani. Hatuna muda wa kurudia rudia kauli unatupotezea muda . By the way ushauona ushahidi wa Mkwawa aliyewachachafya wajerumani alikuwa mwislamu?
Nina watu ambao wana credibility ya kulizungumzia hilo na Inshaalah kama itawezekana Jumatano nitakuwa hapa kusema hao wazee wangu wamesema nini.
 
Sawa MS, haina tabu. Ila kwa faida ya wasomaji wengine kuna maswali mawili katika aya hiyo na yana alama ya kuuliza (?) Hivyo mwingine atakaye yaona kwa upeo tofauti basi si vibaya kuyaweka bayana ili twende sawa.

Wewe nae huulizi maswali yanayoeleweka, unauliza unatoa maelezo mareeefu. Nenda moja kwa moja kwenye swali achana na maelezo mareefu.
 
Mkuu nashukuru kwa hoja yako.

Binafsi nimepata kufanya kazi na waarabu, miongoni mwao walikuwa waarabu wa kutoka misri na mmoja wao alikuwa ni mkristo.

Ukweli ni kwamba alikuwa anaandika kwa irabu za kiarabu. Alikuwa anasali kwa kiarabu. Kwahiyo hoja ya mtu kuandika ama kusoma irabu za kiarabu haimfanyi kuwa muislamu moja kwa moja.

Tatizo ni kwamba mnaposema mmeshakutana na "waarabu" wakristo wanaandika kiarabu. Mlitaka Waarabu waandike kwa kiswahili.

Ningewaona mna point japo kidogo mngetoa mfano wa Mtanganyika aandikae kiarabu naye sio Muislaam.

Nyie mmekezana wamisri, wairaq, wa lebanon, wasyria wakristo, Kwani ukristo ni lugha? Ikiwa hao wote ni waarabu wawe dini yoyote ile wakiandika Kiarabu cha ajabu ni nini?. Mkwawa alikuwa Mwarabu? Kimweri alikuwa Mwarabu? Hiyo ndio ajabu kwani inajulikana huku kwetu Waafrika waandikao kwa irabu za Kiarabu ni Waislaam.
 
FaizaFoxy bwana!! Irabu za kiarabu zilitumika kwanza kabla ya hizi za kirumi. Na sote tunafahamu kwamba Waarbu ndiyo walikuwa ni Wakoloni wetu wa pili baada ya Wareno ambao walitimuliwa na waarabu. Sasa lugha rasmi likuwa ni kiswahili na lugha za kienyeji zilizoandikwa katika Irabu za kiarabu. Mbona kitu rahisi lakini unataka kukifanya kionekane kigumu??
 
Naam, maana naona mengine tunarudi kule kule tu. NItafurahi sana kama inshallah siku moja tuweze kujadiliana kwa kina kitabu chako cha Sykes. Itakuwa ni heshma kubwa kwangu.

Na uombe radhi ukumbi kwa kupotosha aya za Qur'an kuandika isivyo. Mbona hili unalikimbia halafu unaitamka InshaAllah, halafu huyo huyo Allah aya zake unabandika utakavyo wewe, sijui tukueleweje?
 
Wewe nae huulizi maswali yanayoeleweka, unauliza unatoa maelezo mareeefu. Nenda moja kwa moja kwenye swali achana na maelezo mareefu.

Ohoo mama wa mizaha umeingia shift sasa upepo utabadilika. Hayo maelezo "mareeeefu" nia yake kuonesha contradictions zilizopo katika hoja husika hivyo kwa mtu wa kina kifupi sikutarajii kuona lolote. Katika post yangu moja niliuliza swali kwa sentensi moja tu lakini mpaka sasa bado sijajibiwa, hivyo kwa sasa nikiambiwa maelezo "mareeefu" najua tu jibu laweza kuwa ndio hitimisho.
 
Hoja yangu hapa ni kwamba Uislam au Ukristo siyo utakatifu wa kuhalalisha nafasi ya mtu kwenye jamii yetu. Kama tukiwa wakweli wakati huo wa kupigania uhuru bila watu wa kanda ya ziwa kukubali kuiunga mkono TANU leo hii ingewezekana kabisa historia ya nchi hii isingekuwa hivi.
Hewaaa! mkuu. Na tusisahau kuwa sisi tumetawaliwa kwa nyakati tofauti. Kuna maandiko yanayosema kila zama na kitabu chake. Kwa maana hiyo wakati wa mreno wapo walioongea kireno, ikaja waarabu, wajerumani na waingereza.

Kutokana na makala inaonyesha kuwa Sykes aliongea kijerumani vizuri sana, je hiyo inatosha kusema alikuwa mkristo! Platan alikataa kutumia jina la kijerumani nje ya watawala ikionyesha kuwa ni mazingira fulani yalimlazimisha kutumia jina hilo bila ridhaa ya moyo wake.
Vivyo hivyo walioandika kiarabu walikuwa na mazingira ya namna hiyo kwahiyo kuonekana kwa irab za kiarabu hakuna tofauti na Sykes kuongea kijerumani.

Tatizo ni kuwa hoja ikijijenga yenyewe haina utata, utata ni pale inapobandikwa ili ilete maana iliyokusudiwa. Tunakubaliana wapo wakristo walipinga harakati za ukoloni kama waislam walioshirikiana na mkoloni kumpiga mwislam mwenzao. Fair! Nisichokubaliana nacho ni kudanganya kuwa wapo waliokuwa watiifu wa nchi hii mwanzo hadi mwisho, halafu kuchukua sehemu ya historia na kuifanya kama ndiyo historia yote, na kuacha kwa makusudi kabisa pale panapokinzana na nafsi zetu au masilahi yetu.

Bishop Tutu alisimama Soweto, Jburg kulaani ubaguzi. Abel Muzorewa alisimama na Ian Smith kutetea ubaguzi. Ukimchomoa mmjoa na kuandika historia yake kwa ukristo wao ni kupotosha jamii kwasababu zipo pande mbili za shilingi.
 
FaizaFoxy bwana!! Irabu za kiarabu zilitumika kwanza kabla ya hizi za kirumi. Na sote tunafahamu kwamba Waarbu ndiyo walikuwa ni Wakoloni wetu wa pili baada ya Wareno ambao walitimuliwa na waarabu. Sasa lugha rasmi likuwa ni kiswahili na lugha za kienyeji zilizoandikwa katika Irabu za kiarabu. Mbona kitu rahisi lakini unataka kukifanya kionekane kigumu??

Kwanza kasome vizuri historia. Ulivyoeleza si sawa.

Halafu nisome vizuri nilivyoandika.

Tatu, hicho kiswahili chenyewe kinatokana na Kiarabu.

Mohamed Said Kasema Mkwawa alikuwa Muislaam na akiandika kiarabu. Sasa nyinyi njooni na ushahidi kama hilo mnapinga, isitoshe, pia kasema Kimweri alikuwa Muislaam, nalo pia njooni na ushahidi kama sivyo. Sio mnapinga tu bila ushahidi.
 
Taathira za wareno kututawala zinaonekana kwenye lugha ambayo wametuachia, maneno kama pesa (Pesso) Meza (Medza) na mengine. Wajerumani wao wametuachia jina adhimu la Shule (Schule) ingawa neno darasa linatokana na neno la kiarabu MadDrassa.Kiarabu ndiyo lugha yenye mchango mkubwa sana kwenye kiswahili hiki tulichonacho leo. Kiswahili ni kama Kiarabu na Kiarabu ni kama Kiswahili. kiarabu kina maneno mengi sana kwenye Lugha ya Kiswahili na athari za tamaduni za waarabu zinaonekana waziwazi kwenye Kiswahili na tamaduni zake. Pia tusiwasahau wahindi nao baada ya waarabu basi ni wao walifuatia. Maneno kama Sukari (sughari) Chai (Chae) na Gari (Gharri) yanatokana na lugha yao ya Kihindi.
 
Nina watu ambao wana credibility ya kulizungumzia hilo na Inshaalah kama itawezekana Jumatano nitakuwa hapa kusema hao wazee wangu wamesema nini.

Kila la kheri, but tunaomba utakaowauliza na vile vile uwaulize akina Muhammad bin Khalfan bin Khamis Al-Barwan a.k.a Rumaliza ni nani? Na wakupatie tarehe za Mkwawa kuanzia alivyozaliwa mpaka kufariki. Pia wakupatie details za watu wake wa karibu, rafiki ukoo na kadhalika. Kiufupi wakupatie taarifa zote ili ukirudi hapa uwe umekamilika mkuu ili uje kutujuza kwa uwazi zaidi kwani wengine hatuna tunu kama yako mkuu.
 
Mungu akijaalia!!
 
Kwanza kasome vizuri historia. Ulivyoeleza si sawa.

Halafu nisome vizuri nilivyoandika.

Tatu, hicho kiswahili chenyewe kinatokana na Kiarabu.

Mohamed Said Kasema Mkwawa alikuwa Muislaam na akiandika kiarabu. Sasa nyinyi njooni na ushahidi kama hilo mnapinga, isitoshe, pia kasema Kimweri alikuwa Muislaam, nalo pia njooni na ushahidi kama sivyo. Sio mnapinga tu bila ushahidi.

Mie nimewapatia Article imeandikwa na mzungu mwaka 1969 ikionyesha Mkwawa alipata daawa kutoka kwa wazee wa Tariqa. Na akawa undugu wa damu (urafiki wa damu) na moja wa watu wa tariqa ya Qadiriyya ambaye alimteua kuwa mshauri wake mkuu. Hata hivyo sio mbaya yeye akija na evidence zinazosema tofauti kwani mie nilikuwa nafahamu Mkwawa alikuwa hana dini (historia tuliyofundishwa na Tanu na CCM). Ila nimeona kwa Mohamed Said amesema alikuwa mwislamu akimtaja kuwa ukitaka habari zaidi za Mkwawa aulizwe Rumazila. Na pia nina articles mbali mbali za nje ya nchi zinazosema kuwa Mkwawa alikuwa mwislamu. Hivyo sio mbaya yeye akija na taarifa nzito za kutujuza zaidi.
 
Back
Top Bottom