Kigarama
JF-Expert Member
- Apr 23, 2007
- 2,492
- 1,230
Nadhani "mnakasha' umefika pazuri sasa. Utaona kwamba hata wale waliomuua Gaddaffi wenyewe pia hawakuwa na lengo moja mara tuu walipompata. Hata wakristo na waislamu wapo wema na wabaya. Huwezi kwa ujumla ukasema wakristo walikuwa na lengo la kudhulumu waislamu haki yao ya kuanzisha mapambano dhidi ya wakoloni.Nguruvi3,
Huo ndiyo ukweli kuwa Wamanyema, Wazulu na Wanubi waliingia Tanganyika kutoka nje na walikuwa watumishi wa Wajerumani na walipigana dhidi ya wazalendo wa nchi hii.
Hilo ni wazi kabisa.
Mabadiliko yalikuja kuletwa na watoto wao ambao walizaliwa katika utawala wa Waingereza. Naweka tena kwa faida ya wanaukumbi:
Hoja yangu hapa ni kwamba Uislam au Ukristo siyo utakatifu wa kuhalalisha nafasi ya mtu kwenye jamii yetu. Kama tukiwa wakweli wakati huo wa kupigania uhuru bila watu wa kanda ya ziwa kukubali kuiunga mkono TANU leo hii ingewezekana kabisa historia ya nchi hii isingekuwa hivi.