Nimechukua time kama nilivyoahidi na phew ! kuna mengi yamesemwa humu hadi kufikia kuchombeza kuwa Mag3 kakimbia mjadala ! Hili wazushi kama kawaida yao wamelirudia si mara moja, na haya ndiyo ninayoyaita porojo kama anayoyasimulia huyo anayejiita Mohamed Said. Mimi ni binadamu, naenda kibaruani, napumzika, nalala, naugua na ninasafiri - sikeshi hapa JF 24/7 kama FaizaFoxy, yeye yupo kibaruani na kwa mpango maalum, ambao hata hivyo sitasita kuwaambia ukweli, hautafanikiwa. Hautafanikiwa si hapa Tanzania ninayoijua fika toka kabla na baada ya uhuru kwani misingi aliyoijenga Mwalimu Nyerere ya upendo na amani bila kubaguana katu hawataweza kuivunja.
Ni porojo tu na kwa hakika zingeweza kupuuzwa kama tu hazikutolewa wakati huu. Hebu tuanze kwa kujiuliza kidogo tu, why now ? Wakati uongozi wote wa juu umeshikwa na Waislamu, kuna kikundi cha Waislaam wamepewa pasi kupita mikoani kupandikiza chuki miongoni mwa wananchi kwa kuchochea mifarakano ya kidini, why now ? Wakati viongozi wote wa juu wa serikali na chama tawala cha CCM ni Waislaam, kuna mchochezi kwa jina Mohamed Said amepewa pasi anaandika magazetini kuwa Baba wa Taifa kwa kuuchukia Uislaam, kwa makusudi aliwakandamiza Waislaam, why now ? Jibu lililo wazo kabisa hata kwa kipofu ni kwa sababu CCM inaelekea kupoteza imani miongoni mwa wananchi.
FaizaFoxy ni mfano halisi wa hali inayotubidi sisi sote wapenda amani wa nchi hii bila kujali dini wala kabila tupambane nayo bila kurudi nyuma. FaizaFoxy represents a symbol, an institution and a state sponsored legion which has all state resources at its disposal. FaizaFoxy hahitaji kulala, kula hata kwenda uani, anachohitaji ni kubadilisha umbo tu kidogo na naona sasa anatishia hata kuwaumbua kwa majina wachangiaji, mimi namwambia bring it on. Huu mpango waliokuwa nao hawa wachochezi umeanza zamani sana lakini kwa sababu ya taifa letu kujengwa katika misingi imara, kazi ya kuibomoa misingi hiyo imekuwa ngumu ila wamepata kaupenyo kadogo kwa kutumia Udini.
Mohamed Said represents a tool and a very convenient tool kwa sababu ni rahisi kuteka sehemu ya jamii kwa kutumia udini. Fikiria mtu anakubaliana na hoja kuwa serikali inayoongozwa na Waislaam inawadhulumu Waislaam hao hao kwa sababu inaongozwa kwa mfumoKristo ! Huu Mfumo Kristo unaowapa nafasi viongozi wote wa juu serikalini kuwa Waislaam kwa nia ya kuukandamiza Uislaam na kudhulumu Waislaam...!..kwa mtu asiye na upungufu wa akili, mambo mengine ni vigumu kuyaamini. Halafu "scholar" anayetoa madai haya eti sasa ameamua kuandika kitabu cha historia na rejea kuu ikiwa ni masimulizi ya wazee wake ambao kwa madai yao ndio waliopigania uhuru wa Tanganyika, upuuzi mtupu.
Nilionya kuwa hatari ya uwongo ukiachwa unarudiwarudiwa sana bila kukemewa, unaweza kujenga hisia potofu katika jamii kulingana na uwezo binafsi kuupokea bila tafakari. Katika huu mjadala tunawashuhudia watu kama hao na utawatambua tu wanavyomeza hizi hadithi za Mohamed Said na FaizaFoxy kuhusu chuki za Mwalimu dhidi ya Uislaam. Fikirieni jamani dai hili la Mwalimu kumwomba Gadafi hela ya kujenga msikiti halafu kukalia hizo hela (alizifisadi) hadi kufa kwake ndio msikiti ujengwe. Fikirieni hili la Mohaned Said kuwa Chifu Mkwawa alikuwa Muislaam na ndio maana alipambana na Wajerumani halafu kuna watu kama mazezeta wanaitikia chorus, huu kama si utumwa ni nini ?
Lakini narudia tena kusema hawa watu tusiwapuuze, wanayo ajenda na hiyo ajenda yao itafanikiwa tu kama Watanzania katika umoja, mshikamano na upendo tulionao bila kujali dini wala kabila (asante Mwalimu), hatutaupiga vita. Tahadhari ni kuwa tukiwapa nafasi wakafanikiwa basi, sisi kama taifa tumekwisha, tunayoyashuhudia yakitokea kwa mfano Somalia na kwingineko tutakuwa tumeyafungulia mlango. Labda tuanze kwa kujiuliza swali moja zito, wakati hizi mbegu za chuki zikipandwa mchana kweupee, usalama wa taifa uko wapi, serikali iko wapi na CCM iko wapi na kwa nini wako kimya ! Jibu mnalo wana jamvi, ukiona vyaelea vyaundwa na sasa vyarembwa.
Adam angeweza kuwa Muislaam sawa lakini si lazima baba yake Sapi alikuwa Muislaaam na kama na yeye pia alikuwa Muislaam si lazima babu yake Chifu Mkwama alikuwa Muislaam, ndivyo tulivyoishi bila kubaguana katika familia. Mfano mzuri mwingine ni Paul Bomani alikuwa Mkristo lakini baba yake mzazi alikuwa Muislaam au Bob Makani Mwenyekiti wa kwanza wa Chadema alikuwa Muislaam lakini ndudu zake wa kuzaliwa ni Wakristo. Tofauti na pwani huko bara mambo ni tofauti na ndiyo maana mimi nasema mtu wa pwani tena mzaliwa wa Gerezani asithubutu kudai anaandika historia ya wapigania uhuru wa Tanganyika, hapana, anaandika simulizi za wazee wake wa Gerezani, period.
Haya tuendelee........................