Mdondoaji,
Nitajibu maeneo mawili katika hoja zako;
Suala la kukataliwa kwa MoU ya sheikh Ponda linaanzia kwa mzee wetu al haj ali hassan mwinyi aliyekuwa raisi wakati hiyo proposal imepelekwa.
Lakini pili, juzi wakati kikwete anawaambia na ninyi pelekeni proposal yenu ili mpate ruzuku, hapo ndio palikuwa mahali muafaka pa kumweleza muislamu mwenzenu kwamba kuna proposal ya sheikh ponda tayari na serikali haijasema ina mapungufu gani!
Sasa ukituuliza sisi hapa sababu za kukataliwa kwa hiyo proposal ya sheikh ponda wakati ukifahamu kwamba serikali haikuwahi kutoa majibu inakuwa vigumu kukujibu.
Wandugu,
Kama kuna uwezekano wa kuweka hiyo proposal hapa jukwaani tuione .......halafu mwenye proposal ya Wakatoliki/Wakristo..........atuwekee ili tuidadavue tujue pumba ziko wapi na mchele uko wapi..........
serikali ni watu na watu ndio sisi..............kama proposal ilikataliwa naamini kabisa ilikuwa ni baada ya uchambuzi wa binadamu kama sisi hapa JF.....kwa hiyo ninaamini hiyo proposal ikiwekwa hapa tutaona kama ina mapungufu au ilikuwa "mfumokristo" kuweka ntimanyongo.....
NOTE: Kwa atakayeweka hiyo proposal hapa......tafadhali atuwekee the original version.........