Historia ya Uhuru isimuliwavyo na Mohammed Said yakosolewa

Historia ya Uhuru isimuliwavyo na Mohammed Said yakosolewa

Mohamed Said;2822965] Kigarama, Wako waloteguka mguu lakini Alhamdulilah si mimi
Ngoja tuangalaie kwa ufupi kama hujateguka
Mohamed Said;2822965][Ukitaka kupambana na mie katika haya ule ushibe na uage kwenu.
Wanohusika wako kimya mnajitahidi nyie wachezea pemben.

Mohamed Said;2824213]Mgalanjuka,Tatizo la udini wahusika wamelisikia.Hilo ndilo muhimu kwetu Waislam
Wahusika wapo kimya! wahusika wamelisikia
Mohamed Said;2823208]Sweke34,Sisi tuna "inferiority complex."ma?Nani kasema? Hivi wewe unavyosoma nyuzi zetu sie tumeelekea kuwa na "complex?"Hebu pitia nyuzi zangu na niambie wapi na kitu gani kimekupa hisia hiyo
Unaposema waislam wanafanywa second citizen una maana gani kama si inferiority complex. Unapoonyesha Nyerere peke yake alishinda baraza la wazee 170 na kamati kuu ya TANU hadi kusambaratisha umma ni nini kama si kuonyesha inferiority complex
East African Muslim Welfare Society (EAMWS) aliunda nani?Al Jamiatul Islamiyya aliunda nani?Au hujui kuwa ilihujumiwa na Nyerere akiwatuma akina Geofrey Sawaya mikoani kutoa milungura ili BAKWATA ipate viongozi?
EAMWS iliundwa na Agakhan, kijana wako Mdondoaji alileta nondo hapa. Wewe umeshadidia kuwa Agakhan alipoacha u-patron ikafa! na haijarudi ila kuna kamati nyingi na taasisi zisizo na idadi
Mohamed:Unamsimanga yatima asiye na baba wala mama kwa nini siku ya Eid hana nguo za kuvaa akenda Mnazi Mmoja kucheza kama wenzake?Hivyo si ndiyo unamkumbusha wazazi wake waliotangulia mbele ya haki?
Halafu unasema hakuna inferiority complex
Mohamed:Unatusimanga kwa shule mnazoziendesha kwa hela ya serikali (MoU)
Juzi Kikwete kafungua mradi wa umeme wa wakristo kule nyanda za juu. Ukimaliza hadithi kijana wako kama baru baru ataendeleza ulipoachia ya kuwa wenzetu wana MoU ya umeme! miaka inasonga mbele. Mohamed huoni kama hilo ni jibu unataka wahusika wakujibu nini zaidi.
Mohamed Said;2820949] Mambo yakawa yamevurugika zaidi kwa kuwa rais waEAMWS, Tewa Said na makamo wake Bibi Titi Mohamed walikuwa katika baraza lamawaziri la Nyerere na wakapoteza nyadhifa zao za ubunge katika uchaguzi mkuuwa mwaka 1965. Kwa ajili hii basiserikali ikawa inaeneza propaganda kuwa kwa kuwa Tewa na Bibi Titi walikuwa katika uongozi wa juu waEAMWS, walikuwa wanatumia nafasi zao kujijengea himaya mpya kutoka kwa Waislamdhidi ya Nyerere. Viongozi hawa ikawa lazima washughulikiwe na kuangamizwa. Mtuwa kufanya kazi hii hakuwa mwingine ila Adam Nasibu katibu wa EAMWS Bukoba,mwalimu wa shule ya msingi ambae elimu yake wala haikuwa kubwa
Kwani shehe Ponda anayeandika MoU anaelimu gani, hebu tusaidie kwa hili pia.

Umesahau kuwa kabla ya kupoteza kiti uliwahi kusema Tewa alipelekwa ubalozi wa China. Alikubali vipi akijua ni njama za kuua EAMWS.
Ukimuacha Nasibu aliyepewa kazi ya kuua EAMWS, Tewa alikuwa na role gani, Fundikira, Jumbe, Maswanya, Kawawa ushiriki wao ulikuwaje. Mbona historia ya Tanganyika inawaruka.
 
NARUDIA KUBANDIKA TENA HILI BANDIKO KWANI SIELEWI NI KWANINI FAIZAFOXY NA MOHAMED SAID HAWATAKI KUNIJIBU SWALI LANGU HILI.

Waislamu wana Nguzo zao tano wanazoziamini kama ndiyo msingi wa dini yao. Kama kweli waislamu wa Tanzania tangu Tanganyika walikuwa wanakandamizwa, ni nguzo ipi kati ya hizi tano ambayo waislam wa Tanzania wanakatazwa kuitimiza na Serikali kwa sababu serikali inadhibitiwa na MfumoKristu?

1. Kushahadia

2. Kuswali swala tano

3. Kufunga

4. Kutoa zaka

5. Kuhiji kwa mwenye uwezo

Kama waislamu wangekuwa wanakandamizwa katika hizo nguzo tano za uislamu ningeelewa hoja za MS. MS na wenzake watuambie ni wapi na ni lini waslamu walikatazwa kwenda kuhiji, kuswali. kufunga kwa Sunnah na Kufunga Ramadhani, kutoa zaka au kushahadia. Sijawahi kuona mfumo wa serikali ukikataza wakristo kusilimu au waislamu kujenga misikiti au kuadhini. Naijua misikiti ambayo iko katikati ya makazi ya watu kwenye mchanganyiko wa wakristo na waislamu na sijawahi kusikia serikali ikikataza waislamu kuadhini kwa sababu 'wanawasumbua" wasio waislamu kwa adhana zao.

Waislamu wanapotaka kwenda Mecca kuhiji hakuna siku walikatazwa kwenda badala yake serikali mara kadhaa imewahi kutoa fedha kusaidia waislamu kwenda kuhiji, sasa hapo waislamu wanakandamizwaje na huo mfumokristu na inakuwaje mfumokristu unashindwa kuzuia waislamu kuhiji, kusilimisha wakristo au kuadhini?

Hivi karibuni serikali si ilishawahi kutoa zaidi ya Shilingi Bilioni 2 kusafirisha mahujaji kwenda Mecca kuhiji? Kanisa lilikuwa wapi kuizuia serikali kutoa fedha hizo??
kuna shughuli nyingi za Waislam zimekwama ikiwa ni pamoja na ujenzi wa baadhi ya Miskiti kwa kisingizio cha Al-qaida. Mifano hai ipo mingi lakini hebu angalia tamko la Maaskofu kupinga OIC na Mahakama ya Qadhi na Serikali kuwafatisha!
 
Mkuu Barubaru, shukurani kwa darsa ulilo nipa nakuomba usinichoke, nini kinakwamisha masheikh wapande hizo mbili wasikae pamoja na kulitatua tatizo?Huoni chuki na ubaguzi unaopandikizwa na mzee Mohamed unazidi kuwagawa waislam?Kama masheikh wa BAKWATA wanadharauliwa hivyo kwamba wao sio masheikh wa wawaislam sasa kumbe ni wawakristo au wasisi "atheists"? Unasababu ipi kunishutumu kwamba nachagua maneno mawili kukukosoa, wakati wewe ndie unae wabagua waislam wenzako?
Mvurugaji ww. Huna cha maana unachoongea. Unachukuwa nusu ya sentensi unaitafsiri utakavyo! 'out of context' nani kakuambia ni Masheikh wa wakristo? Au......
 
Mkuu Kikwebo, ashakumu si matusi, amakweli nyani haoni kundule - unawezaje kumtuhumu mwanamijiji kwamba anatumia ID mbalimbali kama vile Nguruvi3,Wild Card,Mag3 et.al na ukashindwa kumutuhumu mzee Mohamed Said kuwa naye anatumia ID ya ritz, Faiza,Barubaru na Mdondoaji kujenga na kueneza hisia zake za chuki kwa kutumia imani ya dini ya kiislam? Lakini sikushangai hata kidogo kwa sababu sumu ya ubaguzi ya mzee Mohamed Said imekutafuna kiasi kwamba husikii wala huambiwi jingine. Ubaya nikwamba ubaguzi wa kidini umemtafuna hata yeye mwenyewe mzee Mohamed kiasi kwamba ameanza kuwabagua hata waislam wenzake, kwake yeye waislam ni wale tu wanao shabikia mihadhara yake na wale wanao hudhuria sherehe za idd chini ya BAKWATA hao kwake sio wenyewe, kwani hao wapo kula wali na chai ya ikulu. Hii ndio taabu ya ubaguzi.
Hayo ndio matunda aliyotuachia Nyerere. Alitutoa kwenye umoja wa EAMWS akatuundia na kutuachia BAKWATA na ubaguano na migogoro lukuki mpaka leo!
 
kuna shughuli nyingi za Waislam zimekwama ikiwa ni pamoja na ujenzi wa baadhi ya Miskiti kwa kisingizio cha Al-qaida. Mifano hai ipo mingi lakini hebu angalia tamko la Maaskofu kupinga OIC na Mahakama ya Qadhi na Serikali kuwafatisha!

Kama kuna mifano mingi si ungetoa hata mmoja? Lakini pia ufahamu mambo ya Al Qaida yameanza wakati Nyerere ni marehemu tayari. Kuna jambo la maana la kujiuliza, misikiti iliyopo haitoshelezi, tatizo la waislam linalolalamikiwa na Mohamed Said ni ukosefu wa sehemu za kuabudia za Waislam?

Mimi ninavyoelewa ni kwamba watu wengi wanaopinga kujiunga na OIC hoja yao kubwa ni kwamba OIC kuna kipengele ambaocho kinataka mwanachama wake awe ni nchi yenye kuhimiza ujenzi wa dini ya Kiislam au ni nchi ya Kiislam kupitia serikali.

Wakati fulani Mohamed na wenzake walikuwa wanadai mbona Vatican wana ubalozi hapa nchini kwa nini OIC wanazuiliwa. Mimi si mkatoliki lakini katika vitu ninavyoelewa ni kwamba Vatican ni nchi lakini inayoendeshwa kidini kama ilivyo kwa Iran, Saudi Arabia, Uingereza au Uturuki. Haitakuwa ajabu kwa Saudi Arabia kuleta Balozi wake akiwa na sifa ya Ulamaa. Vatican ni nchi na OIC ni shirika la Kiislam linalohimiza ujenzi wa Uislam kupitia serikali, na sisi tunataka serikali yetu isijuhusishe na ujenzi wa dini yoyote ile.

Katika watu wanaounga mkono uanzishwaji wa mahakama ya Kadhi mimi ni mmojawapo. Lakini pia katika watu wanaopinga mahakama ya Kadhi kuingizwa kwenye katiba yetu mimi ni mmojawapo. Wakristo wanasheria yao ya kanisa ya mambo ya ndoa inayosema kwamba "alichokiunganisha mungu, mwanadamu hatengeui" lakini kwa sababu sheria hiyo ya kanisa haitambuliwi na katiba yetu, hao hao waliofunga ndoa kanisani wakienda kwenye mahakama za kawaida za serikali ndoa yao inatenguliwa. Kanisani watatengwa na hawataruhusiwa kuoana tena nje ya ndoa yao ya awali, lakini kwa sheria ya nchi ndoa yao haipo tena na wanaruhusiwa kuoana na mtu mwingine.

Jamii yetu imechanganyikana sana, tunataka mahakama ya kadhi iwe na nguvu kwenye misikiti lakini siyo kwenye kila nyanja ya maisha ya watanzania. Hebu fikiria kuna mwanamke ameishi na mume wake kwa miaka 20 na kuchuma mali mbali mbali, lakini mume huyo anataka waachane na anapeleka Kesi yake kwenye Mahakama ya Kadhi inayotambuliwa na Katiba, mwanamke si muislam. Haki ya huyo mwanamke itallindwa vipi na mahakama ya Kadhi wakati katiba inatamka masuala yote ya ndoa za waislam yatashughulikiwa na Mahakama ya Kadhi wakati mwanamke mwenyewe si muislam?
 
Ngoja tuangalaie kwa ufupi kama hujategukaWahusika wapo kimya! wahusika wamelisikiaUnaposema waislam wanafanywa second citizen una maana gani kama si inferiority complex. Unapoonyesha Nyerere peke yake alishinda baraza la wazee 170 na kamati kuu ya TANU hadi kusambaratisha umma ni nini kama si kuonyesha inferiority complexEAMWS iliundwa na Agakhan, kijana wako Mdondoaji alileta nondo hapa. Wewe umeshadidia kuwa Agakhan alipoacha u-patron ikafa! na haijarudi ila kuna kamati nyingi na taasisi zisizo na idadi Halafu unasema hakuna inferiority complex Juzi Kikwete kafungua mradi wa umeme wa wakristo kule nyanda za juu. Ukimaliza hadithi kijana wako kama baru baru ataendeleza ulipoachia ya kuwa wenzetu wana MoU ya umeme! miaka inasonga mbele. Mohamed huoni kama hilo ni jibu unataka wahusika wakujibu nini zaidi.Kwani shehe Ponda anayeandika MoU anaelimu gani, hebu tusaidie kwa hili pia.

Umesahau kuwa kabla ya kupoteza kiti uliwahi kusema Tewa alipelekwa ubalozi wa China. Alikubali vipi akijua ni njama za kuua EAMWS.
Ukimuacha Nasibu aliyepewa kazi ya kuua EAMWS, Tewa alikuwa na role gani, Fundikira, Jumbe, Maswanya, Kawawa ushiriki wao ulikuwaje. Mbona historia ya Tanganyika inawaruka.

Nguruvi3,

Itakuwa tunazunguka humo humo.

Mimi nilokusudia nimelitimiza Alhamdulilah.
Historia ya kweli ya TANU nimeiandika, ipo na inasomwa vyuo vyote duniani wanakosomesha historia ya Afrika na Uislam.

Ndani yake nimeandika sehemu nzima ambayo ndiyo mwisho wa kitabu changu: "Njama Dhidi ya Uislam."
Watu wanaisoma na wameelewa mengi kuhusu nchi hii.

Kitabu hiki kimenifanya nitambulike ndani na nje ya mipaka yetu.

Nimezungumza Kenyatta University, University of Ibadan, University of Johannesburg, Marekani nk. na wanafunzi wa Kiislam katika vyuo vyote Tanzania wamenialika na nimezungumza, shule za Kiislam ndiyo usiseme kila siku mialiko inamiminika.

Nilichokusudia kimekamilika Waislam sasa wanaelewa hali ilivyo nchini kwetu.
Wewe halikadhalika naamini umejifunza kitu katika kujadiliana na mimi kama mie nilivyojifuza kutoka kwenu.

Kubwa nililojifunza ni kuwa hamuamini au akili tu inakataa kuamini.

Sina la zaidi.

Mohamed
 
Tanzania na Tanganyika kuna madhehebu mbalimbali ya Kiislamu, Kihindu na Kikristu ambayo yalitofautiana kimtazamo na kimchango wakati wa enzi za Tanganyika kudai uhuru. Kuna madhehebu ya Kiislamu kama Dawood Bohra, Shia Ithnasheri, Ismailia, n.k. ambayo Waumini wake wengi walipinga Tanganyika kupewa uhuru kutokana na faida za mfumo wa upendeleo uliokuwapo enzi hizo ambapo Wahindi walikuwa juu ya Waafrika kwenye nyanja zote za kijamii, kisiasa, kiutamaduni, n.k., lakini JKN alikuwa na busara tosha za kuwajumuisha watu kama Al Noor Kasoom na Amir Jamal, ambao walikuwa Wai-Ismailia (kama sikosei) kwenye serikali yake baada ya uhuru. Jee, Mohamed Said ana hoja gani kuhusu hili?

Ndjabu,

Si kama mie najua kila kitu.

Mohamed
 
Swali labda lipelekwe mbele zaidi. Wanapowaita ni "second class citizens" wanawapimia nini? Dini yao, hali yao ya maisha, elimu yao, utajiri au kitu gani?

a. Haiwezi kuwa dini - kwa sababu hakuna nafasi yoyote nchini ambayo Muislamu amewahi kukataliwa kuishika. NONE.
B. Haiwezi kuwa elimu - kwa sababu wapo Waislamu wengi waliosoma na wanaoendelea kusoma nchini na hakuna shule yoyote ambayo inakataza - kama kanuni au mfumo - Waislamu kuingia isipokuwa zile ambazo zimetengwa kwa ajili ya mafunzo ya kiroho ya waumini wa dini hizo.
c. Haiwezi kuwa hali - kwa sababu hali ya maisha inawakuta Wakristu sawasawa na Waislamu, Wapagani sawasawa na wenye kuamini imani nyingine.
d. Haiwezi kuwa utajiri - kwa sababu hakuma Muislamu tajiri ambaye amenyang'anywa utajiri wake au kukatazwa asiwe tajiri kwa sababu ni Muislamu.

Kwa hiyo, huu 'usecond class' tunaoambiwa ambao unaimbwa kuwafanya Waislamu watembee kwa aibu kwenye nchi yao au kujiona kuwa 'hawalingani' unatokana na nini? Utaona kuwa karibu mara zote ni viongozi wa Kiislamu au Waislamu viongozi ambao hutoa kauli zenye kuwafanya Waislamu wajione duni.

"Waislamu someni kama Wakristu"
"Waislamu tukuzeni elimu"
"Waislamu kwanini nyini nanyi msiombe MoU kama Wakristu"
"Waislamu... "

Hakuna kiongozi Mkristu ambaye amewahi kutoa kauli za namna hii. Cha kushangaza viongozi wanaosema hivyo ni Waislamu! Sasa kwanini wanataka wenzao wajione duni?

MM,

Kama kawaida kupata mantiki katika maandishi yako "is like looking for a needle in a hay stack."

Ntakujibu moja niloelewa.

Mwembechai wameuliwa Waislam sheria inasema kwa vifo kama vile lazima "Inquest" ifanyike.
Serikali imekataa kufanya "Inquest" hadi leo.

Kauliwa mbwa jina lake Immigration.
Kesi imekwenda mahakamani.

Mbwa kapewa thamani kuliko Muislam.

Do I need to say more?

Mohamed
 
Kama kawaida Mohamed anataka kukwepa swali la msingi. Swali ni kuwa, kwa vile waislam waliikataa BAKWATA kuanzia enzi hizo(ingawa imekubalika miaka yote na wengi) Je ni chombo gani kinawakilisha waislam sasa hivi nje ya BAKWAT. Hili ndilo swali analopaswa kulijibu.

Pili, Mohamed usidanganye watu au kufanya propaganda. Majuzi Kikwete alipohudhuria baraza la Idd, lilikuwa limeandaliwa na BAKWATA. Watu wameona. Shughuli za BAKWATA bado zipo na hili la kusema Mohamed Said yupo starlight ni majigambo.
Ni ukweli kwa kuwa watakaohudhuria ni watu wa Gerezani na Tandamti kama ambavyo walikwenda kumuangalia George Weah shule ya uhuru akifanya mazoezi. Sasa sijui na hiyo tusemeje.

Ni nani huko Kilwa anamjua Mohamed Said? Watu wamepigwa na dhiki na wanachotaka ni kujiondoa na balaa hilo la umasikini. Ukimwambia anunue mwananchi ni tusi, sasa leo Mohamed anasema waislam wa Tanzania. Ni hadithi ile ile ya wapigania uhuru wa Tanganyika wasiojua Iringa au Moshi.

Anyway, turudi kwenye swali la msingi la taasisi inayowakilisha waislam. Haitoshi kusema sisi, sisi ni akina nani.

Nguruvi3,

Waswahili tuna msemo, "Usilojua usiku wa kiza."

Mohamed

"On 28 April, 1993 bizarre occurrence took place. Indesperation and in its effort to salvage BAKWATA the Minister of Home Affairsand Deputy Prime Minister Augustine Mrema convened a meeting between Muslimsand Christians at the Diamond Jubilee Hall, Dar es Salaam. The agenda was not known.The Church sent a strong delegation. Muslims abstained except BAKWATA. The fewMuslims who turned up were there out of curiosity rather than conviction that the meeting would bear fruits. When the time for introduction between the two parties came, Muslims present at the meeting refused to shake hands with the Church leadership. This was an embarrassment to the government propaganda machinery sent to the meeting by the Christian Lobby to record and broadcast the event. Mrema addressed the meeting in which in his speech it was revealed that elections for BAKWATA were long overdue and could not be held because of lack of funds. The Church volunteered to provide money to BAKWATA to enable it hold its elections. The Minister for Home Affairs Augustine Mrema also helped to collect money from the business community to fund BAKWATA elections."
 
MM,

Kama kawaida kupata mantiki katika maandishi yako "is like looking for a needle in a hay stack."

Ntakujibu moja niloelewa.

Mwembechai wameuliwa Waislam sheria inasema kwa vifo kama vile lazima "Inquest" ifanyike.
Serikali imekataa kufanya "Inquest" hadi leo.

Kauliwa mbwa jina lake Immigration.
Kesi imekwenda mahakamani.

Mbwa kapewa thamani kuliko Muislam.

Do I need to say more?

Mohamed
Muislam ni binadamu kwanza, kwa hiyo binadam wanaouliwa na serilkali hii ni wengi mno. Bulyankulu, Pemba, wafanyabiashara wa madini wa Mahenge, dereva aliyeuawa na Dittopile, Mererani, mgodi wa North Mara kwa sumu toka kwenye mgodi inayoingia kwenye maji yanayonywewa na mifugo na binadamu. orodha ni ndefu Mohamed.

Mauaji haya tukiyaangalia kwa jicho la udini hatuwezi kufika popote. Hii serikali lazima tuibane iache kuua wato hovyo hovyo.
 
Nguruvi3,

Waswahili tuna msemo, "Usilojua usiku wa kiza."

Mohamed

. Muslims abstained except BAKWATA.
Is BAKWATA not a Muslim organization? Ndiyo maana watu wanakuuliza waislam ni wale tu unaowakubali wewe au ni wale wanaokubaliwa na Mwenyezimugu kwa misingi ya dini ya Kiislamu kwa kufuata Quran Tukufu?
 
Kama kuna mifano mingi si ungetoa hata mmoja? Lakini pia ufahamu mambo ya Al Qaida yameanza wakati Nyerere ni marehemu tayari. Kuna jambo la maana la kujiuliza, misikiti iliyopo haitoshelezi, tatizo la waislam linalolalamikiwa na Mohamed Said ni ukosefu wa sehemu za kuabudia za Waislam?

Mimi ninavyoelewa ni kwamba watu wengi wanaopinga kujiunga na OIC hoja yao kubwa ni kwamba OIC kuna kipengele ambaocho kinataka mwanachama wake awe ni nchi yenye kuhimiza ujenzi wa dini ya Kiislam au ni nchi ya Kiislam kupitia serikali.

Wakati fulani Mohamed na wenzake walikuwa wanadai mbona Vatican wana ubalozi hapa nchini kwa nini OIC wanazuiliwa. Mimi si mkatoliki lakini katika vitu ninavyoelewa ni kwamba Vatican ni nchi lakini inayoendeshwa kidini kama ilivyo kwa Iran, Saudi Arabia, Uingereza au Uturuki. Haitakuwa ajabu kwa Saudi Arabia kuleta Balozi wake akiwa na sifa ya Ulamaa. Vatican ni nchi na OIC ni shirika la Kiislam linalohimiza ujenzi wa Uislam kupitia serikali, na sisi tunataka serikali yetu isijuhusishe na ujenzi wa dini yoyote ile.

Katika watu wanaounga mkono uanzishwaji wa mahakama ya Kadhi mimi ni mmojawapo. Lakini pia katika watu wanaopinga mahakama ya Kadhi kuingizwa kwenye katiba yetu mimi ni mmojawapo. Wakristo wanasheria yao ya kanisa ya mambo ya ndoa inayosema kwamba "alichokiunganisha mungu, mwanadamu hatengeui" lakini kwa sababu sheria hiyo ya kanisa haitambuliwi na katiba yetu, hao hao waliofunga ndoa kanisani wakienda kwenye mahakama za kawaida za serikali ndoa yao inatenguliwa. Kanisani watatengwa na hawataruhusiwa kuoana tena nje ya ndoa yao ya awali, lakini kwa sheria ya nchi ndoa yao haipo tena na wanaruhusiwa kuoana na mtu mwingine.

Jamii yetu imechanganyikana sana, tunataka mahakama ya kadhi iwe na nguvu kwenye misikiti lakini siyo kwenye kila nyanja ya maisha ya watanzania. Hebu fikiria kuna mwanamke ameishi na mume wake kwa miaka 20 na kuchuma mali mbali mbali, lakini mume huyo anataka waachane na anapeleka Kesi yake kwenye Mahakama ya Kadhi inayotambuliwa na Katiba, mwanamke si muislam. Haki ya huyo mwanamke itallindwa vipi na mahakama ya Kadhi wakati katiba inatamka masuala yote ya ndoa za waislam yatashughulikiwa na Mahakama ya Kadhi wakati mwanamke mwenyewe si muislam?

Kigarama,

ndio maana waswahili wanasema Usilo lijua ni kama usiku wa kiza. Fanya siku moja utembelee nchi ya Vatican kisha uangalie yafuatayo:
1. Je nchi hiyo ina raia gani na idadi yake na eneo lake.
2. Je ina wanawake wangapi?
3. Je ina watoto chini ya miaka 10 wangapi?
4. Je hao mabalozi wake wanaowakilisha nchi hiyo ni raia wa nchi gani?
5. Kiongozi wake anapatikananje na anachaguliwa na raia wa nchi gani?

Jaribu hata kupitia kwenye mtandao kisha utajua Vatican ni nini?
 
Is BAKWATA not a Muslim organization? Ndiyo maana watu wanakuuliza waislam ni wale tu unaowakubali wewe au ni wale wanaokubaliwa na Mwenyezimugu kwa misingi ya dini ya Kiislamu kwa kufuata Quran Tukufu?

Kigarama,

Nakuelewa sana na swali hili nimeulizwa mara nyingi tena na rafiki zangu Wakristo kwa nia njema kabisa.
Hujitahidi kuwaeleza BAKWATA imeanzishwa na nani na katika mazingira gani kama nilivyoeleza humu ukumbini.
Wengi wao hupigwa na butwaa.

Nikiwaeleza kuwa vyombo vya serikali, Usalama wa Taifa na Polisi walitumika kuiweka BAKWATA madarakani.

Watu wakahongwa kuieneza BAKWATA kwao ni mambo mapya sana.

Wanashindwa kuelewa.

Ninawaeleza habari za EAMWS. Habari za Sheikh Hassan bin Amir kama kiongozi wa Waislam juhudi zake katika kupigania uhuru wa Tanganyika. Mradi wa kujenga Chuo Kikuu nk. nk.

Nikifika hapa ndiyo kabisa nimewachanganya.

Unategemea nini ikiwa mtu kama Prof. Haroub baada ya kusoma kitabu changu akawa kataabika kiasi cha kumwendea Nyerere na Ahmed Rashad Ali kuhakikisha maneno yangu.

Kwa Mkristo yoyote haya kwake ni mambo yako mbali sana na yeye.

Lakini fanya utafiti wako mwenyewe kuhusu BAKWATA ikiwa una uwezo huo.
Utajua.

Hivi sasa nina darsa kuhusu BAKWATA...fatilia na ubongo wako uache wazi usikie yale ambayo hukuwa unayajua.

Mohamed
 
Muislam ni binadamu kwanza, kwa hiyo binadam wanaouliwa na serilkali hii ni wengi mno. Bulyankulu, Pemba, wafanyabiashara wa madini wa Mahenge, dereva aliyeuawa na Dittopile, Mererani, mgodi wa North Mara kwa sumu toka kwenye mgodi inayoingia kwenye maji yanayonywewa na mifugo na binadamu. orodha ni ndefu Mohamed.

Mauaji haya tukiyaangalia kwa jicho la udini hatuwezi kufika popote. Hii serikali lazima tuibane iache kuua wato hovyo hovyo.

Kigarama,

Nakuelewa.
Mauaji ya Mwembechai nia sawasawa na mauaji ya North Mara...

Katika kitabu cha Mwembechai Killings kuna maelezo ya Zahaki ambae alikuwa polisi wakati wa operesheni ya Mwembechai. Mahojiano yale nilimfanyia mimi.

Tafadhali yasome kisha Insha Allah rejea tuzungumze.

Kuna msemo, "Mvaa kiatu ndiye ajuae wapi kinabana."

Mohamed

PS: Kiswahili kizuri ni "ovyo" siyo "hovyo"

Tuendelee na darsa...:

"Wakazi wa Dar es Salaam kila mwaka walikuwawakifanya maulidi katika viwanja vya Mnazi Mmoja kuadhimisha kuzaliwa kwa MtumeMuhammad (SAW). Huu ndiyo toka asili ulikuwa uwanja ambao TANU ilifanyamikutano yake yote wakati wa kupigani uhuru. Mwezi Juni 1968 maulidi mbilikatika usiku mmoja zilisomwa kuadhimisha kuzaliwa kwa Mtume (SAW). Maulidi moja ilisomwa Mnazi Mmoja na nyingineIlala. Chanzo cha haya yote ni kuwepo kwa kutoelewana kati ya viongozi waWaislam waliokuwa wanajiona kuwa ni ëwazalendoí wafuasi wa TANU na wale na waleviongozi wa EAMWS ambao kambi nyingine ilikuwa ikiwaona kama wapinzani wa TANU.Yale maulidi yaliyosomwa Ilala yalihudhuriwa na viongozi wa EAMWS na yalipatawatu wengi na yakafana sana ukilinganisha na yale maulidi ya Mnazi Mmoja, yawafuasi wa TANU. Uongozi wa TANU ulitishika na hali hii iliyokuwa ikijitokezakwa maana ilikuwa inaonyesha kuwa chama kilikuwa kinapoteza wafuasi ambao walikuwa wakijiunga na kambi ya Tewa na Titi iliyokuwaikisemekana ipo dhidi ya Nyerere. [1]Tarehe 17 Oktoba, 1968, Adam Nasibu akatokeatena katika magazeti lakini sasa hakuwa tena mgeni machoni mwa watu, alikuwaanafahamika kama katibu mwenye hamasa za siasa wa EAMWS kutoka Bukoba ambaealiunga mkono Azimio la Arusha na kutoa maelekezo kwa viongozi wengine waKiislam akieleza vipengele vya azimio hilo. Adam Nasibu alitangaza kupitiaradio ya serikali na na magazeti ya TANU kuwa mkoa wake, Bukoba unajitoa kutokaEAMWS.[1]Ghafla Adam Nasibu akawa mtu mashuhuri wa kufahamika nchi nzima, magazeti yaTANU na radio ya serikali ikaanza kumjenga haiba yake pamoja na kuutangaza kilekilichokuja kujulikan kama ëmgogoroí wa Waislam. Magazeti ya TANU chini yaBenjamin Mkapa yakawa yamepata habari ya kushabikia: ëRadio ya serikali namagazeti ya TANU kwa pamoja yanatoa habari kwa uzito wa hali ya juu kuhusukuhusu kujitoa kwa Bukoba katika EAMWS. Magazeti ya TANU yakiwa yameshehezavichwa vya habari na maelezo ya mgogoro na picha za Adam Nasibu zikipambakurasa zake za mbeleí. [1]Ilikuwa baada ya magazeti na radio kutangaza nakuandika habari hizo ndipo Waislam kwa mara ya kwanza wakaja kutanabahi kuwawalikuwa wanakabiliwa na ëmgogoroí mkubwa wa nchi nzima. Lakini matatizoyalikuwa yameanza hasa toka siku ile watu wa Dar es Salaam waliposoma maulidimbili mwezi wa Juni, 1968. Siku tano baadae, yaani tarehe 22 Oktoba, SheikhJuma Jambia mwanakamati wa halmashauri kuu ya EAMWS kutoka Tanga na yeyeakatangaza kuwa Tanga inajitoa katika EAMWS. [1] Mwenyekiti wa EAMWS TewaSaid Tewa akamfahamisha Sheikh Jambia kuwa uamuzi wake ulikuwa ni uamuzi wa mtummoja. Jibu la Sheikh Jambia lilikuwa ni kutoa taarifa kwa vyombo vya habarikuvifahamisha uamuzi huo. Sheikh Jambia alitoa taarifa hiyo pamoja na mtu mmojaliyefahamika wa jina la Abdi Matunga. Haukupita muda mrefu, Iringa nayoikatangaza kuwa inajitoa kutoka EAMWS.Uongozi wa EAMWS kwa haraka ukaitisha mkutanokujadili hali ile mpya iliyojitokeza. Vyombo vile vya habari, Uhuru na TheNationalist ambavyo vilikuwa vikitumikia wale waliokuwa wanaodai kujitenga naEAMWS, sasa vikawa havitaki kutoa au kuandika habari za viongozi wa EAMWS ambaowalikuwa wanapigania umoja wa Waislam. Hapa ikawa ni wazi kuwa serikali ilikuwainatumia vyombo vya habari, yaani magazeti yaliyokuwa chini ya TANU na radio yaserikali kuwahujumu Waislam na EAMWS. Uongozi wa EAMWS ulipokuja kutanabahi ninani walikuwa nyuma ya hujuma ile wakawa wamebaini hatari iliyokuwaikiwakabili, kwa ajili hii basi waliwageukia Waislam kutaka msaada wao."

Mohamed
 
MM,

Kama kawaida kupata mantiki katika maandishi yako "is like looking for a needle in a hay stack."

Ntakujibu moja niloelewa.

Mwembechai wameuliwa Waislam sheria inasema kwa vifo kama vile lazima "Inquest" ifanyike.
Serikali imekataa kufanya "Inquest" hadi leo.

Kauliwa mbwa jina lake Immigration.
Kesi imekwenda mahakamani.

Mbwa kapewa thamani kuliko Muislam.

Do I need to say more?

Mohamed

Serikali imefanya inquest kwa mauaji ya Arusha au waliokufa Arusha siyo Watanzania? Imefanya inquest Nyamongo au waliokufa siyo Watanzania? Wamepigwa juzi watu Iringa na Mbeya umesikia serikali imefanya inquest au investigation yoyote? Kwanini unaulizia kwa kulinganisha Waislam na tukio la kuuliwa kwa mbwa? yaani umeshindwa kulinganisha Waislamu na Watanzania wenzao wa Arusha, Nyamongo, Bulyanhulu, Geita na Tarime (ambako wote huko Watanzania wamuawa mikononi mwa polisi) umeamua kulinganisha na lile tukio la mbwa Sumbawanga? Really?

Au unaumwa kwa kuuliwa Waislamu kuliko kuuliwa kwa Watanzania (bila kujali dini zao)? Kama aliyeuliwa na Polisi ni John wewe hutosema kitu lakini ukisikia ni Juma unakuja juu? Really?
 
Mkuu Barubaru, shukurani kwa darsa ulilo nipa nakuomba usinichoke, nini kinakwamisha masheikh wapande hizo mbili wasikae pamoja na kulitatua tatizo?Huoni chuki na ubaguzi unaopandikizwa na mzee Mohamed unazidi kuwagawa waislam?Kama masheikh wa BAKWATA wanadharauliwa hivyo kwamba wao sio masheikh wa wawaislam sasa kumbe ni wawakristo au wasisi "atheists"? Unasababu ipi kunishutumu kwamba nachagua maneno mawili kukukosoa, wakati wewe ndie unae wabagua waislam wenzako?

Gwalihenzi,

Kama nilivyo kudarsisha huko nyuma. Bakwata ni chombo cha Serikali ya Tz ambacho kimeundwa maalum na mahsus kabisa kuthibiti waislam. Na nikakwambia hata mfumo wake ni sawa sawa na ule wa Serikali, Sheikh wa mkoa, wilaya, kata , tarafa n.k. Na kila serikali inapofanya ima kuongeza mikoa na wilaya nao wanaongezeka sambasamba nao. Hivyo hicho ni chombo kama kilivyo chombo kingine cha Serikali. na ndio maana wanaitwa Sheikh wa Bakwata wa Mkoa, au wilaya n.k na sio sheikh wa waislam wa masjid fulani au sheikh wa masjid fulani.

Ni vigumu sana kuwachanganya hawa wawili kwani Waislam wanafuata Qur,an na Sunna za Rasul Mohamad tu Lakin bakwata wameongeza na Serikali kama wafadhili wao na wanaowaweka madarakani ikiwa pamoja na mali walizorithishwa na Serikali mali za EAMWs.

Hiyo ni sawa na kanisa katoliki kukataa kuungana na makanisa mengine ndani ya Tz. Na ndio maana anapoapishwa Rais wa Tz utaona kuna kiongozi wa muungano wa makanisa Tz na kiongozi wa kanisa Katoliki. Hao wote ni wafuasi wa Yesu lakini huwezi kuwachanganya.
 
Kigarama,

ndio maana waswahili wanasema Usilo lijua ni kama usiku wa kiza. Fanya siku moja utembelee nchi ya Vatican kisha uangalie yafuatayo:
1. Je nchi hiyo ina raia gani na idadi yake na eneo lake.
2. Je ina wanawake wangapi?
3. Je ina watoto chini ya miaka 10 wangapi?
4. Je hao mabalozi wake wanaowakilisha nchi hiyo ni raia wa nchi gani?
5. Kiongozi wake anapatikananje na anachaguliwa na raia wa nchi gani?

Jaribu hata kupitia kwenye mtandao kisha utajua Vatican ni nini?

Nijue kitu gani tena wakati kwenye bandiko langu nimeandika kwamba Vatican ni nchi lakini inayotawaliwa kidini. Ni aina gani ya nchi au watu wanaoishi humo au idadi ya wanawake waliopo mabaozi wake ni wa nchi gani. Ninajua ni aina gani ya nchi ambayo Vatican inatambuliwa na ninajua ni kwanini Vatican ina sifa hizo ambazo ni za "kipekee" duniani. Wao ni kanisa lakini pia ni nchi.
 
Kigarama,

Nakuelewa.
Mauaji ya Mwembechai nia sawasawa na mauaji ya North Mara...

Katika kitabu cha Mwembechai Killings kuna maelezo ya Zahaki ambae alikuwa polisi wakati wa operesheni ya Mwembechai. Mahojiano yale nilimfanyia mimi.

Tafadhali yasome kisha Insha Allah rejea tuzungumze.

Kuna msemo, "Mvaa kiatu ndiye ajuae wapi kinabana."

Mohamed

PS: Kiswahili kizuri ni "ovyo" siyo "hovyo"

Tuendelee na darsa...:

"Wakazi wa Dar es Salaam kila mwaka walikuwawakifanya maulidi katika viwanja vya Mnazi Mmoja kuadhimisha kuzaliwa kwa MtumeMuhammad (SAW). Huu ndiyo toka asili ulikuwa uwanja ambao TANU ilifanyamikutano yake yote wakati wa kupigani uhuru. Mwezi Juni 1968 maulidi mbilikatika usiku mmoja zilisomwa kuadhimisha kuzaliwa kwa Mtume (SAW). Maulidi moja ilisomwa Mnazi Mmoja na nyingineIlala. Chanzo cha haya yote ni kuwepo kwa kutoelewana kati ya viongozi waWaislam waliokuwa wanajiona kuwa ni ëwazalendoí wafuasi wa TANU na wale na waleviongozi wa EAMWS ambao kambi nyingine ilikuwa ikiwaona kama wapinzani wa TANU.Yale maulidi yaliyosomwa Ilala yalihudhuriwa na viongozi wa EAMWS na yalipatawatu wengi na yakafana sana ukilinganisha na yale maulidi ya Mnazi Mmoja, yawafuasi wa TANU. Uongozi wa TANU ulitishika na hali hii iliyokuwa ikijitokezakwa maana ilikuwa inaonyesha kuwa chama kilikuwa kinapoteza wafuasi ambao walikuwa wakijiunga na kambi ya Tewa na Titi iliyokuwaikisemekana ipo dhidi ya Nyerere. [1]Tarehe 17 Oktoba, 1968, Adam Nasibu akatokeatena katika magazeti lakini sasa hakuwa tena mgeni machoni mwa watu, alikuwaanafahamika kama katibu mwenye hamasa za siasa wa EAMWS kutoka Bukoba ambaealiunga mkono Azimio la Arusha na kutoa maelekezo kwa viongozi wengine waKiislam akieleza vipengele vya azimio hilo. Adam Nasibu alitangaza kupitiaradio ya serikali na na magazeti ya TANU kuwa mkoa wake, Bukoba unajitoa kutokaEAMWS.[1]Ghafla Adam Nasibu akawa mtu mashuhuri wa kufahamika nchi nzima, magazeti yaTANU na radio ya serikali ikaanza kumjenga haiba yake pamoja na kuutangaza kilekilichokuja kujulikan kama ëmgogoroí wa Waislam. Magazeti ya TANU chini yaBenjamin Mkapa yakawa yamepata habari ya kushabikia: ëRadio ya serikali namagazeti ya TANU kwa pamoja yanatoa habari kwa uzito wa hali ya juu kuhusukuhusu kujitoa kwa Bukoba katika EAMWS. Magazeti ya TANU yakiwa yameshehezavichwa vya habari na maelezo ya mgogoro na picha za Adam Nasibu zikipambakurasa zake za mbeleí. [1]Ilikuwa baada ya magazeti na radio kutangaza nakuandika habari hizo ndipo Waislam kwa mara ya kwanza wakaja kutanabahi kuwawalikuwa wanakabiliwa na ëmgogoroí mkubwa wa nchi nzima. Lakini matatizoyalikuwa yameanza hasa toka siku ile watu wa Dar es Salaam waliposoma maulidimbili mwezi wa Juni, 1968. Siku tano baadae, yaani tarehe 22 Oktoba, SheikhJuma Jambia mwanakamati wa halmashauri kuu ya EAMWS kutoka Tanga na yeyeakatangaza kuwa Tanga inajitoa katika EAMWS. [1] Mwenyekiti wa EAMWS TewaSaid Tewa akamfahamisha Sheikh Jambia kuwa uamuzi wake ulikuwa ni uamuzi wa mtummoja. Jibu la Sheikh Jambia lilikuwa ni kutoa taarifa kwa vyombo vya habarikuvifahamisha uamuzi huo. Sheikh Jambia alitoa taarifa hiyo pamoja na mtu mmojaliyefahamika wa jina la Abdi Matunga. Haukupita muda mrefu, Iringa nayoikatangaza kuwa inajitoa kutoka EAMWS.Uongozi wa EAMWS kwa haraka ukaitisha mkutanokujadili hali ile mpya iliyojitokeza. Vyombo vile vya habari, Uhuru na TheNationalist ambavyo vilikuwa vikitumikia wale waliokuwa wanaodai kujitenga naEAMWS, sasa vikawa havitaki kutoa au kuandika habari za viongozi wa EAMWS ambaowalikuwa wanapigania umoja wa Waislam. Hapa ikawa ni wazi kuwa serikali ilikuwainatumia vyombo vya habari, yaani magazeti yaliyokuwa chini ya TANU na radio yaserikali kuwahujumu Waislam na EAMWS. Uongozi wa EAMWS ulipokuja kutanabahi ninani walikuwa nyuma ya hujuma ile wakawa wamebaini hatari iliyokuwaikiwakabili, kwa ajili hii basi waliwageukia Waislam kutaka msaada wao."

Mohamed

Ahsantu kwa darsa hii.

Hakika kila mtenda mabaya basi Mola atamlipa sawa na matendo yake na mtenda mema halikadhalika. Adam nasib na Alhaj Kundya watakumbukwa daima.

Lakin Pia nakuombea kwa mola Sheikh Mohamed Said akujaalie kila lenye kheir na kukukinga na shari za wenzetu wa upande wa kushoto
.
 
Nijue kitu gani tena wakati kwenye bandiko langu nimeandika kwamba Vatican ni nchi lakini inayotawaliwa kidini. Ni aina gani ya nchi au watu wanaoishi humo au idadi ya wanawake waliopo mabaozi wake ni wa nchi gani. Ninajua ni aina gani ya nchi ambayo Vatican inatambuliwa na ninajua ni kwanini Vatican ina sifa hizo ambazo ni za "kipekee" duniani. Wao ni kanisa lakini pia ni nchi.

Je unaweza kunitajia sifa za nchi na zile za taasisi kama ilivyo Aghakhan au Clinton foundation?
 
Lakin Pia nakuombea kwa mola Sheikh Mohamed Said akujaalie kila lenye kheir na kukukinga na shari za wenzetu wa upande wa kushoto
.

Kuna watu huwa wanafikiri kwamba wanammiliki Mungu. "wenzenu" wa upande wa kushoto ni kina nani tena hao, na nyie ni nani kawaambia kwamba mko mkono wa Kulia?
 
Back
Top Bottom