Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
Unajua kuna vitu vingine vinakuwa simple lakini kuna watu kama wewe mnavifanya kuwa complicated.
Kama ulivyosema haya ni MAJI MAZITO, na nakuona unaanza kuzama; lakini MS atakusaidia. By the way, naendelea kusoma hii historia ya Ukweli kutoka kwa MS.
Mr. Right,
Tuendelee na darsa:
"Kile kikundi kilichokuwa kikidai kujitengakilitoa sababu nyingi za uamuzi wao huo. Lakini katika sababu hizo zao zotekubwa zaidi ilikuwa katiba ya jumuiya ile ilikuwa haipo sawa na uongozi wanchi. Walidai kuwa katiba iwe ya Kitanzania na Aga Khan asiwe patroni. Vilevilewakadai kuwa Katibu Mkuu wa jumuiya awe Mwafrika Muislam. (Wakati ule katibualikuwa Abdul Aziz Khaki, Muismaili na Mtanzania wa asili ya Kihindi). Kikundikile halikadhalika kilitaka kujua vyanzo vya misaada kwa Waislam na misaadahiyo ilikuwa kitumikaje.[1]Dai lingine na hili likawa zito kwa uongozi wa EAMWS lilikuwa kuwa ëviongozi waEAMWS wawe wale wanaoamini malengo ya TANU, wale ambao wanapinga TANU hawafaikuwa viongozi wa Waislam wa Tanzania.[1] Madai haya yalifikishwa makao makuu ya EAMWSna Adam Nasibu, Muhammad Zoharia na Hamisi Kayamba. Tewa Said Tewa akiongozaKamati Kuu ya EAMWS alijaribu kuzungumza na viongozi wale lakini hawakutakamaelewano ya aina yoyote. Siku ya pili baada ya kutoa madai haya Adam Nasibualiitisha mkutano wa waandishi wa magazeti na ndipo akaeleza kuwa Bukoba imejitoa EAMWS.Uislam una kanuni na sheria zake za msingiambazo ndizo zinazowaongoza Waislam katika maisha yao ya kila siku. Madaiwaliyotoa kile kikundi hayakuwa madai yenye uzito mkubwa kiasi cha kusababishafarka kubwa kiasi kile kwa sababu madai yale yote yangeliweza kujibiwa kwaurahisi kabisa. Kulikuwa na baadhi ya madai ambayo yalikuwa hayajadiliki kwasababu ya mafunzo ya msingi ya Uislam. Tatizo la katiba lingeliweza kujadiliwana kumalizwa katika vikao vya kawaida. Lakini kuhoji rangi ya Muislam hilohalijadiliki kwa kuwa Uislam haubagui rangi ya mja kwa kuwa kufanya hivyokunapingana na ujumbe wa Uislam wa dini moja kwa watu wa ulimwengu mzima.Kufanya hivyo ni kwenda kinyume na mafunzo ya Qurían Tukufu.Ilikuwa wazi kuwa wale waliokuwa wanadaiutengano katika EAMWS hawakuwa watu wajinga kiasi cha kukosa kujua kuwa hayowaliyokuwa wakidai yalikuwa kinyume na Uislam. Kwa kuwa walikuwawanangíangíania kujitoa katika EAMWS, ilikuwa sasa kitu dhahiri kuwa hikikikundi cha Waislam waliojawa na ëhamasa za kizalendoí walikuwa na mpangomaalum uliokuwa ukisaidiwa na serikali wa kuvunja umoja wa umma wa Kiislam iliWaislam wadhoofike na wawe hawana nguvu tena katika siasa. Hata hivyo, tarehe14 Novemba, 1968, Baraza la EAMWS la Tanzania liliitisha mkutano wajumbe kutoamikoa yote ya Tanzania kujadili ëmgogoroí. Pamoja na waliohudhuria ni wajumbekutoka mikoa ambayo tayari ilikuwa imekwishajitenga na EAMWS. Mkutano huuulifanyika katika shule ya Kiislam ya Kinondoni.Hapajatokea katika historia ya Uislam Tanzaniamkutano kama ule. Uongozi ulikuwa unaingia katika chumba cha mkutano tayariumeshajeruhiwa vibaya sana na propaganda za magazeti ya TANU na radio yaserikali. Katika moja ya shutuma ambazo zilikuwa zikiandama uongozi wa EAMWSilikuwa ni matumizi mabaya ya fedha za jumuiya.Akifungua mkutano ule Tewa aliwatahadharishawajumbe kuwa makini katika lolote watakaloamua kwa kuwa endapo wajumbewatashindwa kuafikiana basi matokeo yake ni kuvunjika kwa EAMWS, umoja waWaislam na mwisho ya miradi yote ya elimu pamoja na ujenzi wa Chuo Kikuu.[1]Hisia kali zilitawala mkutano huu na baadhi ya wajumbe wanawake walikuwawakilia hasa pale baadhi ya wajumbe walipokuwa wakitoa michango yao katikamjadala walipokuwa wakisoma aya za Qurían Tukufu na kueleza fadhila za kupiganajihad dhidi ya madhalimu na wanafiki. Hisia hizi kali zilitokana na ukweli kuwawajumbe walikuwa wanafahamu kuwa wale wenzao waliokuwa wakidai kujitengawalikuwa wakitumikia Ibilis tu na wala msimamo waliokuwanao haukuwa wao walahawakuwa wanayafanya yale kwa mapenzi ya Allah na Mtume wake. Mwenyekiti wamkutano Tewa Said Tewa aliahirisha mkutano hadi siku ya pili ili wajumbe wapoena watoe mchango wakiwa katika hali ya utulivu. Katika wajumbe ambao walisimamakidete kutetea umoja wa Waislam walikuwa Sheikh Issa Mchowera kutoka Mtwara,Bilali Rehani Waikela, Hassan Johari na Sheikh Abdallah Said kutoka Kigoma.Mkutano uliamua kuunda Tume ya Uchunguzi ya watusaba [1]kuchunguza chanzo cha ëmgogoroí na kisha itoe taarifa. Mussa Kwikima kijanamwanasheria alichaguliwa kuwa katibu wa tume ile ya uchunguzi. Wakati huo mikoatisa ilikuwa tayari imeshajitenga na EAMWS na magazeti ya TANU yakawa tayariyamejenga ëmgogoroí ule kufikia hali ya kuonekana kuwa ni ëmgogoroí wa taifazima ambao kila mtu anaweza kuuingilia na kusema atakalo. Magazeti ya TANUyakawa yanaandika na kuchapisha mambo ya EAMWS kama wanavyotaka, wakizidi kutiachumvi katika ugomvi ambao tayari ulikuwa umeshaleta hofu na farka kubwa katikajamii. Inasemekana viongozi wengine wa EAMWS walikuwa wanaambiwa wajitoe hukuwameshikiwa bunduki." [1]
Mohamed