Barubaru
JF-Expert Member
- Apr 6, 2009
- 7,161
- 2,324
NARUDIA KUBANDIKA TENA HILI BANDIKO KWANI SIELEWI NI KWANINI FAIZAFOXY NA MOHAMED SAID HAWATAKI KUNIJIBU SWALI LANGU HILI.
Waislamu wana Nguzo zao tano wanazoziamini kama ndiyo msingi wa dini yao. Kama kweli waislamu wa Tanzania tangu Tanganyika walikuwa wanakandamizwa, ni nguzo ipi kati ya hizi tano ambayo waislam wa Tanzania wanakatazwa kuitimiza na Serikali kwa sababu serikali inadhibitiwa na MfumoKristu?
1. Kushahadia
2. Kuswali swala tano
3. Kufunga
4. Kutoa zaka
5. Kuhiji kwa mwenye uwezo
Kama waislamu wangekuwa wanakandamizwa katika hizo nguzo tano za uislamu ningeelewa hoja za MS. MS na wenzake watuambie ni wapi na ni lini waslamu walikatazwa kwenda kuhiji, kuswali. kufunga kwa Sunnah na Kufunga Ramadhani, kutoa zaka au kushahadia. Sijawahi kuona mfumo wa serikali ukikataza wakristo kusilimu au waislamu kujenga misikiti au kuadhini. Naijua misikiti ambayo iko katikati ya makazi ya watu kwenye mchanganyiko wa wakristo na waislamu na sijawahi kusikia serikali ikikataza waislamu kuadhini kwa sababu 'wanawasumbua" wasio waislamu kwa adhana zao.
Waislamu wanapotaka kwenda Mecca kuhiji hakuna siku walikatazwa kwenda badala yake serikali mara kadhaa imewahi kutoa fedha kusaidia waislamu kwenda kuhiji, sasa hapo waislamu wanakandamizwaje na huo mfumokristu na inakuwaje mfumokristu unashindwa kuzuia waislamu kuhiji, kusilimisha wakristo au kuadhini?
Hivi karibuni serikali si ilishawahi kutoa zaidi ya Shilingi Bilioni 2 kusafirisha mahujaji kwenda Mecca kuhiji? Kanisa lilikuwa wapi kuizuia serikali kutoa fedha hizo??
KUJIBU HOJA HAMTAKI BADALA YAKE MNALETA BLAH BLAH NA KUPIGIANA CHAPUO
Kigarama,
Ukiona watu wamekaa kimya ujue suala lako ni off point.
Unalizotaja ni nguzo za Uislam tu lakini kinachozungumziwa hapa ni masuala ya Elimu na maendeleo kijumla ya waislam. Suala la nguzo hii ni imani ambayo ukipingana nayo kwa aina yoyote basi lazima damu imwagike. Mfano ni huko Mwanza pale mtu alipochoma Qur,an. najua utakuwa unalijua hilo.Na mfano mwingine ni kule Znz zamaani tuliwahi kufanya maandamano makubwa sana kupinga kauli ya Sofia kawawa (mwenyekiti wakti huo wa UWT) pale alipowaomba masheikh kukaa kitako kubadilisha sheria ya ndoa ya kiislam na kufanya kila mwanaume aruhusiwe kuoa mke mmoja. kwani alidai sheria ya wake wanne inakandamiza wanawake. Hiyo ni imani na sote kwa ujumla wetu tuliingia mtaani kumlaani.
Dhulma imefanywa katika masuala ya kiuchumi na kielimu ili kudumaza maendeleo ya uislamu na waislamu na kufanya upendeleo kwa dini nyingine.
nakuomba umsome vizuri Sheikh Mohamed Said bila jazba na utaelewa nini kinaongelewa.
Tulia na soma kwa nia ya kuelewa.