Historia ya Uhuru isimuliwavyo na Mohammed Said yakosolewa

Historia ya Uhuru isimuliwavyo na Mohammed Said yakosolewa

NARUDIA KUBANDIKA TENA HILI BANDIKO KWANI SIELEWI NI KWANINI FAIZAFOXY NA MOHAMED SAID HAWATAKI KUNIJIBU SWALI LANGU HILI.

Waislamu wana Nguzo zao tano wanazoziamini kama ndiyo msingi wa dini yao. Kama kweli waislamu wa Tanzania tangu Tanganyika walikuwa wanakandamizwa, ni nguzo ipi kati ya hizi tano ambayo waislam wa Tanzania wanakatazwa kuitimiza na Serikali kwa sababu serikali inadhibitiwa na MfumoKristu?

1. Kushahadia

2. Kuswali swala tano

3. Kufunga

4. Kutoa zaka

5. Kuhiji kwa mwenye uwezo

Kama waislamu wangekuwa wanakandamizwa katika hizo nguzo tano za uislamu ningeelewa hoja za MS. MS na wenzake watuambie ni wapi na ni lini waslamu walikatazwa kwenda kuhiji, kuswali. kufunga kwa Sunnah na Kufunga Ramadhani, kutoa zaka au kushahadia. Sijawahi kuona mfumo wa serikali ukikataza wakristo kusilimu au waislamu kujenga misikiti au kuadhini. Naijua misikiti ambayo iko katikati ya makazi ya watu kwenye mchanganyiko wa wakristo na waislamu na sijawahi kusikia serikali ikikataza waislamu kuadhini kwa sababu 'wanawasumbua" wasio waislamu kwa adhana zao.

Waislamu wanapotaka kwenda Mecca kuhiji hakuna siku walikatazwa kwenda badala yake serikali mara kadhaa imewahi kutoa fedha kusaidia waislamu kwenda kuhiji, sasa hapo waislamu wanakandamizwaje na huo mfumokristu na inakuwaje mfumokristu unashindwa kuzuia waislamu kuhiji, kusilimisha wakristo au kuadhini?

Hivi karibuni serikali si ilishawahi kutoa zaidi ya Shilingi Bilioni 2 kusafirisha mahujaji kwenda Mecca kuhiji? Kanisa lilikuwa wapi kuizuia serikali kutoa fedha hizo??

KUJIBU HOJA HAMTAKI BADALA YAKE MNALETA BLAH BLAH NA KUPIGIANA CHAPUO

Kigarama,

Ukiona watu wamekaa kimya ujue suala lako ni off point.

Unalizotaja ni nguzo za Uislam tu lakini kinachozungumziwa hapa ni masuala ya Elimu na maendeleo kijumla ya waislam. Suala la nguzo hii ni imani ambayo ukipingana nayo kwa aina yoyote basi lazima damu imwagike. Mfano ni huko Mwanza pale mtu alipochoma Qur,an. najua utakuwa unalijua hilo.Na mfano mwingine ni kule Znz zamaani tuliwahi kufanya maandamano makubwa sana kupinga kauli ya Sofia kawawa (mwenyekiti wakti huo wa UWT) pale alipowaomba masheikh kukaa kitako kubadilisha sheria ya ndoa ya kiislam na kufanya kila mwanaume aruhusiwe kuoa mke mmoja. kwani alidai sheria ya wake wanne inakandamiza wanawake. Hiyo ni imani na sote kwa ujumla wetu tuliingia mtaani kumlaani.

Dhulma imefanywa katika masuala ya kiuchumi na kielimu ili kudumaza maendeleo ya uislamu na waislamu na kufanya upendeleo kwa dini nyingine.

nakuomba umsome vizuri Sheikh Mohamed Said bila jazba na utaelewa nini kinaongelewa.

Tulia na soma kwa nia ya kuelewa.

NARUDIA KUBANDIKA TENA HILI BANDIKO KWANI SIELEWI NI KWANINI FAIZAFOXY NA MOHAMED SAID HAWATAKI KUNIJIBU SWALI LANGU HILI.

Hivi karibuni serikali si ilishawahi kutoa zaidi ya Shilingi Bilioni 2 kusafirisha mahujaji kwenda Mecca kuhiji? Kanisa lilikuwa wapi kuizuia serikali kutoa fedha hizo??

KUJIBU HOJA HAMTAKI BADALA YAKE MNALETA BLAH BLAH NA KUPIGIANA CHAPUO

Kigarama.

Kuna masuala mengi hapo ya kujiuliza.

Je hao waliopelekwa Macca walikosa nauli?
Kwanini Serikali iliwapeleka yaani walikuwa na speciallity gani kwa Serikali?
Je fungu hilo walitoa kutoka wizara gani?

Lakini kwa kukukumbusha ni kuwa Je unajuwa Serikali ya JMTz ilisaini MoU na kanisa? Na unajua kila mwaka Kanisa linachota billioni 91 kutokana na MoU hiyo? Na unajuwa waislam hawapati kitu hapo?

Je hiyo sio dhulma?

Tafakur.

Tungejua kama hoja zetu zingekuwa zimejibiwa...lakini kwa sababu hutaki kuzijibu hoja zetu hii inabaki kuwa masimulizi tu ya gerezani!
Mwalimu gani anayetoa 'Darsa' lakini akiulizwa maswali na wanafunzi anashindwa kujibu? Cha kushangaza unajivunia kwamba wamejua ilihali wana maswali mengi ambayo hayajajibiwa!

Sweke34,

Kunyamaza pia ni jibu.
Kuna wakati mtu unasema na kuna wakati bora kuwa kimya.

Hivi ndivyo masheikh wetu walivyotufunza.
Ila kusomesha mtu haachi kwa kuwa ni amana.

Mohamed
 
Kigarama.

Kuna masuala mengi hapo ya kujiuliza.

Je hao waliopelekwa Macca walikosa nauli?
Kwanini Serikali iliwapeleka yaani walikuwa na speciallity gani kwa Serikali?
Je fungu hilo walitoa kutoka wizara gani?

Lakini kwa kukukumbusha ni kuwa Je unajuwa Serikali ya JMTz ilisaini MoU na kanisa? Na unajua kila mwaka Kanisa linachota billioni 91 kutokana na MoU hiyo? Na unajuwa waislam hawapati kitu hapo?

Je hiyo sio dhulma?

Tafakur.

Nipe darsa ndugu yangu Barubaru, bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania lenye wabunge waislamu machachari kama Hamad Rashid wa CUF lilipitisha bajeti ya dhulma namna hii bila hata aibu? Pesa hiyo inachotwa kupitia wizara gani ili tuanze kupaza sauti za kupinga kwa nguvu zetu zote bila kujali imani zetu.
 
Shadhuly,

Amin Amin Amin.

Sheikh Nurdin Hussein huyu hapa hii ni 1954/55:

"Kipindi chama badiliko kutoka TAA kuwa TANU kilikwenda vizuri pale makao makuu.Hakukuwa na ya migongano kati ya viongozi wa makao makuu, ukitoa kikundi kidogo cha Waislamu wenye msimamo mkali waliokuwa wakipanga kumg'oa Nyerere kwa kuwa alikuwa Mkristo. Hii ilikuwa ni mara ya pili kwa suala la dini kuzuka tanguNyerere achukue uongozi wa chama kwa mara ya kwanza mwaka 1953.

Mzee Said ulijuaje kuwa kulikuwa na majaribio mawili ya kutaka kumng'oa Nyerere kwa sababu ya Ukristo wake? Kikundi hiki kidogo cha "Waislamu wenye msimamo mkali" kiliongozwa na nani?
 
Hukuna njia ya mkato katika kujenga hoja ili kupinga maandiko ya Mohamed Said..

Ni kujitaidi tu kuandika papers za kutosha na vitabu vingi ili kupambana na Mohamed Said..

Haiwezekani kuzuia mvua Mohamed Said kaishaandika kitabu cha historia ya uhuru wa Tanganyika..

Ni changamoto kubwa kwa watanzania wa Mbeya, Mwanza, Bukoba, Kilimanjaro, Arusha, Shinyanga, na mikoa mingine..

Kama mnaona Mohamed Said anapotosha watu na historia yake ya uhuru wa Tanganyika..

Njooni na nyie na historia za kupigania uhuru wa Tanganyika kutoka baadhi ya mikoa nilioitaja inaweza kuwa kweli kuna wapigania uhuru hawakutajwa na Mohamed Said kutokana na chuki zake..

Zaidi ya yote kama mtashindwa kuja na historia mbadala basi Mohamed Said hatabaki kuwa shujaa wa kwanza Tanzania kuandika historia ya uhuru wa Tanganyika
 
Sweke.
Nazidi kukushauri Sweke, Huwezi hata siku moja kujibu hoja za Mohamed kwa kusoma tu humu jamvini bali kwa kufanya utafiti na kuuliza masuala yaliokuwa constructive na sio ya kejeli na mas'khara.
Hivi haya maswala mengi aliyoulizwa humu Mohamed Saidi hayakuwa constructive?
Hebu nisaidie katika hili ingawaje linaonekana ni swali dogo.......hivi kwenye 83% christians na 17% muslims unapata % ngapi ya wasiokuwa na dini?
Hicho kitu kinahitaji utafiti kweli? Si mtu anatakiwa akubali tu kuwa amekosea?

Sasa unaniambia mimi nifanye utafiti wa historia wakati mimi mtu wa ICT na nimekuja baadaye kabisa baada ya uhuru. Hivi ni usomi gani wa kuandika paper halafu ukikosolewa unawaambia watu waandike nao paper. Kwa hiyo nao wakisolewa waseme hivyo hivyo andika na wewe paper...kweli huo ndiyo usomi? Mkuu wewe si una Ph.D? Umepita njia gani mpaka umeipata hiyo Ph.D...? kwa kusema andika na wewe Thesis?
Mohamed Said habebeki, amefulia...na 'Darsa' lake limeshalala 'doro'...!
 
Hukuna njia ya mkato katika kujenga hoja ili kupinga maandiko ya Mohamed Said..

Nikujitaidi tu kuandika papers za kutosha na vitabu vingi ili kupambana na Mohamed Said..

Haiwezekani kuzuia mvua Mohamed Said kaishaandika kitabu cha historia ya uhuru wa Tanganyika..

Ni changamoto kubwa kwa watanzania wa Mbeya, Mwanza, Bukoba, Kilimanjaro, Arusha, Shinyanga, na mikoa mingine..

Kama mnaona Mohamed Said anapotosha watu na historia yake ya uhuru wa Tanganyika..

Njooni na historia za kupigania uhuru wa Tanganyika kutoka baadhi ya mikoa nilioitaja inaweza kuwa kweli kuna wapigania uhuru hawakutajwa na Mohamed Said kutokana na chuki zake..

Zaidi ya yote kama mtashindwa kuja historia mbadala basi Mohamed Said hatabaki kuwa shujaa wa kwanza Tanzania kuandika historia ya uhuru wa Tanganyika
Ritz,

Sadly to say wote hapa hawana intellectual authority to write a book or academic paper to challenge what Mohamed said has presented in front of them. Labda namsubiria Professa Saida wa UDSM (Mke wa Professa Haroub Othman) ambaye nilisikia watatoa kitabu cha maisha ya mwalimu na nina hamu nikisome nijue kuna nini.

Wengineo humu jamvini wanachokijua ni kutafuta mahali pa kukosoa wakikosa wanabadilisha maneno ili mjadala uonekane hauna maana. Nimewaambia andike an academic paper tutaisoma tu wala huna haja kuja JF kuileta tutaipata huko huko zinakohifadhiwa na kuisoma.

Mohamed Said watu wengine tumemsoma kabla hata Jambo Forums haijaanzisha wala kufikiriwa kuanzishwa. Tunajua wapi tuliona utafiti wake. Na nyie andikeni tuwasome.

Kigarama nakuja na nondo za kujibu hoja zako kuhusu Mkwawa just be ready.
 
Hivi haya maswala mengi aliyoulizwa humu Mohamed Saidi hayakuwa constructive?
Hebu nisaidie katika hili ingawaje linaonekana ni swali dogo.......hivi kwenye 83% christians na 17% muslims unapata % ngapi ya wasiokuwa na dini?
Hicho kitu kinahitaji utafiti kweli? Si mtu anatakiwa akubali tu kuwa amekosea?

Sasa unaniambia mimi nifanye utafiti wa historia wakati mimi mtu wa ICT na nimekuja baadaye kabisa baada ya uhuru. Hivi ni usomi gani wa kuandika paper halafu ukikosolewa unawaambia watu waandike nao paper. Kwa hiyo nao wakisolewa waseme hivyo hivyo andika na wewe paper...kweli huo ndiyo usomi? Mkuu wewe si una Ph.D? Umepita njia gani mpaka umeipata hiyo Ph.D...? kwa kusema andika na wewe Thesis?
Mohamed Said habebeki, amefulia...na 'Darsa' lake limeshalala 'doro'...!

I smell a sense of denial hahaha nimekuambia ratio ya 83% Christians and 17% Muslims depends upon the data Mohamed Said has. Inawezekana kweli iko hivyo hivyo au pengine sample yake ina mapungufu ya taarifa but haimaanishi alichokisema ni uongo. Are you familiar with sample biaseness. Fanyeni utafiti mtakutana na hayo otherwise mko kwenye denial tu.

Usilazimishe mjadala kulala doro pole sana.
 
Usilete mipasho na mambo ya kichen party kwenye mambo ya msingi...

Mohamed Said, endelea na Darsa lako tunakusoma kwa umakini mkubwa!

Wewe kitu kikubwa unachofanya humu JF ambacho nakipenda ni kuendelea kupigia mistari maandiko!
 
Mdondoaji,

Tatizo liliopo mwenzao Mohamed Said, mkononi ana kitu na wengine mkononi wana mzigo wa porojo..

Huwezi kuzuia mvua
 
I smell a sense of denial hahaha nimekuambia ratio ya 83% Christians and 17% Muslims depends upon the data Mohamed Said has. Inawezekana kweli iko hivyo hivyo au pengine sample yake ina mapungufu ya taarifa but haimaanishi alichokisema ni uongo. Are you familiar with sample biaseness. Fanyeni utafiti mtakutana na hayo otherwise mko kwenye denial tu.

Usilazimishe mjadala kulala doro pole sana.
Wacha ushabiki na majungu yako, huyo mzee Mohamed wako amekuwa analiona hili swali yeye mwenyewe na ameshindwa kulijibu, sasa kwa nini wewe umjibie? kwanini upotoshe wakati authority(Mohamed) ipo?
 
Usilete mipasho na mambo ya kichen party kwenye mambo ya msingi...

Mohamed Said, endelea na Darsa lako tunakusoma kwa umakini mkubwa!

Wewe kitu kikubwa unachofanya humu JF ambacho nakipenda ni kuendelea kupigia mistari maandiko!
Hakuna cha darsa wala nini, zaidi ni uhujumu na uchochezi wenye nia mbaya, nambaya zaidi sumu ya uchochezi ya mzee wenu huyu imeshawatafuna hamuoni wala hamsikii! Hamna majibu ya kisomi zaidi ya kulialia hapa".....mara oh na nyie fanyeni utafiti......oh andikeni historia yenu........."Jibuni hoja acheni kulazimisha mambo.
 
Sweke.

Kitendo cha kuuliza suala maana yake umesoma na kuelewa na pale ulipoona mush'kira ndio ukauliza suala na hii inadhihirisha wazi kuna athari katika akili yako kuhusu masuala yaliyoelezwa japo unajifanya sintofahamu. Lakini pia kuna vitabu maalum vinauzwa na paper mbalimbali zinakuwa presented kwenye universities mbalimbali kwa wana taaluma na hivyo watu kuelewa na kujadili.

Nazidi kukushauri Sweke, Huwezi hata siku moja kujibu hoja za Mohamed kwa kusoma tu humu jamvini bali kwa kufanya utafiti na kuuliza masuala yaliokuwa constructive na sio ya kejeli na mas'khara.

Kumbuka nia kuu yya Mohamed Said ni kutupa upande wa pili wa Historia ya Tanganyika ambayo ilisahaulika. Na yeye hakufanya ajizi amefanya utafiti na ametunga kitabu na papers kibao.

Ni jukumu lako na wewe kuweka mambo hadharani kwa kutoa makala maalum kuonyesha wapi Mohamed said amepotoka na wewe kusasahihisha. Kwa kutumia Jf huwezi Abadan.
Sasa, kama Mohamed hawezi kujibu maswali yetu basic, mnakimbilia eti tusome vitabu au tufanye utafiti, what the hell are we doing here?
Mohamed, as a scholar and a researcher, should be able to answer all questions thrown at him without just saying "nimekusikia" au soma bandiko langu. He should be able to enhance the digestion and questions that emanate from his own writings. Baadhi yetu tumesoma vitabu vyake lakini bado tuna maswali. Tukiyauliza mnatuambia tufanye tafiti zetu wenyewe. What is this?
 
Maswali yenu nafikiri ni kizushi si kitaalam..jaribuni kuuliza maswali ya maana..
 
Hakuna cha darsa wala nini, zaidi ni uhujumu na uchochezi wenye nia mbaya, nambaya zaidi sumu ya uchochezi ya mzee wenu huyu imeshawatafuna hamuoni wala hamsikii! Hamna majibu ya kisomi zaidi ya kulialia hapa".....mara oh na nyie fanyeni utafiti......oh andikeni historia yenu........."Jibuni hoja acheni kulazimisha mambo.

Mchomchezi labda wewe sisi tuko kwenye fact findings..

Sumu ya uchochezi what?? of course bila haki lazima kutakuwa na sumu..
 
Ritz, Labda namsubiria Professa Saida wa UDSM (Mke wa Professa Haroub Othman) ambaye nilisikia watatoa kitabu cha maisha ya mwalimu na nina hamu nikisome nijue kuna nini.
Mndondoaji naomba unieleweshe kidogo, una maana kuwa pamoja na vitabu vyote ambavyo vimewahi kuandikwa kuhusu maisha ya Mwalimu, unasubiri cha Prof. Saida wa UDSM (mke wa Prof. Haroub Othman), ili iweje. Je baada ya hicho kitabu kutoka, kama atatokea mtu asiyekubaliana na kilichoandikwa na yeye atatakiwa kwanza aandike cha kwake ndio apate haki ya kukikosoa ? Je kama ndani ya hicho kitabu kutakuwapo na hoja zinazopingana na hizi simulizi za Gerezani, utakuwa tayari kuungana na sisi wengine kumnyooshea kidole huyo Mohamed Said kwa upotoshaji wake uliojikita zaidi katika kuchochea mfarakano ndani ya jamii kwa msingi wa dini ?
Nimewaambia andikeni an academic paper tutaisoma tu wala huna haja kuja JF kuileta tutaipata huko huko zinakohifadhiwa na kuisoma.
Je kwa hapa unatutaka tusihoji chochote alichoandika Mohamed Said kutokana na simulizi za utotoni kwa msingi kuwa bila kuandika academic paper hatuna hiyo haki ya kuhoji ? Mimi kwa mfano kuna mengi ninayoyajua na nimejaribu kuyasema humu kwenye mnakasha na kumhoji Mohamed Said kwa nini historia ya wazee wake wa Gerezani anataka kutusukumizia kooni kwamba ndiyo ya Tanganyika na hata data tumempa. Mathalani jimbo lililokuwa likitoa pesa nyingi kuiendesha TANU lilikuwa jimbo la ziwa, lakini yeye kakazania kuelezea soksi alizovaa Mwalimu au mchuuzi moja wa samaki wa Kariakoo kumpelekea Mwalimu kitoweo nyumbani kwake ! Hapo ndio tunatofautiana !
Mohamed Said watu wengine tumemsoma kabla hata Jambo Forums haijaanzisha wala kufikiriwa kuanzishwa. Tunajua wapi tuliona utafiti wake. Na nyie andikeni tuwasome.
Na hapa kosa analolijutia Mohamed Said ni huu mnakasha kutinga JF kwani amekuta siyo tu pumba zikichambuliwa lakini anapatiwa somo kuhusu umbo zima la mnyama tembo. Angeuacha huko kwingine anakopigiwa makofi hata akiongea utumbo na wala hangetusikia wengine lakini hili la kufikiri JF hadithi zake zitamezwa tu bila maswali, kafeli kwa asilimia kubwa tu. Of course, wako akina Topical na Barubaru, always handy and faithful hata wakilishwa sumu wataitikia hewala bwana, watu wa aina hiyo hawakosekani na ndiyo hutumiwa na Mohamed Said kurutubisha mbegu zake za chuki.
 
I smell a sense of denial hahaha nimekuambia ratio ya 83% Christians and 17% Muslims depends upon the data Mohamed Said has. Inawezekana kweli iko hivyo hivyo au pengine sample yake ina mapungufu ya taarifa but haimaanishi alichokisema ni uongo. Are you familiar with sample biaseness. Fanyeni utafiti mtakutana na hayo otherwise mko kwenye denial tu.

Usilazimishe mjadala kulala doro pole sana.
Mlifanya wote utafiti? Sisi tunataka atuambie yeye mwenyewe hayo maneno yako!
 
Nguruvi3: Msomi kama marhum Othman utakutana naye viwanja tu, na wala hujui anafanya nini. Utasikia BBC kateuliwa kusuluhisha nini n.k. Shivji hapigi kifua ila mambo zake zinampigia kifua. Wewe hujibu maswali unakazania nimekwenda Ibadan, Tonga,comoro, fiji na Vanuata, who cares hayo ni masimulizi ya chumbani kwako au gerezani na kipata barazni, usipotezee watu muda toa hoja jibu hoja.Kujigamba ni dalili ya inferiority complex.

Kikwebo;2838803]Sheikh Mohammed..pole kwa kejeli hizi toka kwa Nguruvi3. Imma kejeli kuwa habari hizi ulizozitafiti na kuziandika kuwa ni masimulizi ya chumbani..au porojo kama alivyogusia mtu mmoja wa pote lake ni dhihaka kubwa. Siamini maandishi ya siyo na quality na yenye quantity tu kama Nguruvi3 anavyozidi kukariri yangethubutu kufanyiwa reviews na kuwa references kwenye vyuo kadhaa
Sikuzungumzia tafiti kama masimulizi ya chumbani. Nilichosema ni kuwa habari za yeye kwenda Ulaya, Marekani, Vanuata n.k zinafaa azionglee chumbani kwasababu hazitusaidii. Nabaki na kauli hiyo kama tofauti yangu na wewe inavyojidhiri hapo juu bila kupinda ukweli.
Mfano, Nimemuuliza swali, kuna uhusiano gani kati ya vurugu za mabucha ya nguruwe na umasikini wa Kigoma, Tabora, Kilwa na Mtwara? Jibu la Mohamed: Mimi ninaalikwa sehemu nyingi sana nimekwenda Ibadan, Marekani na ulaya.

Swali: Kama Diamond jubilee hawakuwepo waislam isipokuwa BAKWATA, ilikuwaje waislam wasiokuwepo ukumbini wakakataa kushikana mikono na viongozi wa kikristo?
Jibu la Mohamed: Mimi nimeandika paper nyingi sana, kama mnataka kaandikeni paper kwasababu vitabu hamviwezi.

Swali: Nini ushiriki wa Kawawa kama 'right hand man wa Nyerere'.
Jibu la Mohamed: Nimeandika paper nyingi sana hata idadi yake siikumbuki hadi mtu aseme ndipo nakumbuka.

Na mwisho, watu wanasoma vitabu ili kuongeza uelewa katika hivyo vyuo vikuu, haina maana wana endorse kitabu chake. Je, wale wanaosoma kitabu cha Suleiman Rushdie nao wame endorse au wanafanyia reference kwa maana halisi zaidi ya kutafuta maarifa.
Barubaru;2838814]Nguruvi3, Sioni kama ni jambo la busara kuandika mistari 10 au 20 katika JF kutaweza kukidhi mahitaji au hamu ya waTz kujua historia hiyo kama ilivyobainishwa na kutungiwa kitabu na paper nyingi na Mohamed Said.
Huo ni ushauri wangu
Kwani Mohamed alipoleta mada hapa alitegemea watu wafanyaje, si angeiacha huko magazetini. Kinachofanyika hapa ni uchambuzi ambao Mohamed anakiri kuwa unamsaidia. Hivi mtu akiuliza Abdulwahid na Nyerere walikuwa ni wazanaki wote? Hivi kuna haja ya kufanya utafiti ili kubaini ukweli. Kama Mohamed atasema, hapana hawana uhusiano kuna shida gani hapo.
Tatizo msiloliona wengi ni kuwa Mohamed ameandika mambo asiyoweza kuyatetea kwa maneno yake, njia bora ni kuweka vipande vya kitabu chake kwa lengo la propaganda na kukwepa kujibu. Mapungufu haya utayaona ukisoma between the lines, lakini katika hali ya ushabiki 'ukipenda chongo utaita kengeza' Ima huo ushauri wa kuandika magazetini ninauzingatia kwasababu miaka michache iliyopita nilikuwa natoa makala Raia mwema.
Barubaru;2840095]Sweke.Kitendo cha kuuliza suala maana yake umesoma na kuelewa na pale ulipoona mush'kira ndio ukauliza suala
Aha! kuumbe, hebu tuangalie mfano mzuri
Mohamed Said: Kipindi chama badiliko kutoka TAA kuwa TANU kilikwenda vizuri pale makao makuu.Hakukuwa na ya migongano kati ya viongozi wa makao makuu, ukitoa kikundi kidogo cha Waislamu wenye msimamo mkali waliokuwa wakipanga kumg'oa Nyerere kwa kuwa alikuwa Mkristo. Hii ilikuwa ni mara ya pili kwa suala la dini kuzuka tanguNyerere achukue uongozi wa chama kwa mara ya kwanza mwaka 1953
Kuna huyu msomaji hakuelewa sehemu fulani na anauliza
Mwanakijiji:Mzee Said ulijuaje kuwa kulikuwa na majaribio mawili ya kutaka kumng'oa Nyerere kwa sababu ya Ukristo wake? Kikundi hiki kidogo cha "Waislamu wenye msimamo mkali" kiliongozwa na nani
Mohamed hajajibu na hatajibu, unaona jinsi unavyotusaidia kuuona ubabaishaji wa mzee. Sasa hapa huyu msomaji anatakiwa akaandike paper ili aelewe kitu asichokielewa kutoka katika maandishi ya simulizi za Mohamed kweli!!!!! Hivi jibu halisi linaweza kuzidi mistari 2.
 
Kwa sababu moja au nyingine, Mohamed Said jana aliweka wazi kisingizio cha "usahaulifu" kuelezea sababu zake za kukosa majibu ya kutetea hoja na maandishi yake mwenyewe. Kwa hiyo usishangae kwamba "hajajibu na hatajibu" hoja na maswali yote lukuki aliyoulizwa tokea awali ya mjadala huu.
 
Back
Top Bottom