Syll...
Mimi nakuhadithieni historia ya nyumbani kwetu nimeandika kitabu cha historia ya jamii yangu ambayo kabla haikuwapo.
Vipi mtu ataniambia kuwa hiyo siyo historia yetu?
Bahati mbaya au nzuri Nyerere ni sehemu ya historia hii.
Ingewezekana mimi ningemtoa katika historia hii nisingemtaja lakini historia hii itakuwa na upungufu mkubwa.
Angalia picha hiyo hapo chini.
Huyo kulia ni Mama Sakina mimi namwita bibi mwanae mmoja Mustafa alikuwa rafiki ya baba yangu.
Huyo kushoto ni Bi. Tatu bint Mzee akiishi Kirk Street (Mtaa wa Lindi) mbele ya mtaa huu ni Mtaa wa Kipata niliozaliwa mimi.
Bi. Tatu bint Mzee ni rika moja na mama yangu kwa hiyo Bi. Tatu mimi ni mama yangu.
Nimezaliwa na watu hawa na nimeishinao.
Sasa uongo uko wapi hapo?
Kuwa hawakuijenga TANU wala kupigania uhuru?
Jiulize wamefika vipi kuwa na Nyerere wanamsindikiza safari ya kwanza UNO 1955 na kumfanyia dua ya kumuaga katika jengo la Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika?
View attachment 2168905