Historia ya Uhuru isimuliwavyo na Mohammed Said yakosolewa

Wewe si ndiyo ulie anza kulia lia kwamba kuna watu unawajua wengi mno wamepigani uhuru, sasa kama unashindwa kuwataja, uliandika ili ufurahishe nafsi yako ?

Anae dai ujue ana ushahidi wa hilo, unapo amua kumpinga umpinge kwa hoja.

Dogo, matusi hayana uwezo hata wa kubadili herufi moja,sasa naona unapoteza muda kutukana.

Sasa kama ni hoja ya kitoto, inakuwaje unashindwa kuikosoa na kuiweka sawa, bali hata swali dogo la kuwataja kumi tu unao wajua unashindwa. Siyo kila mjadala uchangie, mingine ni bora kuwa msomaji na kupata faida.

Huwa siitiki mpaka niitike au unakuwa kama mwanamke mjamzito, visirani mia.

Shukrani.
Wewe jamaa, acha kiherehere. Tokea mwanzoni nakuona unajiingiza katika malumbano ambayo wewe huhusiki, labda sababu umezoea ubishi wa kijinga wa kwenu uswazi. MS anaweza kujibu kila hoja na swali bila ya wewe kujichomeka utadhani ni chawa wake.
 
Ni msemo ukimaanisha kuwa uongo ukirudiwa rudiwa mara nyingi hugeuka kuwa 'ukweli''
Haina maana uongo huo ni ukweli bali watu watauamini uongo huo na kuamini uongo kuna upa uhalali wa ukweli.

Mathalan, uongo wa kwamba Abdul Sykes alimpokea Mwalimu Dar es Salaam umerudiwa rudiwa sana kiasi kwamba watu wanaamini kuwa Abdul alimpokea Mwalimu. Kule kuamini ndio kunafanya uongo huo uonekane ukweli lakini haina maana ni ukweli, ni uongo uliorudiwa sana ukaonekana ukweli.
Ndugu yangu Nguruvi3, juhudi za Mohamed Said, kumpamba mjomba wake, mlowezi Abdul Sykes, kama mkombozi wa Watanganyika naona bado zinaendelea kwa nguvu zile zile.

Masikini Mohamed Said, amepambana kweli kweli kwa zaidi ya nusu karne akizipaka rangi ngano zilizopandwa kichwani mwake barazani na wazee wake mtaa wa Gerezani toka utotoni.

Ngano zikakua, zikamea na kukomaa na kazi iliyobaki sasa ikawa ni ya kuwatafuta walaji...walaji watakaoshawishika kuzimeza mazima mazima bila kuzitafuna ilhali zimewekwa mezani.

Na hapo ndipo Mohamed Said alipotumia ile falsafa ya uongo kutetewa na uongo na hali hii kurudiwarudiwa hadi ikaanza kufananafanana na ukweli na huyo Kisai ni zao la mafanikio hayo.

Nawatakia mjadala mwema...
 
Ni msemo ukimaanisha kuwa uongo ukirudiwa rudiwa mara nyingi hugeuka kuwa 'ukweli''
Haina maana uongo huo ni ukweli bali watu watauamini uongo huo na kuamini uongo kuna upa uhalali wa ukweli
Uongo ni uongo tu hata uweje, hata kama ikatokea wakaamini hauwezi kupata uhalali wa ukweli, bali kitakacho bakia hapo ni kuwa watu hawajui kama ni uongo.
 
Wewe jamaa, acha kiherehere. Tokea mwanzoni nakuona unajiingiza katika malumbano ambayo wewe huhusiki, labda sababu umezoea ubishi wa kijinga wa kwenu uswazi. MS anaweza kujibu kila hoja na swali bila ya wewe kujichomeka utadhani ni chawa wake.
Sihusiki kivipi kwani anaongelea nini ? Basi Historia iliyoandikwa nayo haituhusu. Maana yake hatutakiwi kujadili hii mada kwa ujumla wake.

Ukiwa unajadili haya mambo unatakiwa uwe mjuzi wa jambo husika au ukae kimya na uulize. Sasa hapa nimekuuliza swali dogo sana tena limetokana na kile ulichokiandika wewe mwenyewe, ajabu unashindwa kujibu.
 
Na hapo ndipo @Mohamed Said alipotumia ile falsafa ya uongo kutetewa na uongo na hali hii kurudiwarudiwa hadi ikaanza kufananafanana na ukweli
Nimecheka sana, ukweli ni kwamba hata kitabu kimoja cha mzee wetu sijawahi kukisoma, sababu mimi sipendi kona kona nimeona mna udhaifu mkubwa sana katika kuhoji mambo na kujenga hoja.

Sasa mfano wa udhaifu huo unao wewe, ambao hujaona shida kwa unaye mkingia kifua na kudai mimi ni zao la huyu mzee. Wewe unapo sema ya kuwa wao watu wengi wamefanya jambo fulani, maana yake unawajua. Sasa mtu akikuuliza basi katika hao wengi, tutajie walau watano. Unaposhindwa kutaja unamaanisha nini ? Sasa mkumbushe mwenzako akiandika jambo awe na ujuzi nalo.
 
Syll...
Mimi nakuhadithieni historia ya nyumbani kwetu nimeandika kitabu cha historia ya jamii yangu ambayo kabla haikuwapo.

Vipi mtu ataniambia kuwa hiyo siyo historia yetu?

Bahati mbaya au nzuri Nyerere ni sehemu ya historia hii.

Ingewezekana mimi ningemtoa katika historia hii nisingemtaja lakini historia hii itakuwa na upungufu mkubwa.

Angalia picha hiyo hapo chini.

Huyo kulia ni Mama Sakina mimi namwita bibi mwanae mmoja Mustafa alikuwa rafiki ya baba yangu.

Huyo kushoto ni Bi. Tatu bint Mzee akiishi Kirk Street (Mtaa wa Lindi) mbele ya mtaa huu ni Mtaa wa Kipata niliozaliwa mimi.

Bi. Tatu bint Mzee ni rika moja na mama yangu kwa hiyo Bi. Tatu mimi ni mama yangu.
Nimezaliwa na watu hawa na nimeishinao.

Sasa uongo uko wapi hapo?
Kuwa hawakuijenga TANU wala kupigania uhuru?

Jiulize wamefika vipi kuwa na Nyerere wanamsindikiza safari ya kwanza UNO 1955 na kumfanyia dua ya kumuaga katika jengo la Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika?

View attachment 2168905
Picha safi kabisa na nina uhakika dua ilimfikia, kwani alisafiri salama na kurudi salama, si unajua tena mambo ya Dua.

Mzee hakuna Uwongo kwani dhana haina uwongo mzee au?

Huo mtaa wa Lindi kumbe ulikuwa unaitwa Kirk st? Daktari Kirk? au

Mzee wangu wala usikwazike, kila mwanadamu ana historia yake na jamii yake. Tutakubaliana hapo. Nashukuru kwa hadithi. Walakin hadithi nilizofundishwa ni kuwa Waarabu kama vile Watu wa ulaya 'wazungu' walitufarakanya kwa Biblia upande mmoja na fimbo upande mwingine, Quaran upande mmoja na upanga upande mwingine, sasa leo hii ndio unaona hapa tunayo misuguano ya "Ustaarabu" na Uungwana au nimekosea? Au Historia haitufanyi hivyo?

Asante lakini kwa 'Hadithi' lakini tukubaliane kuwe dhana ya Historia au Hadithi unazotuhabarisha zina mtazamo wa kendeleza mfrakano wa Kale kati ya 'Waislamu' na 'Wakristo' sasa sie Waungwana tunaropoka ropoka tu bila kujua tunapigana Vita siyo yetu au ni seme sio vita yangu 'Mwafrika'.

Alamsiki Mkuu
 
Syll...
Mimi nakuhadithieni historia ya nyumbani kwetu nimeandika kitabu cha historia ya jamii yangu ambayo kabla haikuwapo.
Sawa sawa halafu unaaminisha watu ni Historia ya Tanganyika! kuna tofauti ya jamii na Jamii kama Tanganyika
Vipi mtu ataniambia kuwa hiyo siyo historia yetu?

Bahati mbaya au nzuri Nyerere ni sehemu ya historia hii.

Ingewezekana mimi ningemtoa katika historia hii nisingemtaja lakini historia hii itakuwa na upungufu mkubwa.
Nyerere anakukera sana ndiyo maana kwa 'fasihi' huachi kumdogosha kama si kumzodoa
Kwamba Nyerere kapata tu mwenyewe ni Abdul Sykes! Hapana kila mmoja na historia yake
Angalia picha hiyo hapo chini.

Huyo kulia ni Mama Sakina mimi namwita bibi mwanae mmoja Mustafa alikuwa rafiki ya baba yangu.

Huyo kushoto ni Bi. Tatu bint Mzee akiishi Kirk Street (Mtaa wa Lindi) mbele ya mtaa huu ni Mtaa wa Kipata niliozaliwa mimi.

Bi. Tatu bint Mzee ni rika moja na mama yangu kwa hiyo Bi. Tatu mimi ni mama yangu.
Nimezaliwa na watu hawa na nimeishinao.

Sasa uongo uko wapi hapo?
Kuwa hawakuijenga TANU wala kupigania uhuru?

Jiulize wamefika vipi kuwa na Nyerere wanamsindikiza safari ya kwanza UNO 1955 na kumfanyia dua ya kumuaga katika jengo la Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika?
Nani kasema hao akina mama unaoeleza ni 'Uongo'

Usitafute kitu cha kutumbukiza kutuondoa kwenye hoja.

Hoja ni kuwa Abdul Sykes hakumpokea Nyerere !
Kwamba Abdul hakumuona Dar kwa mara ya kwanza , alikutane naye kabla
Kwamba Nyerere aliakwa mkutano Mkuu, hakuzamia tu kutoka Tabora

Kwamba Nyerere alikula mayai kwa Abdul Sykes hilo tutabisha vipi ? Alikula !
Sijui kama aliweza kukunja chapati! Sijui kama aliweza kufinyanga Biriani! tena akiwa na Kaptula.
 
Sawa sawa halafu unaaminisha watu ni Historia ya Tanganyika! kuna tofauti ya jamii na Jamii kama Tanganyika

Nyerere anakukera sana ndiyo maana kwa 'fasihi' huachi kumdogosha kama si kumzodoa
Kwamba Nyerere kapata tu mwenyewe ni Abdul Sykes! Hapana kila mmoja na historia yake

Nani kasema hao akina mama unaoeleza ni 'Uongo'

Usitafute kitu cha kutumbukiza kutuondoa kwenye hoja.

Hoja ni kuwa Abdul Sykes hakumpokea Nyerere !
Kwamba Abdul hakumuona Dar kwa mara ya kwanza , alikutane naye kabla
Kwamba Nyerere aliakwa mkutano Mkuu, hakuzamia tu kutoka Tabora

Kwamba Nyerere alikula mayai kwa Abdul Sykes hilo tutabisha vipi ? Alikula !
Sijui kama aliweza kukunja chapati! Sijui kama aliweza kufinyanga Biriani! tena akiwa na Kaptula.
Nguruvi,
Unapenda sana kejeli.

Hakuna shida.
Nimeandika kitabu na kinasomwa sasa mwaka wa 24.

Leo ipo historia ya Chuo Cha CCM Kivukoni (1981) na ipo yangu (1998) na ipo ya akina Shivji (2020).

Uwanja bado uko wazi.
 
Picha safi kabisa na nina uhakika dua ilimfikia, kwani alisafiri salama na kurudi salama, si unajua tena mambo ya Dua.

Mzee hakuna Uwongo kwani dhana haina uwongo mzee au?

Huo mtaa wa Lindi kumbe ulikuwa unaitwa Kirk st? Daktari Kirk? au

Mzee wangu wala usikwazike, kila mwanadamu ana historia yake na jamii yake. Tutakubaliana hapo. Nashukuru kwa hadithi. Walakin hadithi nilizofundishwa ni kuwa Waarabu kama vile Watu wa ulaya 'wazungu' walitufarakanya kwa Biblia upande mmoja na fimbo upande mwingine, Quaran upande mmoja na upanga upande mwingine, sasa leo hii ndio unaona hapa tunayo misuguano ya "Ustaarabu" na Uungwana au nimekosea? Au Historia haitufanyi hivyo?

Asante lakini kwa 'Hadithi' lakini tukubaliane kuwe dhana ya Historia au Hadithi unazotuhabarisha zina mtazamo wa kendeleza mfrakano wa Kale kati ya 'Waislamu' na 'Wakristo' sasa sie Waungwana tunaropoka ropoka tu bila kujua tunapigana Vita siyo yetu au ni seme sio vita yangu 'Mwafrika'.

Alamsiki Mkuu
Syll...
Historia au ''hadithi,'' kama uitavyo hukuwa unaijua hadi pale uliposikia ''hadithi, hadith,'' kutoka kwangu nawe ukaitika, ''Hadithi njoo utamu kolea.''

Mwanangu Mwanasiti kijino kama chikichi...

Mwalimu wangu Sheikh Haruna kanisomesha mlango wa adabu yaani kuheshimu watu na kanambia nikubali kuwa kama mtu anavyotaka niwe.

Anasema ikiwa mtu anataka kunifanya mimi ni mjinga yeye ndiye hodari na mjuzi basi mimi nisimvunje niikubali ile nafasi aliyoniweka.

Hukupata kuita ''hadithi,'' yaliyokuwa katika kitabu cha Kimambo na Temu (1969) na ''Historia ya TANU,'' (1981):

Nimerejea kukufahamisha kuwa sikujaaliwa kipaji cha kupigia watu hadithi:

PUBLICATIONS/RESEARCH PAPERS/ARTICLES
  1. The Life and Times of Abdulwahid Sykes 1924 –1968 The Untold Story of the Muslim Struggle against British Colonialism in Tanganyika, Minerva Press London, 1998 translated into Kiswahili as Maisha na Nyakati za Abdulwahid Sykes 1924-1968 Historia Iliyofichwa Kuhusu Harakati za Waislam Dhidi ya Ukoloni wa Waingereza, Phoenix Publishers, Nairobi, 2002.
  2. The Torch on Kilimanjaro, Oxford University Press, Nairobi, 2006
  3. Contributing author for an African anthology: The Mermaid of Msambweni and Other Stories, Oxford University Press 2007, Nairobi.
  4. Contributing author Dictionary of African Biography (DAB), Oxford University Press 2011, New York.
  5. Uamuzi wa Busara, Abantu Publications 2008, Dar es Salaam.
  6. Watu Mashuhuri Katika Uhuru wa Tanganyika No. 1, Ibn Hazm Media Centre, 2018, Dar es Salaam.
  7. Watu Mashuhuri Katika Uhuru wa Tanganyika No.2, Ibn Hazm Media Centre 2018, Dar es Salaam
  8. Dar es Salaam na Wazalendo Wake Mashujaa Katika Kupigani Uhuru wa Tanganyika Ibn Hazm Media Centre 2018, Dar es Salaaam
  9. Watu Mashuhuri Katika Kuulingania Uislam Tanzania, Sheikh Ilunga, Ibn Hazm Media Centre 2018, Dar es Salaam
  10. Dola, Kanisa na Tatizo la Udini Tanzania, Ibn Hazm Media Centre, 2018, Dar es Salaam
  11. The School Trip to Zanzibar, Africa Proper Education Network 2020, Dar es Salaam
  12. Rajabu Ibrahim Kirama, Jemadari wa Vita Kuwa Jemadari wa Uislam, Readit, 2020, Dar es Salaam
  13. In Praise of Ancestors (1987) Africa Events (London).
  14. Abdulwahid Sykes: Founder of Political Movement (1988) Africa Events (London).
  15. Islam and Politics in Tanzania (1989) Al Haq International (Karachi)
  16. The Plight of Tanzanian Muslim (1993) Change (Dar es Salaam).
  17. Tanzania - The "Secular" Unsecular State (1995) Change (Dar es Salaam).
  18. The Question of Muslim Stagnation in Education in Tanzania - A Muslim Riddle (Paper presented at the Conference of the Global World of the Swahili Intercultural Dialogue on the Indian Ocean Zanzibar, February 20 - 23, 2003).
  19. Islamic Education and Intellectualism in Eastern Africa ‘Themes from the Pulpit in Tanganyika (Tanzania Mainland) 1800 – 2000’ (Paper presented at International Symposium on Islamic Civilisation in Eastern Africa Kampala, Uganda organised by the Islamic Conference Research Centre for Islamic History, Art and Culture (IRCICA), Istanbul and the Islamic University in Uganda, Mbale December 15th – 17th 2003).
  20. Sheikh Hassan bin Ameir - The Moving Spirit of Muslim Emancipation in Tanganyika (1950 – 1968) (Paper presented at Youth Camp Organised by Zanzibar University, World Assembly of Muslim Youth (WAMY) and Tanzania Muslim Students Association (TAMSA) 27th February – 4th March 2004).
  21. Islamic Movement and the Christian Lobby in Tanzania - the Experience of the late Prof. Kighoma Ali Malima (1938 – 1995) (Paper Presented to Tanzania Muslim Students Association (TAMSA) Sokoine University of Agriculture (SUA) Morogoro 11th April 2004).
  22. Terrorism in East Africa the Tanzanian Experience (Paper Presented at the Conference on Islam, Terrorism and African Development University of Ibadan, Nigeria 8th - 10th February 2006).
  23. Al Marhum Sheikh Kassim bin Juma bin Khamis (1940 – 1994) and the Pork Riots of 1993. (Paper Presented at the Regional Conference on Islam in Eastern Africa: Islam Encounter with the Challenges of the 21st Century 1st - 3rd August 2006, Kenyatta University, Nairobi.
  24. Muslim Bible Scholars of Tanzania – The Legacy of Sheikh Ahmed Deedat (1918 – 2005) Paper Presented at the International Symposium on Islamic Civilisation in Southern Africa Organised by The Organisation of Islamic Conference Research Centre for Islamic History, Art and Culture (IRCICA) The National AWQAF Foundation of South Africa (AWQAF SA 1 – 3 September 2006 University of Johannesburg.
  25. Tanzania: A Nation Without Heroes Seminar Organised by IFRA French Institute for Research in Africa and BIEA British Institute in East Africa 23rd and 24th September 2013 at IFRA Nairobi.
  26. Awards: Several Awards
  27. Visiting Scholar: (2011)
  28. University of Iowa, Iowa City, USA
  29. Northwestern University, Chicago, Illinois, USA
  30. Zentrum Moderner Orient (ZMO), Berlin.
  31. OTHER COUNTRIES VISITED
  32. Zambia, Ethiopia, Great Britain, Swaziland, Msumbiji, Zimbabwe, Zambia, Sudan, Egypt, Saudi Arabia, United Arab Emirates, Oman, Yemen, Uganda, Switzerland, Iran, France, Netherlands, Turkey and Abu Dhabi.
 
Huyu mzee udini unampoteza.

Kizazi cha karne ya 21 hatutaki udini wenu.

Msituharibie nchi yetu kwa vihistoria vyenu vya kutungatunga.

Huyu mzee hovyo kabisa.
 
Sang'undi,
Matusi siwezi kujibu.
Unamjibu vipi mtu anaekutukana?
 
Mzee wangu hujakosea
Nianze na kukuhadithia- Wakati nasoma jibu lako nilikuwa nakula, na ni kweli niliitikia "...utamu njoo utamu kolea na nilikenua vijino haswa!

Sasa ujue tu makande niliyokula yalikuwa na sukari na utamu ukakolea sana tu kwavile kijino changu chikichi kilikuwa na ganda la harage... we wacha tu!

Mzee wangu sijapata kuwa na mwalimu wa adabu, nimejifunza kwa kukosea mara nyingi(I am a work in progress) lakini kwa kukusoma inawezekana nilikukwaza-pole vilevile kuna ukweli hapo kuwa mie ni hodari na nimjuzi walakin ujuvi wangu sio wakifidhuli. Huwa najitahidi sana kutofika huko, mbali ya na hayo juu, huwa napenda kuelimishwa-Asante na unisamehe kwa kukwazuka.

Mzee, Kwa kukusoma kweli umebobeka na sikuwa na uhitaji wa wewe kunidhihirishia hili kwa mlolongo mrefu wa himidu(accolades) ninauhakika na Ubobezi wako, hauuliziki.

Mzee sina uhaba wa uelewa na sijashikwa na fadhaa yakuwa katika kutuhadithia huwa(wewe) una lengo la mfarakano-na kama siyo hivyo basi una lengo la kuuza vitabu kwa uhadaa-hayo ndio maoni yangu kwa maandiko yako humu jamvini walakin siyo yote bali baadhi-yana dhana ya udini- lakini simaanishi wewe binafsi una haiba hiyo au ndio haiba yako.

Mzee binafsi sipendi kushushiwa hadhi, sipendi kumshushia hadhi binadamu yeyote na hususani 'Mwafrika' mweusi. Hapo tutalumbana tu na hata kuonekana nina ufidhuli Naomba unielewe

Mzee wangu ni Asubuhi, nakutakia siku njema isiyo na mkwaziko. Tanzania ni yetu sote, tuelimishane. Asante kwa ukarimu tutaendele na hata tufike kujibishana kwa hoja ya mada iliyopo hapa.
 
Syll ...
Mimi sina sababu ya kutaka kuingia katika "gimmicks," ili niuze vitabu.

Publishers wenyewe ni wajuzi wa hilo hivyo marketing ya kitabu haachiwi mwandishi.
 
Mzee MS, acha kudanganya. Kila posting yako ya tatu au ya nne kwenye nyuzi zako wewe huchelewi kukipigia promo kitabu chako cha Abdul Sykes kwa kubandika picha ya cover, na hapohapo kutusihi wanajukwaa tukinunue na kukisoma. Vyote hivi unafanya totally unsolicited! Ni wazi hao publishers wako hawana hela kwenye bajeti yao kufanya promo ya hicho kitabu. Hakiuziki.
 
Mzee MS, acha kudanganya. Kila posting yako ya tatu au ya nne kwenye nyuzi zako wewe huchelewi kukipigia promo kitabu chako cha Abdul Sykes kwa kubandika picha ya cover, na hapohapo kutusihi wanajukwaa tukinunue na kukisoma, vyote hivi unafanya totally unsolicited! Ni wazi hao publishers wako hawana hela kwenye bajeti yao kufanya promo ya hicho kitabu. Hakiuziki.
Gold...
Hapana naweka picha ya kitabu kama sehemu ya niliyoandika msomaji aone kwa jicho lake kinachojadiliwa.

Siweki kama promo.
Kitabu kinauzika kuliko mategemeo yangu.
 
jamani mmemshukia sana mzee mohamed said .... vijana nadhani kwa sasa mumuwache apumzike kwa amani. nadhani atakuwa amejifunza kuwa watu wapo makini na hawadanganyiki kamwe. hayo mengine ni kibinadamu tu anakosea... msameheeni wajameni. tumeona mchele ni upi na chuya ni zipi. miaka hii ni ngumu kuwadanganya vijana hata ukitaa kupitia wenye dini au kabila....wanakuruka na kukufanya ujisikie mnyonge na mpweke.
 
Gold...
Hapana naweka picha ya kitabu kama sehemu ya niliyoandika msomaji alone kwa jicho lake kinachojadiliwa.

Siweki kama promo.

Kitabu kinauzika kuliko mategemeo yangu.
Hoja zako hazina mashiko MS. Kitabu kitakuwa kimedoda kimauzo mzee. Inabidi ufanye jitihada za ziada watu angalau wafahamu bado kipo sokoni. Lakini pamoja na jitihada zako zote miaka nenda, miaka rudi, kitabu bado hakiuziki. Publishers watakuwa wamepata hasara.
 
Back
Top Bottom