Historia ya uundwaji wa Mikoa Tanzania

Historia ya uundwaji wa Mikoa Tanzania

Asante ila kwanza kabisa andiko lako hujalitendea haki katika historia ya mikoa Tanzania rudi upya. Pili, majimbo mliyakataa sasa hiyo ya mikoa ni administration blocks tu kurahisisha wananchi "kutawaliwa"
 
Jaribu kufuatilia namna mipaka ya mikoa na wilaya inavyowekwa utagundua kuwa inatenganisha makabila na tamaduni. Hii ni hatari kwa umoja wa kitaifa!
Hiyo ni yako mkuu halafu utakuwa na ukabila balaa..
 
Ni shida sana, ilivyoletwa kigamboni na ubungo watu hawakulalamika, Ila kuundwa Chato itakuwa ni ukabila!!

Wengi huwa wanaongea wasichokijua kwa undani, from Kakonko mpaka Ujiji ni masaa 5, from Kakonko to Chato almost masaa 2 na nusu, sawasawa na watu wa ngara, mtu anatoka Kabanga anaenda Bukoba mjini kwa shida ya kimkoa watu hawaoni haya!

Moa wa Shinyanga ilikuwa si mkubwa sana by then lakini namna ulivyokuwa umekaa ilikuwa shida wakaamua kuugawa, Arusha pia ikazaa manyara, Rukwa ikazaa katavi, mikoa iliyobaki ni Tabora na Morogoro, mtu yuko Malinyi na ulanga anakuja Morogoro mjini safari ya masaa zaidi ya 8, ndani ya mkoa mmoja.

Katika kuundwa mikoa tunaamini serikali unaona umuhimu wake ndio maana wanaona waongeze eneo kiutawala
Mimi sikatai kugawa maeneo, lakini tuangalie vipaumbele. Unaanzaje kuipa Chato mkoa unaiacha Tabora na Morogoro? Wilaya ya Uyui mkoa wa Tabora kuna kijiji kiko km 420 toka Makao makuu ya mkoa halafu tunaiacha Tabora tunaanza na Chato?
 
Nyerere alikataza na kupinga sana haya mambo...


Tatizo binadamu wa siku hizi ni wabishi sana...
 
Ombi la kuwa na Mkoa wa Chato tulilisikia wakati wa Msiba wa JPM na halikuwasilishwa na Serikali bali Wananchi. Kama ni zuri au baya, tuwaachie wataalam wa Serikali waamue. Otherwise ni umbea na kueneza chuki.
 
Maendeleo gani mkuu unayoyasema, ya Wananchi au viongizi? Toka nipate fahamu sijasikia USA wala Ujerumani wakiongeza Majimbo kwa kuyakata mengine kwa kisingizio cha maendeleo!
Katika vitu ambavyo huwa nawashangaa wa tz ni kufananisha USA ,ulaya na Africa.itikadi zetu ni tofauti,wao walijenga miji yao kwa kuwatumia watumwa.cc tunajenga nchi yetu wenyewe.USA kila jimbo linautawala wake kalibia asilimia 80 linajitegemea
 
Maendeleo gani mkuu unayoyasema, ya Wananchi au viongizi? Toka nipate fahamu sijasikia USA wala Ujerumani wakiongeza Majimbo kwa kuyakata mengine kwa kisingizio cha maendeleo!
USA wapo tangu 1776 uwepo wa taifa lao ni tofauti na uwepo wa hili la kwetu.
 
msifurahie mambo ya kugawa mikoa, ni ukabila mkubwa sana, huu umeletwa awamu ya nne natano, tusikubali kugawana kidogo kilichopo.
Waligawa manyara kusema eti maendeleo karibu na wananchi, them hao wananchi wamepata maendeleo gani?

wanasiasa ni wapuuzi sana.
Kugawa mikoa si tatizo, tatizo ni hizo sababu za kipuuzi zinazowafanya hao wanasiasa wabovu kuigawa mikoa.

Lakini kabla sijaondoka, naomba nikuulize kuhusu hiyo orodha ya juu uliyoiweka hapa, ile ya mwanzo kabisa.
Hiyo namba 7, Nyanda, ni eneo gani lililowakilisha sehemu hiyo?
 
Anajaribu kuuponda mkoa wa Chato kwa dhana zile zile za chuki dhidi ya hayati JPM.
Hakuna lolote lililojificha kuhusu ubaya wa Magufuli katika kufanya mambo kama haya.

Magufuli hakuwa kiongozi wa kuwaunganisha raia; ilikuwa ni kama raha kwake kuona mifarakanyo ndani ya jumuia!
 
Hakuna sababu ya kuendelea kuongeza hii mnayoita mikoa maana kwanza imekaa kiutawala zaidi badala ya kuitumikia jamii.

Ninashauri hii local government iangaliwe upya mfumo wake ili watu waweze kupata huduma ya serikali kiurahisi zaidi ya ilivyo sasa. Halmashauri ziongezwe ikiwezekana katika kata ambazo zisizidi kumi iundwe halmashauri ili watendaji wa halmashauri waweze kutoa huduma kwa urahisi zaidi.

Pia kwenye kata huduma ziongozwe wapelekwe wataalam wa kutosha wenye weledi wanaoweza kuhudumia wananchi idara zote za kiserikali ziwepo ngazi ya kata k.v idara ya ardhi iwepo ngazi ya kata, idara ya sheria, maendeleo ya jamii, idara ya ujenzi n.k na mitaa isizidi 10 kwenye kila kata.

Alafu halmshauri hizo zote ziwe chini ya "majimbo" au "kanda" ambayo kwa jiografia ya nchi yetu yasizidi kumi tu. Hii itapunguza burden kwa serikali kuwa na ngazi nyingi za utawala lakini itaongeza ufanisi katika kufikisha huduma kwa wananchi.
 
Tanzania inahitaji mikoa isiyozidi mitano

Pwani
Kusini
Kaskazini
Kati
Kanda ya Ziwa

Badala ya kujikiti kwenye mifumo ya kudogosha serekali ndio kwanza wanaendelea kutengeneza mazingira ya kupeana ulaji
 
Kama hujui historia ya nchi hii bora ungefanya utafiti kwanza. Nani alikwambia kwamba Tanganyika ilikuwa na majimbo 10 wakati tunapata uhuru ? Ngoja nikusaidie ni hivi, kabla ya mwaka 1959 Tanganyika ilikuwa majimbo 8 nayo ni 1. Jimbo la ziwa 2. jimbo la Magharibi 3. Jimbo la kati 4. Jimbo la Tanga 5. Jimbo la Kaskazini 6 Jimbo la kusini 7. Jimbo la Mashariki 8. Jimbo la nyanda za juu kusini. Mwaka 1959 jimbo la ziwa liligawanywa na kupata jimbo jipya la Ziwa Magharibi, hivyo kuifanya nchi kuwa na majimbo 9 hadi tunapata uhuru mwaka 1961. Kwa taarifa yako mwaka 1974 Nyerere aliunda mikoa mitatu ambayo ni Dar es salaam, Lindi na Rukwa. Mkoa wa Manyara uliundwa wakati wa Mkapa na mikoa ya Geita, Njombe, Katavi, Simiyu na Songwe imeundwa wakati wa Utawala wa Kikwete. Upo hapo ?
 
Baada ya uhuru iliundwa mikoa 17 siyo 16. Nayo ni Mwanza, Pwani, Morogoro, Tanga, Ziwa magharibi, Mara, Shinyanga, Tabora, Iringa, Mbeya, Arusha, Kilimanjaro, Mtwara, Ruvuma, Singida Dodoma na Mara.
Ningeshangaa kama ungemaliza kuandika uzi wako bila kuwataja Watu wa Kilimanjaro[emoji23][emoji23]
 
Binafsi nisingekuwa na tatizo kama mikoa mipya ingetokea Morogoro, Tabora au Pwani.
Tena Morogoro unapatikana mkoa huko wa Kilombero, Ifakara, Malinyi, Mbingu, Ngeta, Mlimba...wala hauibi wilaya wala eneo la mikoa mingine.
Hakuna mgogoro wakati wa ugawaji wa mipaka. Kunakuwa na migogoro ya ardhi katika hili zoezi la umegaji ardhi.

Ila Chato aisee hapana! Hii nchi yetu sote

Everyday is Saturday............................... 😎
Hakuna cha kuiba mikoa. Nchi ni moja Tanzania, wewe vipi ?
 
Back
Top Bottom