History inapingana na wanaosema ''HAKUNA MUNGU'': The simple research you can do to prove it.

Mkuu ninakubaliana kabisa na angalizo lako.

Waswahili wanasema mtoto umleavyo ndivyo akuavyo au samaki mkunje angali mbichi.

Elimu haipatikani darasani peke yake, hata mazingira yanayotuzunguka ni kisima cha kuchota elimu inayomfundisha mwanadamu jambo fulani pale anapoangalia katika mtazamo unaojengwa na hoja ambazo chimbuko lake ni WHY?.

Watanzania wengi bado tunakulia katika mazingira ya uwoga kwa maana kuwa mila na desturi zetu zimetuweka katika mazingira ya kutokuwa wadadisi na kuhoji hoji. Mtoto anayeonekana kuanza kujenga tabia ya kudadisi na kuhoji hoji huwa anawekwa kwenye kundi la watukutu ambapo hata hoja zake huwa zinaanza kupuuzwa na kupingwa matokeo yake anakosa hata msukumo katika uchunguzi.

Mazingira haya yanasababisha watoto kutokuwa wabunifu, as a result, hata akili inakuwa dormant or passive katika kufanya uchunguzi wa kila kitu kiasi kwamba anajikuta amejenga tabia ya woga na kukubali tu kila kitu kwa vile aliyesema ni mtu ambaye umri wake ni juu yake au 'superior'.
 
Hapo unapodai aya zilishushwa
Mimi najua Vitabu hivi vipo katika Maktaba na km Torati iliandikwa na Mose haikushushwa Amri 10 kashuka nazo Sinai alikopewa na YEHOVA
back to the thread
Hivi kweli km MUNGU hayupo hii Dunia itatawalika, hamuoni kuweka siku za kuabudu ni kupunguza machukizo baina yetu?
Na km kweli yupo kwanini asimuangamize shetani anayeishi milele kuongeza kundi la wanaokuwa -ve kwa miungu ya Baniani , Budha, Mulungu (wa wagogo) Mndumi, Allah (wa Waislam) YESU ( kwa Wakatoliki) nk
By Aboo Treka

Mungu mwenyewe kaniandikia.

humu ndani kuna waliokutana na MUNGU kwa hiyo tusiwabishie ngojeni waweke Proof km hizi
 
nahisi tunatofautiana imani kwanza mkuu sisi kwenye dini yetu (islam) kitabu cha qur an ni maneno ya mungu yaliyoteremshwa kupitia kwa nabii muhamd (s.a.w) na wala sio kwamba vitabu vipo maktaba vikakusanywa pamoja kikatengenezwa kitabu kimoja kikaitwa qur an na katika kila aya ambayo ilikuwa inashuka kuliko kuna sababu ya hiyo aya kushuka kwa wakati huo,

na kama kweli kuhusu mungu yupo kwanini asimuangamize shetani nilijarribu kumjibu hili swala Kiranga kwamba ni kwa sababu mungu ametupa akili ya kufikiria lakini pia ametupa muongozo wa kuufuata as long as tuna akili so hatuwezi kupotea na shetani hawezi kututeka tukamfuata yy iwapo tutazitumia akili zetu vizuri

kuhusu hilo swala la kumuona mungu as far as i knw hakuna mtu ambae amewahi kumuona mungu(binaadamu) labda kama siyo mungu huyu mmoja tunaemkusudia sisi wote.
 
Last edited by a moderator:

Ukwaju.

Very important point.

I repeat.

Very important point.

Kabla ya kwenda kwenye nuances za usefulness of the god idea, ni lazima tukubaliane kwenye reality.

Kama mungu hayupo, na uzuri wa idea ya mungu ni kutisha watu tu wasifanye mabaya, then habari nzima ya mungu inakuwa imejengwa katika uongo.

Na si kweli kwamba watu hawawezi kutenda mema bila kuamini mungu.

Kuna secular humanists kibao hawaamini mungu lakini wanatenda mema.

Kuna Buddhists kibao hawaamini mungu lakini wana a better morality code than Christians.

Kuna Wagiriki walioishi maelfu ya miaka kabla ya Kristo hawakuamini kuwapo kwa roho wala mungu lakini walikuwa na a code of.morality ambayo ilikuwa truthful and better than the Judeo Christian code we have.

Kwa hiyo kusema binadamu hawezi kutenda mazuri bila imani ya mungu ni kujibweteza.

Na tumeona makasisi wanaoamini mungu wakiwala.witi (ashakum si matusi) watoto wadogo kihayawani.

Tatizo naweza kuwa nabishana na watu easiojua falsafa za secular humanists, Buddhists wala ancient Greeks.
 
Last edited by a moderator:

Kabla ya mungu kutupa akili ya kufikiri na kuumba ulimwengu, alikuwa na uwezo wa kuumba ulimwengu ambao mabaya hayawezekaniki.

Shetani hawezi kutokea na binadamu hawezi kuwaza mabaya wala kupatwa na mabaya.

Kwa nini hakuumba ulimwengu huo?
 
Wapi Mungu aliumba umlimwengu wenye Mabaya? Unaweza tupa USHAHIDI HAPA?

Usiwe unauliza ujinga. Kama hujui kitu kaa kimya.

Sasa niletee ushaidi wa Mungu kuumba ulimwengu wenye mabaya..

USIKIMBIE BANA
 
Wapi Mungu aliumba umlimwengu wenye Mabaya? Unaweza tupa USHAHIDI HAPA?
Usiwe unauliza ujinga. Kama hujui kitu kaa kimya.
Sasa niletee ushaidi wa Mungu kuumba ulimwengu wenye mabaya..
USIKIMBIE BANA
yaani mabaya yote huyaoni wanayosema ni ya Shetani
basi anzia na Sodoma na Gomora au kwenye Jiwe la chumvi la mke wa Luttu
ElNino na majanga yote ya Vita na njaa huko soamalia ma DRC

Tumapochangia kumuita mwenzio mjinga unaonesha kabisa hakuna MUNGU maana ni dharau na kibri vilivyoandikwa katika Vitabu vyote vya ....
wewe changia huyo mungu umekutana wapi akakufundisha ujinga?
 
Kabla ya mungu kutupa akili ya kufikiri na kuumba ulimwengu, alikuwa na uwezo wa kuumba ulimwengu ambao mabaya hayawezekaniki.
Shetani hawezi kutokea na binadamu hawezi kuwaza mabaya wala kupatwa na mabaya.
Kwa nini hakuumba ulimwengu huo?
cc Mndengereko hapa lazima atarudi nyuma pale shetani alipojiumba maana hakuumbwa kutokana na vitabu
 
Last edited by a moderator:

Nimekwambia niletee ushaidi wa kuumbwa na Mungu. Huwa hatusemi tuu bila ya ushaidi. Ukiweka madai, tuletee ushaidi kusaidia madai yako. Grow up JF.
 
cc Mndengereko hapa lazima atarudi nyuma pale shetani alipojiumba maana hakuumbwa kutokana na vitabu

Kama shetani kajiumba, hajaumbwa na mungu.

Kama hajaumbwa na mungu, habari ya Biblia, Quran na mapokeo mengine kwamba mungu ni muumba vyote ni uongo.

Kama biblia na quran vimesema uongo katika hili, vimesema uongo katika mengine mangapi?
 
Last edited by a moderator:

Ushaondoka kwenye suala la mungu yupo au hayupo, umeingia kqenye suala la kuuliza, je, kama mungu hayupo, kudanganya kwamba yupo ili ku maintain order ni kitu kizuri au kibaya.

Hili ni swali tofauti.

Lazima ukubali kwamba mungu hayupo ili kulijadili seali hili kwa undani.

Kwa sababu msingi wake ni kutokuwepo kwa mungu.
 
Hukujibu swali.

Nimekuuliza kwa nini mungu kaumba ulimwengu ambao ubaya unawezekana na shetani anawekana wakati ana uwezo wa kuumba ulimwengu wowote ule, ukiwambo ule ambao ubaya hauwezekani kwapobwala shetani hawezekani kuumbika?

Hujajibu swali hili.
 
Last edited by a moderator:
Nimekwambia niletee ushaidi wa kuumbwa na Mungu. Huwa hatusemi tuu bila ya ushaidi. Ukiweka madai, tuletee ushaidi kusaidia madai yako. Grow up JF.

Wewe toa ushahidi wa mwanadamu kuumbwa na mungu.
 
Wapi Mungu aliumba umlimwengu wenye Mabaya? Unaweza tupa USHAHIDI HAPA?

Usiwe unauliza ujinga. Kama hujui kitu kaa kimya.

Sasa niletee ushaidi wa Mungu kuumba ulimwengu wenye mabaya..

USIKIMBIE BANA

By your cosmogony, uwezekano wa shetani kuwepo kwenye ulimwengu huu umeumbwa na nani?
 
Hujajibu swali.

Na hatujawahi kuishi dunia ambayo haina ubaya, kwa hiyo swali lako halijibiki na mtu wa dunia hii.

Bora dunia ambayo haina ubaya lakini watu hawajui wema (kwa sababu hakuna ubaya wa ku u distinguish wema na ubaya) kuliko dunia yenye ubaya na wema ili tu watu waujue wema.

Kama una watoto saba, ukaamua kwa makusudi umuue mmoja ili tu wale wengine sita waweze kuthamini maisha kwa kukijua kifo, wakati unaweza kuzuia kifo na kuwaeleza tu wanao mpaka waelewe kwamba kuna kifo, utaitwa muuaji na kufungwa jela.

Sasa kwa nini mungu mwenye uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote tumuangalie kwa a more lenient standard?

Alishindwa kuwafanya binadamu wajue mabaya na mema bila ya ulimwengu kuwa na mabaya?
 
Wewe toa ushahidi wa mwanadamu kuumbwa na mungu.

Unakimbia dai lako. Unaona tabia ya kudandia treni kwa mbele?
Wapi Mungu aliumba umlimwengu wenye Mabaya? Unaweza tupa USHAHIDI HAPA?
Usiwe unauliza ujinga. Kama hujui kitu kaa kimya.
Sasa niletee ushaidi wa Mungu kuumba ulimwengu wenye mabaya..
USIKIMBIE BANA

Hivi tabia ya kukimbia madai unayo anzisha utaacha lini?
 
Shetani ameumbwa na mungu au katokeaje?

Ulimwengu ambao shetani anaweza kutokea umeumbwa na nani?

Hujajibu maswali.
 
By your cosmogony, uwezekano wa shetani kuwepo kwenye ulimwengu huu umeumbwa na nani?

Inaonekana hujui hata mwanzo wa Shetani. Nenda kajifunze kwanza shetani katoka wapi, ukisha fahamu, utaelewa kuwa Swali lako limekosa elimu ya Shetani.

Nani alimkataza Shetani kuwepo kwenye ulimwengu huu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…