Ng'wamapalala
JF-Expert Member
- Jun 9, 2011
- 6,811
- 6,503
Mkuu ninakubaliana kabisa na angalizo lako.Ng'wamapalala;
Matatizo makubwa jamii zetu ni watu wengi kushindwa kutumia uwezo wao wa kufikiri na kushindwa kutambua.
uwezo wa akili za binadamu kufanya ubunifu.
Vilevile pamoja na kuwa ubongo au akili za binadamu zinaweza kufanya mambo makubwa bado unaweza kudanganywa na kuamini vitu visivyo na ukweli kwa muda mrefu. Kwa mfano niliangalia mazishi ya Kim Jong Il and yale ya Kim Il-Sung, waliokuwa viongozi wa Korea ya kaskazini. Sikuelewa kwanini walifanywa kama Miungu na watu kuamini.
Waswahili wanasema mtoto umleavyo ndivyo akuavyo au samaki mkunje angali mbichi.
Elimu haipatikani darasani peke yake, hata mazingira yanayotuzunguka ni kisima cha kuchota elimu inayomfundisha mwanadamu jambo fulani pale anapoangalia katika mtazamo unaojengwa na hoja ambazo chimbuko lake ni WHY?.
Watanzania wengi bado tunakulia katika mazingira ya uwoga kwa maana kuwa mila na desturi zetu zimetuweka katika mazingira ya kutokuwa wadadisi na kuhoji hoji. Mtoto anayeonekana kuanza kujenga tabia ya kudadisi na kuhoji hoji huwa anawekwa kwenye kundi la watukutu ambapo hata hoja zake huwa zinaanza kupuuzwa na kupingwa matokeo yake anakosa hata msukumo katika uchunguzi.
Mazingira haya yanasababisha watoto kutokuwa wabunifu, as a result, hata akili inakuwa dormant or passive katika kufanya uchunguzi wa kila kitu kiasi kwamba anajikuta amejenga tabia ya woga na kukubali tu kila kitu kwa vile aliyesema ni mtu ambaye umri wake ni juu yake au 'superior'.
