Kiranga
Platinum Member
- Jan 29, 2009
- 78,790
- 128,275
its not about kitu kilicho recent zaidi its about wewe kuwa na open mind na kujiridhisha kwamba mungu yupo,.
Recent is relevant in the context that I have argued your arguments with Jehovah Witnesses in the early nineties, wakakosa majibu.
Kubali.The argument form complexity is defeatist to any theist. Kwa sababu itataka mungu awe na muumba na muumba wake awe na muumba bila mwisho.
Iondoe hiyo argument tuendelee na nyingine.
kucopy and paste siyo ishu kama ulivyoishikialia what maters ni hoja na facts, alafu sio kila kitu ni copied and paste nimesoma nimeelewa ndo nimeleta hoja hapa baada ya kuchambua na kuna vitu vingi tu nimeongezea mimi mwenyewe.....
Indeed ku copy and paste si issue, I will be the first one to tell you that there is nothing significantly new under and over the sun, hata huyo Erasto Mpemba aliyewaweka Watanzania kwenye ramani kwa kugundua "The Mpemba Effect" watu baadaye wakaja kuchunguza na kukuta Wagiriki kina Aristotle walishaandika hayo. Hiyo basis ya string theory imepatikana katika margins za vitabu vya zamani. Edgar Allan Poe aliandika kuhusu habari za black holes kabla hata ya kuwepo kwa Hubble Observatory.
Tatizo si kwamba ume copy paste tu, tatizo ume copy paste vitu vinavyo jicontradict, inaonekana wewe uliye copy na huyo aliyeandika wote hamuelewei mnasimama wapi.
Is matter/ energy neither destroyed nor created or has the universe a beginning?
You can't have both arguments! One is the direct negation of another.
kuhusu hiyo hoja ya matter and energy can neither be created not destroyed hapa nakubali nimejicontrdaict so hiyo fisrt law ya thermodyanamic iweke pembeni (asiyekubali kushindwa si mshindani) it doesnt make sense kusema mungu ni creator wa everything yet nissuport hii theory kwamba no new matter or energy that come to an existance and also there will be no any new matter or energy that will pass out of existance.
Asante kwa kukubali.
Unaona jinsi gani uliyem quote alivyo na mapungufu sasa?
Inabidi ukubali hivyo hivyo kwenye hoja ya complexity.
nyuma nilikuuliza swali kwamba unaamini uwepo wa roho,umepiga kimya umejifanya hujaona,wewe unachotaka uthibitshwe hoja za uwepo wa mungu ubishe ila kutaka kuulizwa wewe maswali hutaki???,
Siwezi kukupigia kimya wewe leo wakati nishasema kitambo hapa kwamba sikubali uwepo sio tu wa mungu, bali wa any supernatural entity.
kwa hiyo hilo linajumuisha roho, mungu, shetani, mapepo, mbingu, jehanamu, majini, uchawi, vinyamkera, popobawa, the loch ness monster etc etc.
As long as ni super natural entity.
tena kuna mdau akakuuliza unaamini maisha baada ya kufa ukaanza blah blah wakat majibu mawili tu huamini au unaamini??,
Obviously hujanisoma. Again, you are late to this party.
Sitaki kuamini, nataka kujua. I am not interested in kuamini, kwa sababu kuamini hakuna sheria. Unaweza kuamini chochote ilimradi huvunji sheria. Kuna maazimio ya Umoja wa Mataifa kuhakikisha kila mtu ana haki ya kuamini anachotaka kati9ka mambo haya.
On that note, nataka waamini wajue kwamba mimi siwaandami wao. Mimi naongelea falsafa ya dini, si imani. Naongelea ujuzi.
Ndiyo maana mtu akiniuliza "unaamini kuna maisha baada ya kifo", response nzuri kwangu si kufupisha mjadala na kusema "naamini" au "siamini".
Nauliza, kwa uthibitisho na ushahidi gani?
Maana naweza kuwa sijapata uthibitisho wa kukidhi misingi ninayoikubali, lakini mtu akanipa uthibitisho huo hapa JF. Kwa hiyo kabla ya kusema naamini au siamini , tuongelee uthibitisho na ushahidi kwamba kuna maisha baada ya kifo.
tunavyokuuliza hivi tuna maana yetu, haya nakuuliza kwa mara nyingine tena unaamini uwepo wa roho katika mwili wa binaadamu??? Kama hutaki kujibu hilo kama mwanzo nakuuliza swali la pili unaamini maisha baada ya kufa,acha blah blah,majibu mawili tu hapo.
Kwa nini nikubali uwepo wa roho? Roho ni nini? Unathibitishaje kwamba ipo na si hadithi tu?