nimekuuliza mtu akifa nini kinaondoka kwenye mwili wake mpk tunasema mwili wa marehemu kama sio roho ambayo wewe huiamini hapa najua utasema pumzi inakatika haya niambie kuna uhusiano gani kati ya mtu kufa na pumzi kukatika nani anayeikata hiyo pumzi/ Anauchukua huo uhai??
Uhusiano kati ya kufa na pumzi kukatika ni kwamba pumzi ikikatika damu inakosa oxygen na rigor mortis ina set in. You don't need a soul there.
Kuhusu mapepo unasemaje ni mental condition wakati yanaweza yakampanda mtu either kwa bahati mbaya au makusudi akiamua ayapandishe??? Na yakimpanda mtu anakuwa haelewi nini yanafanya/hana controll na mwili wake ingawaje pumzi yake bado inakuwepo/anakuwa hajafa na hilo pepo pia lina pumzi yake???
Umesoma mental conditions zote na kuzimaliza?
Kuhusu sababu za kutokea maovu duniani/disaster and disease nishakujibu mara kadha wa kadha kwamba magonjwa yanatokana na siisi kuacha maamrisho ya mungu na jinsi alivyotutaka tuishi kwa mfano ukimwi-tuache zinaa, kipindupindu na magonjwa mengine yanayotokana na uchafu yote tunaweza kuyaepuka tukiwa wasafi na tukifanya mazoezi,na kula kwa kiasi tutapunguza magonjwa mengi yanayotokana na sisi kula sana/kula hovyo kuhusu disaster ni kutokana na sisi kumuasi mungu so moja anatuadhibu hapa hapa duniani pili anatupima imani zetu kwamba je tutaendelea kumfanya mungu tegemeo letu hata katika majanga/matatizo au tutamkumbuka katika raha tu??
Na ukisema kwa nini mungu anaruhusu bad things hapen to good people nishakujibu na pia ukijiuliza swali hilo at the same time jiulize why god has allowed good things to happen to bad people ??
Hata hujaelewa swali unasema umelijibu mara kibao.
Wewe swali unalotaka kulijibu ni lile la kwa nini kuna maovu. Kwa mfano, kwa nini mungu anaachia watu wanakufa kwa UKIMWI. Explanation yako ni kwamba watu wenyewe ndio wanaofanya zinaa.Na hivyo ndio wanaojisababishia UKIMWI (ingawa hata hili jibu halitoshi, kwa sababu kuna watoto wadogo wanazaliwa na H.I.V bila ya kufanya zinaa yoyote)
Kwa hiyo tunaona kwamba, ingawa swali ulilojibu si nililouliza, hata hilo ulilojibu halijibu swali uliloamua kulijibu kikamilifu.
Umesema maovu ni matokeo ya matendo yetu, wakati wengine wanapatwa na maovu kabla hata hawajapata akili ya kutenda maovu wao useme yamewarudia kutokana na matendo yao.
Mtoto mdogo anapopatawa na mabaya anapatwaje na mabaya kwa makosa yake?
Lakini kama nilivyosema mwanzo, hili swali, ingawa umeliboronga, si lile nililouliza.
Swali nililouliza ni, je, pale mungu alipokuwa anauumba ulimwengu huu, kwa kuwa yeye ni mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na mwenye upendo wote, kwa nini hakuuumba ulimwengu ambao hauruhusu mabaya, hauruhusu maovu, kiasi kwamba hata huyo binadamu mnayemlaumu kwamba mabaya yanampata kwa sababu yeye anafanya mabaya asiweze kufanya mabaya in the first place?
Kwa sababu ukifikiria sana haya mambo, utajiuliza kwa nini binadamu anafanya mabaya?
Utasema, anafanya mabaya kwa sababu mbalimbali, malezi, DNA, ujinga, shetani etc. Kwa mujibu wa mapokeo yenu mnamuweka mbele sana shetani kama baba wa ubaya.
Lakini swali linakuja, huyu shetani katokeaje? Kajiumba mwenyewe au kaumbwa na mungu?
Kama kajiumba mwenyewe basi mungu si muumba vyote na muweza yote.
Kama kaumbwa na mungu, basi mungu ndiye katuletea huyu shetani, na alimjua atakavyokuwa hata kabla hajamuumba, kwa sababu kwa mujibu wenu mungu anajua yote.
Sasa kwa nini alikubali kumuumba huyu shetani wakati akijua kwamba huyu shetani ataleta mabaya duniani?
In fact I will go a step further back.
Kwa nini mungu, kabla ya kumuumba shetani, aliumba ulimwengu ambao shetani na mabaya yote yanayowezekana kufamnyika leo, yawezekane?
Kwa nini mungu hakuumba ulimwengu ambao zinaa na UKIMWI haviwezekani?
Alishindwa au hakutaka tu?
Kama alishindwa, basi si muweza yote.
Kama aliweza ila hakutaka tu, basi hana upendo hivyo, kwa sababu alikuwa na uwezo wa kuumba ulimwengu usio na mateso, lakini hakuutumia.
Kwa nini huyu mungu wenu alipokuwa anaumba ulimwengu hakutaka kuumba ulimwengu ambao mabaya hayawezekani kufanyika?