Hitimisho langu juu ya swali la Mungu na Atheists

Nithibitishe nini na ili iweje?

Hiyo sio kazi yangu kumbuka hapa tunafata kanuni na kanuni ambayo nyie mmeichagua ni kuwa anayepinga ndio mwenye jukumu la kuthibitisha

Kama mmeshindwa kuthibitisha mimi sio Mungu wa kweli basi hoja yangu ya kusema Mungu mnayesema yupo, hayupo basi itakuwa na mashiko bila kuzingatia kushindwa kwangu kutoa huo uthibitisho wa kutokuwepo kwake
 
lakini mkuu tukubaliane jambo moja Mungu yupo ila Apo kwenye dini apo tumepigwa nahisi kabsa dini haina uhusiano na Mungu kabsa, japo vitabu vya dini kuna namna vinaongea kaukwel ila vingi ni kwa madhumuni ya interest zao tu.
Mungu Yupo, huo ni ukweli. Nakubali.

Suala la dini kwa hakika ni suala la kujadili kwa undani sana, nakubaliana nawe.
 
Hoja ulivyoiweka vyovyote itavyoleta majibu nakuomba ufanye hili….

Je wewe ni Mungu kweli? (Usinijibu mimi jiulize wewe na nafsi yako tu)

Haijalishi maneno utayapangaje… yataleta majibu unayoyataka… hilo halibadili ukweli.

Mfano mtu ameiba, na ameiba kweli yeye mwenyewe anajua kaiba, lakini ni mtu makini hivyo akaficha ushahidi wote na katu haikugundulika kuwa kaiba, mbele ya mahakama ushahidi ukakosekana… Hakimu akamtangaza kuwa hana hatia.

Je, ni kweli hana hatia?
Au mizani iliyotumika kumpima ina kasoro mahali?
 
Wewe si umezaliwa juzi tu,umeviumbaje vitu ulivyovikuta!?
 
Eti jiulize we na nafsi yako

Haya maswali yako yamekaa kibinadamu binadamu yalikuwa sahihi kuuliza kwa kiumbe mwenzako

Huku ni kumkosea adabu Mungu wako
 
Tomaso hadi muone kwa macho
 
Lakini waanzilishi wa dini zote hawakuwa watawala, ikiwemo kuteswa na kuuliwa na hao watawala.Hoja mbili hizi unasemaje lengo la dini ni kutawala watu.
 
Sasa unazungumziaje watu wa Buddha ambao hawaamini mambo ya Mungu ila wanaamini katika kuachana na tamaa za kidunia kufikia level inaitwa nirvanna
Nimewazungumzia kwa muktadha wa “Dini” na si Mungu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…