May Day
JF-Expert Member
- May 18, 2018
- 6,311
- 9,027
Ni muda mrefu sasa nimekuwa najiuliza hili swali, haswa ninapokuwa na kijana Wangu mdogo wa kiume mwenye umri wa miaka kumi.
Kuna wakati tupo sebuleni tunasikiliza Redio au TV, na habari inayosikika ni kuhusu Mtoto aliyelawitiwa, Binti aliyepewa mimba, Mwanamke aliyebakwa n.k.
Hapa huwa linanijia swali hili haswa ninapomuangalia Mtoto na kumuona akifuatilia habari ile kwa makini:- "hivi Mwanangu hapa hahitaji ufafanuzi wowote kutoka kwa Mzazi kwa anachosikiliza? ina maana ameelewa kila kitu kwa 100%?
Je, ni nini kinamwambia kwamba hili si jambo sahihi kujadili na Mzazi? mbona mengine anakuwa huru kuuliza?..kwa mfano taarifa ikiwa ni ndege imeanguka atauliza maswali mengi huku akisisitiza kuwa yeye hatopanda tena Ndege maishani mwake n.k.
Au huwa anasubiri aende shuleni wakutane na "fundi" wao aliyesikiliza na awape ufafanuzi wa kila kitu wanachotaka kuelewa kuhusu maswala hayo? kama ndivyo, hii ni sawa? kwa nini sisi Wazazi au Waalimu tusikae hapo kati kati na kutimiza wajibu wetu kuwafafanulia?
Huwa najaribu kukumbuka nilipokuwa na umri kama wake (miaka 9-10), na mambo niliyokuwa nakutana nayo/nayasikia nikiwa shuleni...nikiwa darasa la nne tu (nakumbuka hivi kwa sababu nilihama shule ya kwanza nilipoingia tu darasa la tano) kulikuwa na baadhi Wanafunzi wenzetu walikuwa ni "watukutu" na mafundi wa kuongea matusi.
Namkumbuka Jamaa mmoja aliitwa Moses, lakini almaarufu tulikuwa tunamuita "Mozee"...huyu kulikuwa na tuhuma kuwa ni mtumiaji wa sigara bwege...huyu jamaa aliwahi kutusimulia alivyokuwa "anawapiga" (nimetumia tafsida) Ng'ombe akiwa machungani...iwe alisema ukweli au la...ila bado stori zile si zilikuwa ni nzito kwa masikio yale machanga?.
Pia namkumbuka jamaa mmoja aliyekuwa fundi sana wa kutumia matusi kwenye ule mchezo wa ushindani wa matani (natumai wengi wanaufahamu huu mchezo) yaani Wanafunzi wawili mnarushiana matani kwa kushindana na mwishoni apatikane mshindi.
Moja ya matani maarufu ya huyu Jamaa alikuwa anamwambia mwenzake "ulikuwa unapigwa...ukataka kuvunja upepo...ukamwambia jamaa..chomoa nij..be...jamaa akakwambia jamb..a humohumo" basi Wasikilizaji tuliowazunguka tunacheka sana.
Tusi lake lingine maarufu ni "Mama yako anamenya ndizi k.. inapuliza moto"..basi Washangiliaji tena tunacheeeka...hayo ni baadhi ninayoyakumbuka.
Baadae nikiwa nimeshahamia shule nyingine nilikutana na kina James, Walter n.k...nakumbuka kulikuwa na Mwalimu Mjamzito, alikuja darasani amechoka...James akatuambia Mwanamke mimba ikishafikia ukubwa ule hawezi tena kuvaa ch..pi" sasa alisikia wapi hayo sijui.
Siku moja tukiwa Darasani, dawati la mbele alikuwa ameketi Dada mmoja anaitwa Saida, alikuwa ameketi kwenye ukingo wa dawati akiwa ameiachia miguu panu, basi nakumbuka James alinionyesha akaninong'oneza na kuniambia "hapo k..ya Saida imekaa hivi" huku akinionyesha mfano kwa kutumia mdomo wake....kipindi hicho mimi hata sijui hizo k zinafananaje, kwa hiyo hubaki nakodoa macho tu na kumuamini "Mwalimu" wangu James....Dada wa kazi naye home alikuwa haachi upenyo..akiingia bafuni anaziba kila upenyo akijua hivi vidume humu ndani ni vitundu vitapiga chabo.
Lingine kali ni pale tulipoingia darasa la sita, akahamia binti mmoja anaitwa Khadija, alikua mapepe, mjanja mjanja sana, na pia kalikuwa ni karembo kwelikweli...na kalikuwa kana mambo mambo ya kikubwa kuliko umri wake....na ilisemekana kwamba huko shule aliyokuwa walimshindwa wakamfukuza...mimi nilikuwa mpole mpole na muoga muoga sana..nakumbuka siku moja aliniambia "we Katoto unataka?, kama unataka kesho uje na wembe mpya...unasikia?" hata sikumuelewa ana maana gani, nilibaki namshangaa tu..na kumuona huyu Dada ni mchokozi. Ni miaka mingi sasa lakini alichoniambia na sura yake ile bado haijanitoka kichwani, ingawa najua nikikutana naye leo naweza nisimtambue.
Kiufupi yapo mengi sana, ila hayo ni baadhi ya yale ninayoyakumbuka takribani miaka zaidi ya 25 baadae...na nitakuwa Mjinga kufikiri kwamba Mtoto wa sasa hivi hakutani na mambo kama haya niliyokutana nayo mimi...bila kujali kama nyumbani kwao anapitia misingi yote ya malezi...na Wazazi wangu walikuwa wanajitahidi kwa kweli.
SWALI:- ni Wazazi wangapi wanadhani Watoto wao hupitia "shule" za aina hiyo wawapo mbali nao?
SWALI:- je, Wazazi wangu walijua kama nakutana na haya huko shuleni? jibu ni hapana kwa sababu nilikuwa sithubutu kuyasema haya mbele ya Baba au Mama.
Na kama walidhani kila kitu kipo shwari, walikuwa ni Wazazi bora? je ni sahihi kwa Wazazi kukaa pembeni na kuacha dunia iwafunze Watoto wao?.
SWALI:-Vipi kuhusu hawa Wanafunzi watukutu kama kina James na wengine, nao Wazazi wao wanajua Watoto wao wako hivyo, kwamba ni Waalimu wa Wenzao huko shuleni? inawezekana wala hawajui lolote.
SWALI:-Na hivi nao huwa wanajifunza/sikia wapi hayo yote na kuja kuelezea wenzao Shuleni?
SWALI:-Ni nani atakuwa Mwalimu muafaka wa Watoto, Mwanafunzi mwenzake, Mwalimu, Mzazi, Shangazi, Mjomba n.k.
Au tuendelee kuishi kwa kujidanganya tu kwamba kila kitu ni shwari.
Maoni yangu ni kuwa ipo haja Jamii tutafute njia rasmi ya kuwafundisha Watoto wetu , mapema wajue tofauti ya Mwanamke na Mwanaume..wajue kazi ya uume na uke n.k.
Siizungumzii hii elimu ya juu juu ile ya "reproduction" , kuna haja waende ndani zaidi Watoto wajue maana kukutana kimwili, pamoja na athari za kufanya hivyo kabla ya kufikia umri muafaka n.k.
....nawasilisha...