Hivi bado hatuoni haja ya kuwafundisha Watoto wetu elimu ya uzazi/viungo vyao vya uzazi tangu utotoni?

Hivi bado hatuoni haja ya kuwafundisha Watoto wetu elimu ya uzazi/viungo vyao vya uzazi tangu utotoni?

May Day

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2018
Posts
6,311
Reaction score
9,027
Ni muda mrefu sasa nimekuwa najiuliza hili swali, haswa ninapokuwa na kijana Wangu mdogo wa kiume mwenye umri wa miaka kumi.

Kuna wakati tupo sebuleni tunasikiliza Redio au TV, na habari inayosikika ni kuhusu Mtoto aliyelawitiwa, Binti aliyepewa mimba, Mwanamke aliyebakwa n.k.

Hapa huwa linanijia swali hili haswa ninapomuangalia Mtoto na kumuona akifuatilia habari ile kwa makini:- "hivi Mwanangu hapa hahitaji ufafanuzi wowote kutoka kwa Mzazi kwa anachosikiliza? ina maana ameelewa kila kitu kwa 100%?

Je, ni nini kinamwambia kwamba hili si jambo sahihi kujadili na Mzazi? mbona mengine anakuwa huru kuuliza?..kwa mfano taarifa ikiwa ni ndege imeanguka atauliza maswali mengi huku akisisitiza kuwa yeye hatopanda tena Ndege maishani mwake n.k.

Au huwa anasubiri aende shuleni wakutane na "fundi" wao aliyesikiliza na awape ufafanuzi wa kila kitu wanachotaka kuelewa kuhusu maswala hayo? kama ndivyo, hii ni sawa? kwa nini sisi Wazazi au Waalimu tusikae hapo kati kati na kutimiza wajibu wetu kuwafafanulia?

Huwa najaribu kukumbuka nilipokuwa na umri kama wake (miaka 9-10), na mambo niliyokuwa nakutana nayo/nayasikia nikiwa shuleni...nikiwa darasa la nne tu (nakumbuka hivi kwa sababu nilihama shule ya kwanza nilipoingia tu darasa la tano) kulikuwa na baadhi Wanafunzi wenzetu walikuwa ni "watukutu" na mafundi wa kuongea matusi.

Namkumbuka Jamaa mmoja aliitwa Moses, lakini almaarufu tulikuwa tunamuita "Mozee"...huyu kulikuwa na tuhuma kuwa ni mtumiaji wa sigara bwege...huyu jamaa aliwahi kutusimulia alivyokuwa "anawapiga" (nimetumia tafsida) Ng'ombe akiwa machungani...iwe alisema ukweli au la...ila bado stori zile si zilikuwa ni nzito kwa masikio yale machanga?.

Pia namkumbuka jamaa mmoja aliyekuwa fundi sana wa kutumia matusi kwenye ule mchezo wa ushindani wa matani (natumai wengi wanaufahamu huu mchezo) yaani Wanafunzi wawili mnarushiana matani kwa kushindana na mwishoni apatikane mshindi.

Moja ya matani maarufu ya huyu Jamaa alikuwa anamwambia mwenzake "ulikuwa unapigwa...ukataka kuvunja upepo...ukamwambia jamaa..chomoa nij..be...jamaa akakwambia jamb..a humohumo" basi Wasikilizaji tuliowazunguka tunacheka sana.

Tusi lake lingine maarufu ni "Mama yako anamenya ndizi k.. inapuliza moto"..basi Washangiliaji tena tunacheeeka...hayo ni baadhi ninayoyakumbuka.

Baadae nikiwa nimeshahamia shule nyingine nilikutana na kina James, Walter n.k...nakumbuka kulikuwa na Mwalimu Mjamzito, alikuja darasani amechoka...James akatuambia Mwanamke mimba ikishafikia ukubwa ule hawezi tena kuvaa ch..pi" sasa alisikia wapi hayo sijui.

Siku moja tukiwa Darasani, dawati la mbele alikuwa ameketi Dada mmoja anaitwa Saida, alikuwa ameketi kwenye ukingo wa dawati akiwa ameiachia miguu panu, basi nakumbuka James alinionyesha akaninong'oneza na kuniambia "hapo k..ya Saida imekaa hivi" huku akinionyesha mfano kwa kutumia mdomo wake....kipindi hicho mimi hata sijui hizo k zinafananaje, kwa hiyo hubaki nakodoa macho tu na kumuamini "Mwalimu" wangu James....Dada wa kazi naye home alikuwa haachi upenyo..akiingia bafuni anaziba kila upenyo akijua hivi vidume humu ndani ni vitundu vitapiga chabo.

Lingine kali ni pale tulipoingia darasa la sita, akahamia binti mmoja anaitwa Khadija, alikua mapepe, mjanja mjanja sana, na pia kalikuwa ni karembo kwelikweli...na kalikuwa kana mambo mambo ya kikubwa kuliko umri wake....na ilisemekana kwamba huko shule aliyokuwa walimshindwa wakamfukuza...mimi nilikuwa mpole mpole na muoga muoga sana..nakumbuka siku moja aliniambia "we Katoto unataka?, kama unataka kesho uje na wembe mpya...unasikia?" hata sikumuelewa ana maana gani, nilibaki namshangaa tu..na kumuona huyu Dada ni mchokozi. Ni miaka mingi sasa lakini alichoniambia na sura yake ile bado haijanitoka kichwani, ingawa najua nikikutana naye leo naweza nisimtambue.

Kiufupi yapo mengi sana, ila hayo ni baadhi ya yale ninayoyakumbuka takribani miaka zaidi ya 25 baadae...na nitakuwa Mjinga kufikiri kwamba Mtoto wa sasa hivi hakutani na mambo kama haya niliyokutana nayo mimi...bila kujali kama nyumbani kwao anapitia misingi yote ya malezi...na Wazazi wangu walikuwa wanajitahidi kwa kweli.

SWALI:- ni Wazazi wangapi wanadhani Watoto wao hupitia "shule" za aina hiyo wawapo mbali nao?

SWALI:- je, Wazazi wangu walijua kama nakutana na haya huko shuleni? jibu ni hapana kwa sababu nilikuwa sithubutu kuyasema haya mbele ya Baba au Mama.

Na kama walidhani kila kitu kipo shwari, walikuwa ni Wazazi bora? je ni sahihi kwa Wazazi kukaa pembeni na kuacha dunia iwafunze Watoto wao?.

SWALI:-Vipi kuhusu hawa Wanafunzi watukutu kama kina James na wengine, nao Wazazi wao wanajua Watoto wao wako hivyo, kwamba ni Waalimu wa Wenzao huko shuleni? inawezekana wala hawajui lolote.

SWALI:-Na hivi nao huwa wanajifunza/sikia wapi hayo yote na kuja kuelezea wenzao Shuleni?

SWALI:-Ni nani atakuwa Mwalimu muafaka wa Watoto, Mwanafunzi mwenzake, Mwalimu, Mzazi, Shangazi, Mjomba n.k.

Au tuendelee kuishi kwa kujidanganya tu kwamba kila kitu ni shwari.

Maoni yangu ni kuwa ipo haja Jamii tutafute njia rasmi ya kuwafundisha Watoto wetu , mapema wajue tofauti ya Mwanamke na Mwanaume..wajue kazi ya uume na uke n.k.

Siizungumzii hii elimu ya juu juu ile ya "reproduction" , kuna haja waende ndani zaidi Watoto wajue maana kukutana kimwili, pamoja na athari za kufanya hivyo kabla ya kufikia umri muafaka n.k.

....nawasilisha...
 
Write your reply...wafundishe bana mnatupa changamoto nipo kitaa natoka na kimwanafunzi hakajui vzur mizunguko yake hii ni hatari inabid muwape elimu
 
Write your reply...wafundishe bana mnatupa changamoto nipo kitaa natoka na kimwanafunzi hakajui vzur mizunguko yake hii ni hatari inabid muwape elimu
Wewe kesi yako ni tofauti, unatembea na Mwanafunzi sheria itafuata mkondo.

Mimi nazungumzia ishu ya kudhani Watoto wetu hawajui chochote ili hali wanajua kwa njia zisizo rasmi, ambazo mimi naona ni hatari na zinaweza kuwapoteza zaidi.
 
Write your reply...wafundishe bana mnatupa changamoto nipo kitaa natoka na kimwanafunzi hakajui vzur mizunguko yake hii ni hatari inabid muwape elimu
Aisee...hapo subiri na wako aje aliwe kama unavyojidai sasa hivi unakula ka mwanafunzi.

Pia wakumfundisha kujua mzunguko wake ni wewe unayefanya huo uharibifu kwa maana wewe ndio unayejua mnafanya huo mchezo
 
Fafanua kidogo, tupe maelezo.
Sasa unataka wafundishwe kwamba huyu ni jinsia Ke na huyu Me, wakikutana inatokea hivi au vile.

Mbona itakuwa hatari Mzee baba..akili zao bado changa..
 
Sasa unataka wafundishwe kwamba huyu ni jinsia Ke na huyu Me, wakikutana inatokea hivi au vile.

Mbona itakuwa hatari Mzee baba..akili zao bado changa..
Naona hujasoma andiko vizuri Mkuu.
 
Wafundishe Mzee,tena waonyeshe kabisa.
Acha kupanua goli huo ni wajibu wako,akianza tu kuongea mfundishe. Ila kwa shuleni bado kwanza mishahara haijatosha kufundisha hayo.
 
Wafundishe Mzee,tena waonyeshe kabisa.
Acha kupanua goli huo ni wajibu wako,akianza tu kuongea mfundishe. Ila kwa shuleni bado kwanza mishahara haijatosha kufundisha hayo.
Duuh, na waonyeshwe kabisa?

Ila nadhani Mtu baki atafundisha kwa uhuru zaidi kuliko Mzazi.
 
Ni ukichaa kudhani Watoto wetu wadogo hawajui chochote kuhusu ngono.
 
Js tell them its wrong kwa umri wao kujihusisha ama kuhusishwa...wapige kelele ama waseme kwako wakihisi hawako salama

wafundishe jema lipi baya lipi...kwa dalili

mfano
kauli za kutukana ni baya
Mtu kukushika sehemu za siri unazofunika na chupi ama kifuani kwa wa kike ni baya

na urafiki ili waseme upate mbinu na ujitahidi kuwasahihisha
 
Maelekezo mazuri sana.

Ila hoja yangu kuu hapa ni kuona kama sisi Wazazi tujipime kama bado wote tunao huo uwezo wa kuwaelekeza watoto vile inavyopasa?

Hofu yangu ni kwamba kuna Wazazi wengi sana wasiojali na hivyo wanaopoteza watabaki kuwa ni wale Watoto...na ndio hoja yangu hapa.

Je hakuna haja kuwa na Mtaala maalum wa namna nzuri ya kuelekeza Watoto, kwa mfano kuwe na Waalimu na vipindi maalumu kwa kutoa elimu hiyo kwa uwazi ila kitaalamu zaidi..maana nyie mkifichaficha kina Khadija kule wao chepeo wanaita chepeo.
 
Malezi bana ni kitu kigumu na si rahisi ku-control tabia ya mtoto utakavyo. Unaweza ukasema watoto wote wafundishwe hayo unayoyasema ndiyo bado ukapata majanga mengi zaidi, watoto wengi waka-fail zaidi tena kwa vitendo. Yaani ndiyo ukajikuta unakuwa na hao watoto wajanja wajanja wengi zaidi. Kila wa kitoka kujifunza nao wanaendelea kuwa waalimu wanawafundisha zaidi wenzao kwa vitendo.

Ndiyo maana labda kwa sasa tuuchukuwe tu ushauri mzuri uliotolewa kwenye comment #13 na mjumbe LadyRed.
 
Kuna haja ya kuwepo na somo la 'stadi za maisha' nahisi

tulikua nalo kipindi cha dini shuleni sekondari

nadhani ni muhimu sanaa mnoo
Iwe avenue to teach generally accepted and unaccepted cultural morals
 
Malezi bana ni kitu kigumu na si rahisi ku-control tabia ya mtoto utakavyo. Unaweza ukasema watoto wote wafundishwe hayo unayoyasema ndiyo bado ukapata majanga mengi zaidi, watoto wengi waka-fail zaidi tena kwa vitendo. Yaani ndiyo ukajikuta unakuwa na hao watoto wajanja wajanja wengi zaidi. Kila wa kitoka kujifunza nao wanaendelea kuwa waalimu wanawafundisha zaidi wenzao kwa vitendo.

Ndiyo maana labda kwa sasa tuuchukuwe tu ushauri mzuri uliotolewa kwenye comment #13 na mjumbe LadyRed.
Ahsante..Ni kweli ni ngumu..sio siri huwezi ukahakiki maisha ya mwanao 100% ila tujaribu

ndo mana kuna haja ya kumsoma mtoto na kujaribu kucontrol mazingira flani
Aina ya shule,marafiki zake ,mazingira ya nyumbani
Lakini kubwa zaidi ni kumpa elimu ya kupambanua vitu yeye kama yeye ajue jema na baya

hapo elimu ya dini madrasa na makanisani inasaidia pia
Kumpa mtoto vitabu vizuri vya kusoma awe anapata 'exposure' zaidi ya situations na maisha nk
 
Yes well said LadyRed. Thanks.
 
Back
Top Bottom