chiembe
JF-Expert Member
- May 16, 2015
- 16,859
- 28,112
Ningekuwa Mimi ndio Bashungwa, ningepiga kambi Mkoa wa Mara na kuusafisha, nikiwa na kikosi kazi maalum.
Rais hajaridhishwa na yote yanayotokea Mkoa wa Mara, na hatusikii Waziri akitema cheche, amebaki Ally Happy tu alifanya ziara, na kwenye ziara bado anasema ataandika barua sijui TAMISEMI, sijui wapi, nilitarajia Bashungwa angekuwa pale amepiga kambi akichekecha mmoja baada ya mwingine.
Hii wizara kwa staili yake, itamuondoa mapema katika nafasi yake, ni wizara kubwa, pana, inayohitaji maamuzi ya haraka. Huko ndiko Kuna wananchi, TAMISEMI ikiboronga, basi serikali nzima inakuwa na mzigo wa kujitetea kwa umma, wapi makatibu wakuu TAMISEMI? Mmekaa tu Dodoma? Rais akipita mahali na akawa na maswali, tuma timu ikayafanyie kazi.
Bashungwa ajitathmini kama anatosha, kama hachukui hatua kwa Kasi ya mwewe, nashauri SSH aanze kumuondoa yeye, wengine watafata, hiyo ni sampo moja tu ya Mkoa wa Mara, nilitarajia Waziri asambaze moto mkali kwa halmashauri zote nchi nzima, Rais kampa sampo tu kwamba hasimamii vizuri TAMISEMI, Bashungwa, wake up! Kengele za tahadhari zimeanza kulia, maandishi yanasomeka ukutani ...mene mene tekeli na pelesi