Hivi Bashungwa "anatosha" pale TAMISEMI? Pamoja na Rais kutoridhishwa na mambo ya Mkoa wa Mara, bado hajachukua hatua

Ningekuwa Mimi ndio Bashungwa, ningepiga kambi Mkoa wa Mara na kuusafisha, nikiwa na kikosi kazi maalum.

Rais hajaridhishwa na yote yanayotokea Mkoa wa Mara, na hatusikii Waziri akitema cheche, amebaki Ally Happy tu alifanya ziara, na kwenye ziara bado anasema ataandika barua sijui TAMISEMI, sijui wapi, nilitarajia Bashungwa angekuwa pale amepiga kambi akichekecha mmoja baada ya mwingine.

Hii wizara kwa staili yake, itamuondoa mapema katika nafasi yake, ni wizara kubwa, pana, inayohitaji maamuzi ya haraka. Huko ndiko Kuna wananchi, TAMISEMI ikiboronga, basi serikali nzima inakuwa na mzigo wa kujitetea kwa umma, wapi makatibu wakuu TAMISEMI? Mmekaa tu Dodoma? Rais akipita mahali na akawa na maswali, tuma timu ikayafanyie kazi.

Bashungwa ajitathmini kama anatosha, kama hachukui hatua kwa Kasi ya mwewe, nashauri SSH aanze kumuondoa yeye, wengine watafata, hiyo ni sampo moja tu ya Mkoa wa Mara, nilitarajia Waziri asambaze moto mkali kwa halmashauri zote nchi nzima, Rais kampa sampo tu kwamba hasimamii vizuri TAMISEMI, Bashungwa, wake up! Kengele za tahadhari zimeanza kulia, maandishi yanasomeka ukutani ...mene mene tekeli na pelesi
Mhe Bashungwa yuko vizuri sana na kufuatia maagizo ya Rais tayari hatua zimechukuliwa. Mlizoea kila hatua inayochukuliwa inatangazwa lkn si lzm.
RC, RAS wanaendelea kufanya kazi kwa umakini mkubwa.
 
Ccm ni chaka la majizi wa mali za umma na ipo siku mtajutia haya madhambi yenu
 
Katika watu ambao sijui wanapewaje uwaziri ni bashungwa kwanza
1 hajui hata kuongea
2. Kila siku yeye wimbo ni tutaajiri walimu 7000 na hajui upungufu ni kiasi gan
3. Hana haiba ya uongozi cijui alipitaje hata kwenye chama nahisi anapesa
4. Ndo atakayemkwamisha rais maana huyu jamaa labda ana chale za hataree
 
Mhe Bashungwa yuko vizuri sana na kufuatia maagizo ya Rais tayari hatua zimechukuliwa. Mlizoea kila hatua inayochukuliwa inatangazwa lkn si lzm.
RC, RAS wanaendelea kufanya kazi kwa umakini mkubwa.
Umakini mkubwa huo ni upi kingali Halmashauri fulani wakaguzi wameenda kukagua mafaili ya taarifa za ujenzi wilayani pasina kufika mashuleni ambako ujenzi haujakamilika wamesepa kwa kukagua makaratasi majengo yameanza na kuchakaa hata miezi miwili haijaisha.
Bongo bahati mbaya
 
Nakubaliana na wewe. Huyu Waziri kijana ni vizuri ajiongeze ktk utendaji kazi. Ana bahati ya kupewa vyeo lkn impact yake haionekani. Tunaona mathalan ktk wizara ya habari mambo aliyoshindwa kufanya kwa mwaka mzima Nape kayatekeleza ktk muda mfupi - kufungua magazeti, channel za fta, n.k. Hatujui kwa mfano kama Bashungwa ana uwezo wa kuboresha vituo vya mabasi na masoko ktk miji kote nchini. I doubt
Kuna kitu watanzania bado hamwelewi. Hiyo wizara saivi ni muungano wa wizara mbili. Hayo unayoyasema kwenye wizara yake hayakuwepo.
 
Wakaguzi hawa wanakagua makaratasi bila kufika field kujionea uhalisia. Wengine wakifika field hawana kuonana na wanakamati za ujenzi. Wanaonana na wakuu wa shule au wa vituo bila kuziona kamati. Kisha wanasepa. Nyie nyie nyie achani pesa zipigwe. Kama timu maalumu ndo zimekaa kichovu namna hii
 
Acheni wivu mr bash anafanya kazi vyema
 
Back
Top Bottom