maroon7
JF-Expert Member
- Nov 3, 2010
- 11,311
- 15,640
Hivi karibuni kumekua na mijadala mingi ya kuhusu hii mikopo ya mitandaoni na wahanga wakizidi kuongezeka licha ya unyanyasaji na udhalilishaji unaofanywa na watoa huduma ambao hivi karibuni BOT wameukemea baada ya wabunge nao kuona ndugu na jamaa zao nao wamekua wahanga baada ya wao wenyewe kuanza kupokea jumbe za kuwataka wawalipie ndugu zao mikopo waliyoshindwa kuilipa.
Kwanza kwenye hili naomba nidiriki kusema kuwa BOT hawajawatendea haki wananchi kwa kutokua proactive hadi baada ya wabunge kulalamika ndio wakatoa muongozo.
Je ni kweli hawakua wanafahamu hili sakata wakati wao ndio regulators? Pili inachoonekana BOT hawakujiongeza zaidi hata kujaribu kutafuta chimbuko la hili maana mikopo inayotolewa na hizi online applications ni midogomidogo lakini ajabu ni kuwa imekua hailipiki na kupelekea udhalilishaji kwa wateja.
Hawa watoa huduma aisee riba zao (wanadanganya kwa kuita service fee) ni kubwa mno na ni kwa muda mfupi sana wa wiki moja. Kitu ambacho ni ajabu sana mkopo wa 1 week timeline kuwa na riba ya zaidi ya karibu asilimia 40.
Hii hali inapelekea mkopaji kujikuta anashindwa kumudu na kulazimika kukopa kwenye app nyingine na nyingine na nyingine ili aweze kulipa mkopo wa awali kwenye App iliyotangulia.
Mwisho wa siku ndio hayo tunayoyaona ya watu kutangazwa kuwa matapeli wa mitandaoni kisa kuchelewa au kushindwa kulipa na kuanza kuundiwa ma group ya WhatsApp ili watu/ndugu wachange.
Na Apps zinaongezeka kila siku sababu wameona ni shamba la bibi hakuna anaejali wala kuuliza.
Hivi hii hali inatokeaje kama hawa watoa huduma wamesajiliwa ? Kwanini hawadhibitiwi?
Kwanini hamuwapi muongozo wa riba na timeline kama taasisi nyingine mkiwa ninyi ndio regulators?
Najua kwa wenye akili ndogo watasema mtu hajalazimishwa kukopa, ila mjue kwenye taasisi nyeti kama ya fedha ukifanyika uzembe wa namna hii ni dalili mbaya sana kwa mamlaka zetu unless kama nao wanafaidika na hii hujuma.
Kutoa muongozo tu bila kudili na chanzo ni uzembe unaoweza kugharimu maisha ya familia nyingi.
Kama huna mtu wa karibu aliewahi pata changamoto ya hawa wakopeshaji unaweza usielewe.
Ziboresheni ziwe na nia kweli ya kumkwamua mtu kuliko ilivyo sasa ambapo zinania ya kuwatia watu umasikini ndani ya muda mfupi.
Soma Pia: BoT yakataza rasmi kampuni za mikopo mitandaoni kuchukua mawasiliano ya wateja ili kuwadhalilisha. Yatoa mwongozo mpya!
Ajabu nyingine ni TCRA kuwa kimya mpaka sasa kuhusu njia mbalimbali za udhalilishaji na ukiukwaji wa faragha inayotumiwa na hawa watoa huduma ku-blackmail wateja walipe madeni ambayo hayalipiki ikiwemo kushare taarifa za wakopaji kwa watu wasiohusika mradi tu wapo kwenye phonebook ya mkopaji. Hivi ni mamlaka zetu zimelala au?
Otherwise fungia hawa wahindi/ wachina/ Wakenya wanaomiliki hizi Apps kwa sababu hawajawahi kuwa na nia ya kweli kumsaidia mtu wa chini zaidi ya kumkatili kwa kupora alichonacho kwa njia hii.