Hivi BOT mmeidhinishaje hizi riba za hawa mikopo mitandaoni?

maroon7

JF-Expert Member
Joined
Nov 3, 2010
Posts
11,311
Reaction score
15,640
Hivi karibuni kumekua na mijadala mingi ya kuhusu hii mikopo ya mitandaoni na wahanga wakizidi kuongezeka licha ya unyanyasaji na udhalilishaji unaofanywa na watoa huduma ambao hivi karibuni BOT wameukemea baada ya wabunge nao kuona ndugu na jamaa zao nao wamekua wahanga baada ya wao wenyewe kuanza kupokea jumbe za kuwataka wawalipie ndugu zao mikopo waliyoshindwa kuilipa.

Kwanza kwenye hili naomba nidiriki kusema kuwa BOT hawajawatendea haki wananchi kwa kutokua proactive hadi baada ya wabunge kulalamika ndio wakatoa muongozo.

Je ni kweli hawakua wanafahamu hili sakata wakati wao ndio regulators? Pili inachoonekana BOT hawakujiongeza zaidi hata kujaribu kutafuta chimbuko la hili maana mikopo inayotolewa na hizi online applications ni midogomidogo lakini ajabu ni kuwa imekua hailipiki na kupelekea udhalilishaji kwa wateja.

Hawa watoa huduma aisee riba zao (wanadanganya kwa kuita service fee) ni kubwa mno na ni kwa muda mfupi sana wa wiki moja. Kitu ambacho ni ajabu sana mkopo wa 1 week timeline kuwa na riba ya zaidi ya karibu asilimia 40.

Hii hali inapelekea mkopaji kujikuta anashindwa kumudu na kulazimika kukopa kwenye app nyingine na nyingine na nyingine ili aweze kulipa mkopo wa awali kwenye App iliyotangulia.

Mwisho wa siku ndio hayo tunayoyaona ya watu kutangazwa kuwa matapeli wa mitandaoni kisa kuchelewa au kushindwa kulipa na kuanza kuundiwa ma group ya WhatsApp ili watu/ndugu wachange.
Na Apps zinaongezeka kila siku sababu wameona ni shamba la bibi hakuna anaejali wala kuuliza.

Hivi hii hali inatokeaje kama hawa watoa huduma wamesajiliwa ? Kwanini hawadhibitiwi?

Kwanini hamuwapi muongozo wa riba na timeline kama taasisi nyingine mkiwa ninyi ndio regulators?

Najua kwa wenye akili ndogo watasema mtu hajalazimishwa kukopa, ila mjue kwenye taasisi nyeti kama ya fedha ukifanyika uzembe wa namna hii ni dalili mbaya sana kwa mamlaka zetu unless kama nao wanafaidika na hii hujuma.

Kutoa muongozo tu bila kudili na chanzo ni uzembe unaoweza kugharimu maisha ya familia nyingi.

Kama huna mtu wa karibu aliewahi pata changamoto ya hawa wakopeshaji unaweza usielewe.

Ziboresheni ziwe na nia kweli ya kumkwamua mtu kuliko ilivyo sasa ambapo zinania ya kuwatia watu umasikini ndani ya muda mfupi.

Soma Pia: BoT yakataza rasmi kampuni za mikopo mitandaoni kuchukua mawasiliano ya wateja ili kuwadhalilisha. Yatoa mwongozo mpya!

Ajabu nyingine ni TCRA kuwa kimya mpaka sasa kuhusu njia mbalimbali za udhalilishaji na ukiukwaji wa faragha inayotumiwa na hawa watoa huduma ku-blackmail wateja walipe madeni ambayo hayalipiki ikiwemo kushare taarifa za wakopaji kwa watu wasiohusika mradi tu wapo kwenye phonebook ya mkopaji. Hivi ni mamlaka zetu zimelala au?

Otherwise fungia hawa wahindi/ wachina/ Wakenya wanaomiliki hizi Apps kwa sababu hawajawahi kuwa na nia ya kweli kumsaidia mtu wa chini zaidi ya kumkatili kwa kupora alichonacho kwa njia hii.
 
Wabunge si ndio serikali. Ipo hivi Serikali ya Tanzania ipo kwaajili ya viongozi wa ccm au waliopo kwenye mfumo wao. aipo kwa ajili yako wewe mwananchi. Kwaiyo imewagusa ndugu wa wabunge ndio maana wamekemea iyo Mambo.
 
Kwakweli inashangaza kwa taasisi nyeti kama BOT kufanya kazi kisiasa. Kimsingi ni kama hawajui kinachoendelea huku chini zaidi ya kusubiri kuskia nini kimetokea kwa wanasiasa
 
Nipe code huwa naiona ona tu huko mitandaoni.
Shukuru Mungu imekupita pembeni. Ni kilio huko, watu hadi wameshindwa kupeleka watoto shule sababu ya hiyo. Wanaku-backmail, Meseji zinatumwa kwa majirani,bodaboda wako, wakwe,mashemeji, michepuko, maboss zako, wateja wako, waalimu wa watoto wako, school bus driver, house girl wako na kila uliemsave kwenye simu yako. Kisha wanakuundia group la WhatsApp uchangiwe. Na TCRA wapo maana wanasema kabisa wameshakureport TCRA wanamkataba nao. Ukichelewa kulipa (kimsingi unakuta hata tarehe inayoonekana kwenye App haijafika) ila wakikupigia simu matusi utakayopewa unazeeka kabla ya muda na kupata kisukari na presha ndani ya miezi miwili tu. Wanakutukania wazazi,watoto, hadi kuku zako Wajaribu mkuu. Wiki mbili tu unakonda hadi watu wanakusahau
 
CHADEMA chukueni pointi hapa CCM wameshindwa kusaidia wananchi na mikopo hii ya kausha damu
 
Wana riba kubwa sana hawa wasenge, nilikopa 50,000 nikabetia bahati na nilishinda nikalipa 69,800 siku ya sita tu wakaanza kudai.
 
Mafedhuli sana hawa, siku moja nimetingwa nilidowload app moja ya mikopo nikakopa 50000, ajabu wakanipa 48000 kuja kucheki riba na kiasi ninachotakiwa kurejesha nikakuta natakiwa nirejeshe 80000 ndani ya mwezi mmoja aagh nilijilaumu sana ikabidi nilipe hapo hapo tena kwa kurudisha kia48 chao na nikasongesha mkopo ili nisisumbuane nao maana haukuwa msaada bali uuaji😔😔
 
Wana riba kubwa sana hawa wasenge, nilikopa 50,000 nikabetia bahati na nilishinda nikalipa 69,800 siku ya sita tu wakaanza kudai.
Sasa usiombe ukope kwenye App nyingi. Bora uliishia hapo tu maana dunia ungeiona chungu
 
Kuna jamaa ana kawaida ya kukopa halafu halipi. Alikopaga Branch nikamwambia hao wana riba ndogo ila jitahidi ukipata hela tu warejeshee chao kwa wakati, akawacheleweshea.

Sasa hivi hawataki kumkopesha wanamrusha siku 7 kila wakati.
Tena utafikiri wameambizana kajaza app kibao za mikopo zote wanamkatalia tu.

Anadaiwa songesha, mgodi, nivushe plus, M-PAWA na hapa ana shida ya hela ila binadamu wanakataa kumkopesha na mitandao inakataa.
 
BOT ni hopeless kabisa. Wao ni kutoa matamko na miongozi tu kisha wanakaa kimya.
BOT ni mpaka liwapate wanasiasa ndio wanaibuka. Walipaswa kufungia kwa muda hizi taasisi ili zitakazokidhi vigezo zifunguliwe. Sasa wao wametoa muongozo tu halafu wamepotea na hakuna kilichobadilika. Leo kampuni ya Oya wamedunda mdaiwa wao hadi wameua
 
Kulipa deni ni jukumu la mkopaji.
Watu wote mnatakiwa kujua kwamba kujulikana kwamba unadaiwa sio jambo baya ingawa baadhi ya wakopeshaji kwakuwa ubunifu wao ni mdogo wanadhani kwamba kutangaza Kwa watu kwamba wamekukopesha ni jambo la faida kwao.

Kamwe usiogope kujulikana kwamba unadaiwa ingawa kama kwenye maelekezo ya mkopo wako hakipo kipengele kinachomruhusu mkopeshaji kutangaza Kwa jamii Yako kuhusu mkopo wako basi unaweza kwenda kuwashtaki mahakamani au unaweza kuamua kuacha kulipa ili Hiyo jamii au watu wako wa karibu waliombiwa kuwa unadaiwa wakulipie deni.

Pia kuhusu kiwango Cha riba ikiwa umekopa lipa kwanza mkopo wako Kisha nenda mahakamani kafungue mashitaka ili aliyekukopesha atoe sababu za kiuchumi zilizomfanya atoe mkopo Kwa riba ya 45% Kwa muda wa wiki Moja au mbili.
Shida za ghafla zinaweza kumfanya mtu aombe mkopo bila kuzingatia masharti lakini hii sababu haimnyimi haki za kisheria mkopaji.

Kuhusu masharti ya kulipa nimeangalia baadhi ya kampuni Huwa wanaeleza kwamba kutakuwa na Ada ya kuchelewa kulipa mkopo lakini kitu kizuri Kwa wakopaji ni kwamba shariti hili halijaonesha muda wa kuchelewa ni siku ngapi au ni miaka mingapi kwahyo sharti Hilo linakufanya mkopaji uwe huru kulipa hata baada ya miaka kadhaa muhimu ujue tu kwamba kadri unavyozidi kuchelewa kulipa ndivyo deni lako linavyozidi kukua ingawa utakuwa na haki za kumshitaki mkopeshaji endapo makadilio ya riba yatakuwa nje na vigezo na masharti ya kiuchumi.

Usione haibu kudaiwa wewe daiwa tu ikikubidi ingawa vigezo vizingatiwe.
Mfano Mimi nadaiwa na LOAN BOARD (Bodi ya mikopo ya elimu ya juu) walinikopesha nikasoma nikamaliza nawashukuru sana Tena mno ila mbaya zaidi hadi saizi Bado Sina uwezo wa kulipa na mkataba unasema deni lataanza kusoma miaka miwili baada ya kuhitimu na kutakuwa na nyongeza ya Ada ya kuchelewa kulipa hivyo hadi Sasa nikipiga hesabu naona nakaribia kuwa na deni la zaidi ya Milioni 15 ila naamini nitalipa tu na Kwa hakika naomba mungu nisife hadi nilipe madeni ya watu.

MWISHO: NAOMBA KAMA KUNA MTU ANAWEZA KUNIKOPESHA MILIONI 5 ZA KITANZANIA ANISAIDIE ILI KUSUDI NIWEZE KUFANYA BIASHARA AMBAYO ITANISAIDIA KUENDESHA FAMILIA NA KUJIJENGA KIUCHUMI.
 
Kudaiwa sio kosa ni kweli. Kosa ni ulaghai unaokuwemo umejificha ndani ya mkopo, na njia inayotumiwa na wadaiwa kama inavunja sheria au kukiuka taratibu. Na hapo ndio tumewalaumu BOT wao kama regulators
 
Hivi karibuni kumekua na mijadala mingi ya kuhusu hii mikopo ya mitandaoni na wahanga wakizidi kuongezeka licha ya unyanyasaji na udhalilishaji unaofanywa na watoa huduma ambao hivi karibuni BOT wameukemea baada ya wabunge nao kuona ndugu na jamaa zao nao wamekua wahanga baada ya wao wenyewe kuanza kupokea jumbe za kuwataka wawalipie ndugu zao mikopo waliyoshindwa kuilipa.

Kwanza kwenye hili naomba nidiriki kusema kuwa BOT hawajawatendea haki wananchi kwa kutokua proactive hadi baada ya wabunge kulalamika ndio wakatoa muongozo.

Je ni kweli hawakua wanafahamu hili sakata wakati wao ndio regulators? Pili inachoonekana BOT hawakujiongeza zaidi hata kujaribu kutafuta chimbuko la hili maana mikopo inayotolewa na hizi online applications ni midogomidogo lakini ajabu ni kuwa imekua hailipiki na kupelekea udhalilishaji kwa wateja.

Hawa watoa huduma aisee riba zao (wanadanganya kwa kuita service fee) ni kubwa mno na ni kwa muda mfupi sana wa wiki moja. Kitu ambacho ni ajabu sana mkopo wa 1 week timeline kuwa na riba ya zaidi ya karibu asilimia 40.

Hii hali inapelekea mkopaji kujikuta anashindwa kumudu na kulazimika kukopa kwenye app nyingine na nyingine na nyingine ili aweze kulipa mkopo wa awali kwenye App iliyotangulia.

Mwisho wa siku ndio hayo tunayoyaona ya watu kutangazwa kuwa matapeli wa mitandaoni kisa kuchelewa au kushindwa kulipa na kuanza kuundiwa ma group ya WhatsApp ili watu/ndugu wachange.
Na Apps zinaongezeka kila siku sababu wameona ni shamba la bibi hakuna anaejali wala kuuliza.

Hivi hii hali inatokeaje kama hawa watoa huduma wamesajiliwa ? Kwanini hawadhibitiwi?

Kwanini hamuwapi muongozo wa riba na timeline kama taasisi nyingine mkiwa ninyi ndio regulators?

Najua kwa wenye akili ndogo watasema mtu hajalazimishwa kukopa, ila mjue kwenye taasisi nyeti kama ya fedha ukifanyika uzembe wa namna hii ni dalili mbaya sana kwa mamlaka zetu unless kama nao wanafaidika na hii hujuma.

Kutoa muongozo tu bila kudili na chanzo ni uzembe unaoweza kugharimu maisha ya familia nyingi.

Kama huna mtu wa karibu aliewahi pata changamoto ya hawa wakopeshaji unaweza usielewe.

Ziboresheni ziwe na nia kweli ya kumkwamua mtu kuliko ilivyo sasa ambapo zinania ya kuwatia watu umasikini ndani ya muda mfupi.

Soma Pia: BoT yakataza rasmi kampuni za mikopo mitandaoni kuchukua mawasiliano ya wateja ili kuwadhalilisha. Yatoa mwongozo mpya!

Ajabu nyingine ni TCRA kuwa kimya mpaka sasa kuhusu njia mbalimbali za udhalilishaji na ukiukwaji wa faragha inayotumiwa na hawa watoa huduma ku-blackmail wateja walipe madeni ambayo hayalipiki ikiwemo kushare taarifa za wakopaji kwa watu wasiohusika mradi tu wapo kwenye phonebook ya mkopaji. Hivi ni mamlaka zetu zimelala au?

Otherwise fungia hawa wahindi/ wachina/ Wakenya wanaomiliki hizi Apps kwa sababu hawajawahi kuwa na nia ya kweli kumsaidia mtu wa chini zaidi ya kumkatili kwa kupora alichonacho kwa njia hii.
Miongozo na sheria za bot zipo, nina wasiwasi kuna conflict of interest utakuta kigogo wa bot ndio kampuni yakebau anakula percent unategemea nini, haiwezekani hawa watu wanasumbua wananchi namna hii na bot wapo kimya
 
Back
Top Bottom