Hivi Deusdedith Soka ndio amezimwa kama alivyozimwa Ben Saanane?

Hivi Deusdedith Soka ndio amezimwa kama alivyozimwa Ben Saanane?

TUPUNGUZE UJUAJI NA KUTUMIKA KAMA LESO
Mzee Kibao alikua na ujuaji gani na alikua anatumika kama leso?

Vipi lele tukio la Tarimo ni la kisiasa kwamba alikua anatumika na Ujuaji anao?


Mkuu kwa jinsi hali alivyo kwa sasa ukinyatia demu mmoja na mkubwa unawezapotezwa/pesa zako ulizotafuta kwa Jasho wakiamua kikupugia hesabu ili wazichukue unawezapotezwa vilevile

Haya matukio hayana fomula
 
Ipo siku kitasambazwa kituo kizima kilichohusika hapo labda akili itawakaa waache waendelee na hii tabia
 
Wametumbukizwa kwenye pipa la Asidi kibari Mkemia Mkuu
Inasikitisha sana ,madogo hawana effect yeyote ,yaani kutoa maoni tu wanaenda kumalizwa.

Wanashindwa kuelewa kwamba hauwezi kuzuia watu kutoa maoni ,wamemuua Ben lakini wameibuka wengine ,hauwezi kumaliza watoa maoni/wanaharakati ,Utafanya Ubabe miaka 10 yako inaisha unakaa Benchi na kujutia midhambi yako ,Awamu ya Jiwe imemuua ben ,imempiga lissu risasi ,kiko wapi sasa? wamepata faida gani?

Yaani unaua mtu kisa madaraka? non sense.
 
Cha kujiuliza ni kwamba soka,Ben saanane walikua wamebeba Siri Gani kubwa Hadi wapotee bila KESI ya mahakamani!!!?

Yaani kwanini washughulikiwe kimafia vile bila Sheria kuchukua mkondo wake!!?he kosa lao ni la kihaini!!?au kuhatarisha usalama was jamhuri!!?

Haya ni baadhi ya maswali ya wanajamhuri huwa tunajiuliza pia!

Soka ndiyo imeisha hiyo.

Kwani Tanzania unahitaji kufanya kosa kubwa kumalizwa?

Huhitaji kosa kubwa.

Wanakufanya mfano tu kwa wengine ili watu wasijione wako huru sana.

Mkijifikiria mko huru tu. Mnakumbushwa.

"Not to that extent" alishasema Magufuli.

Au mmesahau?
 
Historia inaonyesha wanasiasa wa upinzani wenye ushawishi mkubwa Alfonsi Mawazo, mgombea ubunge jimbo la Busanda, Daniel John katibu wa Chadema kata ya Ananasifu, Anthony Lyimo alikuwa mgombea udiwani kata Nganga Mfumuni wote hawa walitekwa waliteswa na kuumizwa na kutupwa, wengine waliokotwa wamekufa na wengine wakiokotwa wakiwa hai bila kujitambua.
 
Soka ndiyo imeisha hiyo.

Kwani Tanzania unahitaji kufanya kosa kubwa kumalizwa?

Huhitaji kosa kubwa.

Wanakufanya mfano tu kwa wengine iki watu wasijione wako huru sana.

Mkijifikiria mko huru tu. Mnakumbushwa.

"Not to that extent" alishasema Magufuli.

Au mmesahau?
Na vile habari nilivyoenda viral mpaka DW na BBC wakareport nikajua hawarudi hawa, mtu pekee nilikuwa naimani wanaweza muacha ni yule aliyechoma picha ila hawa wa Chadema, niliamini hawarudi. Chaula angeweza kupigwa biti na asiongee ila ni tofauti kwa hawa wengine.
 
huku kwetu kuna washikaji wetu wanne walienda dar kununua mizigo ya biashara,...hawajarudi mpaka leo ni zaidi ya miezi saba mpaka sasa,.. police nchi nzima inataarifa,....kubarikiwa kwa haya matukio na serikali, kumetengeneza madhingira ya hofu kwa jamii pia imekuwa ni fursa kwa watu wenye nia ovu
 
Bado yupo hai,wanaendelea kumtesa sijui hatma yake.
 
huku kwetu kuna washikaji wetu wanne walienda dar kununua mizigo ya biashara,...hawajarudi mpaka leo ni zaidi ya miezi saba mpaka sasa,.. police nchi nzima inataarifa,....kubarikiwa kwa haya matukio na serikali, kumetengeneza madhingira ya hofu kwa jamii pia imekuwa ni fursa kwa watu wenye nia ovu
Serikali ikiamua inawadaka hata kesho. Something is wrong
 
Back
Top Bottom