Hahahah
, CAF sio mahakama, ni chombo cha usimamizi na uendeshaji wa soka Afrika, bogus. Kwa muhibu wa kanuni zao, Ukiwapelekea tuhuma zozote, haijalishi zimeletwa na nani au dhidi ya nani, watachunguza kwa mbinu zao kujua ukweli au uongo na kutoa uamuzi kwa kadri ya kanuni!
Kama ulikuwa hujui CAF ni taasisi yenye idara nyingi ndani yake
Moja kati ya hizo idara imetengwa kwa ajili ya kushughulikia kesi za wanachama wake.
CAF hawachunguzi madai, CAF wanachunguza ushahidi ulioletwa na mleta madai.
Ngoja nikueleweshe.
Kwenye scenario ya jana na ile controversial ya goli la Azizi Ki, mkasema mpeleke madai CAF kuwa mmedhulumiwa maana yake ushahidi ambao mtaambatana nao ni ile clip ya kuonesha mpira ulivyovuka goal line.
Kwa maana hiyo CAF wao watajizatiti katika ushahidi wenu kuangalia ni kweli ule mpira ulivuka au haukuvuka.
Ikithibitika kuwa mpira ulivuka basi adhabu itatolewa kwa refa bila kuathiri matokeo aliyoyaamua.
Kwa maana hiyo ni kuwa mtakuwa mmefanya tu kulipiza kisasi kwa refa ili aadhibiwe lakini haiwezi kubadilisha maamuzi yake aliyoyafanya kwa kukataa goli.
Lakini ukasema utumie clip hiyo kama madai ya kusema ni match fixed, basi safari hii, clip peke yake haitatosha kuwa ushahidi, utaombwa ushahidi mwingine kusapoti hoja yako.
Kwasababu mpaka hapo ushahidi wako wa mwanzo hauoneshi match fixed bali unaonesha uzembe wa refa. Kwa hiyo uzembe wa refa unathibitishaje moja kwa moja kuwa ni conspiracy ya kupanga matokeo?
Ukiombwa uthibitisho utaweza kuutoa?
Match fixed huwa zinafanywa kwa protocol kali na za kisiri watu wanafiriki hafi kutumia dark web wasionekane na ndio maana maamuzi ya kuamua kuwa hii ni match fixed hayatolewi kwa kuangalia matukio yaliyotokea uwanjani.