Baina yetu Watanzania kuna asilimja kubwa saana ya watu wenye tabia za uchawa, achana na hawa wanaowasema kina manara, yule baba levo, wale kina h baba, mwijaku, zile ndio tabia halisi za watz wengi.
Mfano mdogo(level ya chini) subiri upate vifanikio kidogo, utaona wanaanza kukuposti, hata wale ambao hamna uwana huo, au walikuwa hata hampostiani, watanza kukuposti, subiri wagundue tarehe yako ya kuzaliwa, oohh, ishi miaka mingi damu yangj, sijui kimeenda kimerudi. Ama unakuta mtu kamposti mtu anammwagia sifa kedekede lakini kwenye life la mawaida hawa hawana ukaribu huo.
Hivyo usishangae hilo, kwa level ya juu huko, marehemu alikuja kustimyuleti hii tabia, sababu alikuwa anapenda saana sifa, sisemi huko nyuma haikuwepo la hasha, ila kwa mwendazake ilishika kasi.