residentura
JF-Expert Member
- Mar 1, 2017
- 8,146
- 11,434
Ni kakikundi kameandaliwa na kanalipwa kwa kazi hiyo.Habari wana JF,
Binafsi nna kama Miezi 6 au zaidi sijakutana na mwanachi anaeishangilia na kuisifia hii serikali ya Awamu ya Sita.
Ingawa kuna ongezeko la mishahara na Ajira lakini bado kila sehemu malalamiko ikiwa ina Maana hii serikali bado inahitajika kufanya kitu cha ziada kwa Wananchi wake.
Swali: Hivi hawa raia walijaa mitandaoni kusifia sana wanatoka wapi mbona mitaani hatuwaoni? Au ndio wako maofisini wanatafuta teuzi?
Pia kwenye kila alipo Mh. Rais Samia, kunakuwepo kikundi cha vijana kinaitwa "vijana wa hamasa".
Kazi yao ni kusifia.