Hivi haya mabanda ya Machinga kila kona Dar wameshindwa kuyadhibiti?

Mkubwa kasema baadhi ya mitaa ifungwe kabisa Watu wapige hela Sasa wachumi wa jiji wameona Bora wasifunge Ila tupite hivyohivyo kwa kubanana Ila Watu wapare ridhiki.
 
Ndugu ni nchi nzima....Ni aibu...miji yote ni michafu....

Arusha ni balaa tupu...ni aibu....
Aibu kwa Nani ? Unayemuonea aibu ni Nani? Wakati huko dunia ya kwanza Homeless/ machokoraa wamejaa kibao hawajui hata watakula Nini watalala wapi Sasa aibu unamuonea Nani? Acha Watu wapige hela.
 
Kwa kweli taswira ya jiji imeharibika sana. Sokoine drive mbele ya Mahakama ya Rufaa, Kempiski hotel mpaka feri kuna mabanda machafu sana. Watu wanapanga mafungu ya bamia na matembele kwenye njia ya waenda kwa miguu.

Hata kama ni haki ya Wajasiriamali kufanya biashara. Si busara kuchafua kila mahali kwa mabanda na hasa mji mkongwe(maeneo ya posta) bora kuwe na sehemu yao maalum.

Mama lishe pia wanapika kwa kuni kila sehemu mjini kati. Lazima kuwe na udhibiti.
 
Exactly na ndio tunachosema kama wanaruhusiwa mabanda basi isiwe kila mahali natena yawe same standard kama vile vibanda vya askari vya Asas hata ukiweka kinapendeza. Au waruhusiwe maeneo baadhi kama buguruni,manzese etc othewise wajenge masoko
 
Yaani mkuu inatia kinyaa aisee ukiangalia miundombinu inavyopendeza mfano pale mahakama ya rufaa hadi feri lakini mauchafu ya yale mabanda mpaka mtu unajiuliza kama hawa viongozi wanatembeaga hata nchi za jirani tu kujifunza.
 
Mkuu unaakili ndogo sana....na umekurupuka hata hujaelewa mada...na inaonekana ww hata nchi ya jiran yoyote hujaenda....hebu vuka boda kidogo afu utajua watu wanavyofanya vitu kwa utaratibu. Usiwe na akili za bashite
 
Kwakweli hili linasikitisha sana jiji lote limekuwa slum sababu ya wamachinga, wafanyabiashara wanaolipa kodi kariakoo wanashindwa fanya biashara sababu ya hao wachuuzi. Mbaya zaidi kiuchumi hawana impact sababu sio wazalishaji ni ongezeko la wachuuzi tu ambao ni middle men, kodi hawalipi.

Kwakweli sekali inapaswa kulisimamia hili haiwezekani kuwa na mji hauna utaratibu yaani ukifika posta pale jengo la benjamin mkapa, jengo la mabilion watu wanakaanga mihogo barazani vibanda kila upande. Hivi watalii watakuja kweli kutalii slum city?
 

Basi serikali itumie hayo maeneo ya chini ya hayo madaraja Ubungo na Tazara kuweka maeneo sahihi ya matumizi ya wananchi wa kawaida, inawezekana sana!



 
Sasa jiwe mwenyewe ndio anataka iwe hivyo,tutafanyaje?
 
Mitano tenaa
 
Miji yote imekuwa takatakaa. Kila mahali mabanda kama kibera slums.

Aiseee ni pachafuuu! Miji inakuwa kama ya machokoraa!
Siasa hovyo sana kisa vitambulisho vya machinga wanaweka mabanda kila mahali aisee miji inachukiza kwakweli wawadhibiti wawe na maeneo baadhi tu ndo waruhusiwe kama manzese etc
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…