Hivi haya matukio ya namna hii hupangwa na CCM, serikali au wavaa kaunda suit?


 
UKISIKIA nyimbo walizotunga na Hata UKISIKIA maneno ya uvccm inaonyesha NI MPANGO yao. MFANO ule wimbo WA wapinzani wakifa watawatupa mto Kagera.
Fikiria mtu hafiki bungeni na haonekani lkn bunge wala haliulizii apo na polisi hawaoneshi kumsaka. It means wanajua alipo. Na ni nini kinachoendelea.
 
Kwa hili la the boy, sitakuamini. Liko hoti achana na zile rongo rongo za zamani
Je kwa makosa unayosikia amefanya hadi kufunga kanisa umeshasikia juhudi zozote za polisi au serikali kumtafuta ili kumfikisha mbele ya vyombo vya sheria?

Je umeshasikia bunge likifuatilia ili kujua alipo mbunge mwenzao tena wa chama chao?

Kwa mtu maarufu wa aina ya mtumishi anaweza kujichimbia sehemu more than 2 days bila serikali kujua mahali apo kweli?

Kwa mtazamo wangu ni kwamba serikali, polisi na bunge wote wanajua alipo. Sema hawana muda wa kushughulika kumuulizia au kumsaka kwa sababu wanajua jamaa yupo kwenye mipango yao kabambe, hivyo wakijifanya kumsaka eti wamkamate ule mpango wao wa kwenda chama fulan utavurugika rasmi.
 
Hongera kwa mtazamo wako japo ni mtazamo wa upotoshaji. Ni hivi, Lowassa hakuandalowa na ccm kwenda upinzani, bali aliutaka sana urais kipitia ccm na akakatwa. Akatumia hela zake kununua nafasi ya kugombea kupitia chama chenye nguvu, nacho ikawa ni cdm. Na kwakuwa Mbowe alikuwa ni mwenyekiti akachota hela.

Ni upotoshaji wa makusudi kuwa Lowassa alirudi ccm baada ya kukamilisha kazi yake. Ukweli ni kuwa wanaccm wengi wanamiliki utajiri walioupata kwa wizi kwenye fedha za umma. Ifahamike Magufuli alikuwa rais mwenye kupenda kukomoa, na alipombana Lowassa kwenye utajiri wake wa wizi, akawa hana ujanja zaidi ya kujisalimisha, na Magufuli alifanya hivyo akitegemea wafuasi wa upinzani wamkubali kwa kudhani wapinzani huwa wanahama na kiongozi.

ACT ni chama kilichonzishwa na kina JK akiwa na kundi lake lan kina Membe, Mwigulu nk, na lengo ilikuwa ni kupata chama cha kupambana na cdm. Membe alikuwa muhanga wa siasa za Magufuli, na ni mmoja wa viongozin wa ccm waliokuwa wanamchukilia Magufuli kama mshamba na mpenda sifa, wakawa wanavutana akahama ccm na kuhamia ACT ambacho ni chama walichokianzisha wenyewe. Ila maalim Seif hakuwa tayari kuchezewa kama mchezo wa Lowasa, ndio maana Zito akakubali Membe agombee urais, lakini Maalim Seif akaamuunga mkono Lisu na sio Membe. Zito hakuwa na namna maana Membe ndio walikuwa wenye chama.

Kwenye huo ujio wa wanaccm walikuwepo akina Nyalandu ila cdm wakamstukia, lakini Mbowe alikuwa anamtaka zaidi Nyalandu na sio Lisi ila alizidiwa nguvu na wanachama wa cdm, ambao hawakitaka upuuzi wa Lowassa ujirudie. Huyo Gwajima ni kweli anaweza kwenda upinzani, lakini hakuna mfuasi wa upinzani mjinga tena. Labda aende Chauma ambayo imeshafahamika ni project ccm.
 
Hizo mbinu za kizamani hakuna wa kuokotwa tena, watu tumebaki tunawachora tu.
 
Usisahau Nyerere alisema upinzani wa kweli utatoka ndani ya CCM. Hakutaja lini na kwa namna gani. CCM ndiko maovu yote yanakoendelea sasa na kukaliwa kimya.

Sasa usishangae wadau wakijiuliza kama Gwajima aliyeongoka ndiye au wamtarajie mwingine?

Usisumbuke bure. Wengi walitarajiwa wakapita hivi hivi. Hata huyu kama siye naye atapita hivii 🫱🏽… Lakini amin, nakwambia, aliyesemwa lazima atokee na huenda tayari yu miongoni mwetu.
 
We pimbi unajua nini?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…