Habari zenu wanaJF wenzangu
Leo naomba nianze na matukio matatu yalioanza kutokea katika chaguzi kuu tatu za Tanzania, ili kujua na kufahamu kuwa ni kina nani ambao huwa wanapanga mipango hii kila inapofikia karibu na uchaguzi mkuu wa Tanzania.
Mwaka 2015, karibu na uchaguzi mkuu, vyama vya upinzani viliungana (UKAWA), kwa lengo la kumsimamisha mgombea mmoja wa uraisi mwenye nguvu, na mvuto wa pekee aje apambane na mgombea yoyote atakaeteuliwa na CCM kugombea nafasi hiyo ya uraisi. Kati ya watu ambao walikuwa wanapewa nafasi kubwa ya kupita katika mchujo wa UKAWA ili aje apambane na mgombea wa CCM bara ni Dr Slaa. CCM japo sijui ni chama au serikali walipoona hivyo wakaja na plan B ya kutengeneza mazingira ya kutoelewana ndani ya chama kati ya Kikwete na Lowasa ili akatwe, ajifanye kuhama chama, na aende akalazimishe kugombea UKAWA. Kweli mission ile ikafanikiwa Lowasa akaenda kugombea UKAWA, kupitia tume ambayo bila shaka alijua kabisa atashindwa ili kukamilisha mission waliyopanga.
Baada ya uchaguzi kuisha Lowasa akazuga zuga baadae akashindwa kuendelea kuzuga akarudi kule kule kwa wenzake.
Mwaka 2020, karibu na uchaguzi zengwe lingine likaanzishwa tena kati ya Magufuli na Membe. Lengo lilikuwa Membe akimbilie katika chama kikuu cha upinzani ambacho kilikuwa tishio kwa mamlaka. Lakini Membe baada ya kuona chama hicho kikuu cha upinzani kimemwita mgombea wao kutoka Ubelgiji, jamaa akawa hana namna zaidi ya kwenda kuzuga ACT Wazalendo. Huko napo alishindwa kumalizia kampeni akaingia mitini na baadae kurudi tena kwa wenzake kama alivyofanya Lowasa.
Mwaka huu naona yale yale yanajirudia. Mtumishi wa Mungu ameona matukio haya yamenza kufanyika toka 2017 enzi za kina Lisu kupigwa risasi kakaa kimya, Ben saa8 kupotea kakaa kimya, mzee kibao kuuwawa kakaa kimya. Sasa umefika muda wa vyama kuanza kutafuta wagombea mbali mbali wa nafasi za uraisi, vikiwemo vyama vya upinzani ndo na yeye anaanza kuibuka kama walivyoibuka kina Lowasa na Membe, ili afukuzwe chamani na kwenda kule ambapo atatumwa akagombee kuharibu mipango ya chama hicho.
Sikatai kwamba ana hoja na aliongea mambo ya msingi. Lakini kwanini hakuyazungumza au kukemea haya mapema toka kipindi kile cha Lisu kupigwa risasi, Ben saa8 kupotea? Au alikuwa hayupo nchini ili tusimlaumu?
Hii ni sawa sawa na watu ambao walikuwa wanapinga raisi Magufuli asifute mikataba mibovu ya madini, kwa madai kwamba wakati mikataba hiyo inasainiwa yeye alikuwa nchini hivyo ilitakiwa aipinge wakati ule ule. Sasa na mtumishi wa Mungu kwanini hakupaza sauti kipindi kile kile?
Yani mtoto amegongwa na nyoka badala ya kuwahi hospital kuzuia madhara ya sumu kupanda, wewe unasubiri sumu ishafika kichwani eti ndo unajifanya kumuwahisha hospital kuokoa maisha yake [emoji1787][emoji1787][emoji1787].
Kwa sasa naamini mtumishi yupo sehem anapewa elimu, na maelekezo ya kwenda kufanya huko apohamia, kusema eti mtumishi yupo chimbo ambalo serikali hailijui ni upuuzi wa kiwango cha ubongo wa sisimizi. Mamlaka inajua alipo, lakn pia inajua yupo huko alipo kwanini.
Huku kungine ni mwendo wa No reform No election. So ACT Wazalendo kuweni makini. Msije kushangaa mtumishi baada ya uchaguzi mkuu anarudi chamani na kuteuliwa na raisi katika zile nafasi za wabunge wa kuteuliwa na raisi kisha kuendelea na maisha kama kawa.
Katika Afrika kila mbinu ya kucheza na akili za watu huwa inawezekana kabisa.