Hivi haya matukio ya namna hii hupangwa na CCM, serikali au wavaa kaunda suit?

Hahaha nlitegemea labda ungeweka facts either ya sauti, video au maandishi yoyote ya Lowasa akisema mwenyewe haya uliyoandika ili tuamini kuwa nimepotisha. Lakini kumbe na wewe umekuja na maandishi yako tu matupu uliyoyafikiria wewe mwenyewe kichwani kwako. Sasa hapo nikisema wewe au sisi wote tumepotosha kwa kuandika vitu bila uthibitisho wa muhusika mwenyewe nitakosea?

Lowasa huyu ambae baada ya uchaguzi kuisha, watu walitaka kuingia barabarani kupinga matokeo ya uchaguzi yeye akawambia eti watulie, waachane na siasa za uanaharakati badala yake wafanye siasa za kikondoo, hivyo kumpa Magufuli uhuru wa kutawala bila zengwe wala heka heka zozote za watu kudai haki zao za kuibiwa. Unakosaje kuonganisha dot kuwa huyo mtu alitumwa?

Ukweli ni kwamba Lowasa alionekana kuwa angekuwa kikwazo kikubwa sana cha ushindi wa CCM kama angesimama na Dr Slaa chini ya UKAWA katika uchaguzi mkuu. Zile kashfa kubwa za ufisadi alizokuwa anaandamwa nazo zingefanya ashindwe hata kusimama mwenyewe jukwaani kujitetea. Na kina Kikwete wangetumia muda mwingi kumsafisha yeye badala ya kunadi wagombea wengine wa ubunge, udiwani nk.

Hivyo suluhisho ikawa ni kumwambia hali halisi tu kwamba ashachafuka sana, hawezi kusafishika wala kuuzika kirahisi kwa muda mfupi vile. Cha kufanya ni kupewa hela, ili akalete kashkash ya kugombea uraisi huko upande wa pili, ambapo kama angepitishwa na CCM kugombea basi wao (UKAWA) walikuwa wameshajipanga kumchana chana vibaya kutokana na zile kashfa zake za ufisadi. Hivyo mambo yakaenda kama walivyoyapanga wenyewe na Mbowe akavuta mpunga.
Hii ya Magufuli ilikuwa mipango ya kumfanya arudi kule alipotoka kwa kisingizio cha kumuogopa Magufuli kumbe geresha tu. Ni kitu gani cha maana ambacho unaweza kusema Magufuli alikitaifisha kutoka kwake hadi ikapelekea yeye kuogopa na kurudi CCM?
Nafikiri umesahau kuwa vyama vyote vimeanzishwa na wana CCM ikiwemo Chadema, CUF, NCCR nk. Na vyote vilianzishwa kwa mpango maalum ndio maana viongozi wote wa vyama hivyo ukiwafuatilia kwa makini unakuja kugundua mwishoni kwamba wanatumika au kutumiwa na viongozi wa serikali ya CCM. Ukimuangalia Mrema wa 95 katika uchaguzi mkuu jinsi alivyokuwa na nguvu kisiasa, na tishio kubwa kwa CCM sidhani kama kuna siku watu wangekuja kugundua kwamba jamaa alikuwa anafanya kazi na serikali ya CCM kuihadaa dunia na watanzania kwa ujumla.

Hivyo hivyo kwa kina Marando, Lipumba, Mbatia, Cheyo, Mbowe nk. Hivyo vyama vyote vilianzishwa na CCM au wana CCM, sema ndani ya vyama hivyo wanaweza kupatikana baadhi ya watu wakawa wapinzani wa kweli japo ni mfumo pekee ndo huwafahamu watu hao kwa vile hawakuingia nao makubaliano yoyote.
Hii ya Nyalandu kukosa kosa kugombea Chadema 2020, naikumbuka sana mkuu.
 
Wengi waliambatanisha kauli hii ya Nyerere na ujio wa Lowasa upinzani mwaka 2015. Baada ya pale sidhani tena kwa sasa hivi kutokea mtu wa aina hiyo. Huyu mtumishi yeye kapangwa tu aje na mbinu zile zile za kina Lowasa, Membe, Nyalandu nk.

Wajanja washashtukia ndomaana hili tukio wanaliangalia tu waone mwisho wake.
 
Mkuu umeandika sana lakini mimi naona hii si habari kubwa ya kukusumbua kisasi hicho. Gwajima anaweza kuwa tapeli au diversion. Haijalishi sana. Akili kichwani. Watu wanatapeliwa kila siku. CHA MAANA angalau sauti moja imesikika kuhusu ushenzi unaozidi kukua na kukomaa nchini.

Hata tawala mbovu kama za Mobutu, Idi Amin, Nguema hazikufikia kiwango cha IMPUNITY katika utekelezaji wa unyama kwa wapinzani na wakosoaji kama tulipofikia. Mamlaka zikiulizwa zinatoa majibu ya kijeuri sana na kufunga mjadala kwa nguvu.

Watu wanachukuliwa na Polisi Mahakamani asubuhi wananchi wakiona na media zikirekodi, wanaenda kuteswa, kisha kutelekezwa machakani. Polisi wakiulizwa wanajibu kwa kejeli. Mtu anachukuliwa na polisi/usalama ndani ya basi mchana kweupe. Licha ya taarifa kuenea wakati huohuo kesho yake mwili wake unapatikana eneo la jirani umesulubiwa vilivyo na macho kutobolewa! Mamlaka zinatoa maneno ya kejeli.

Kwa kadiri siku zinavyosonga mamlaka zimeamua kutelekeza vyombo na taasisi za kisheria. Mahakama zinazidi kupoteza maana. Ni njia za mkato tu. Kuteka, kunyanyasa, kutesa, kudhalilisha, kuua na kupoteza. Due process can go to hell! Tutaishia wapi?

Acha Gwajima atiririke. Kama ni mbabaishaji au mropokaji IS NOT A BIG DEAL. Angalau ujumbe anaotoa utaanza kutikisa uozo unaotaka kuangamiza taifa. Hakuna mwingine anayesema. Kama ndio utawala mbovu unazidi kufitinika, so well be it. Integrity ya Gwajima tutasumbuka nayo miaka ijayo; sio leo. Kwa sasa atajijua na Mungu wake.
 
Inasikitisha sana
 
Mkuu? Awali ya yote naomba nikuombe radhi kwanza kwa kutokusoma mada yako ambayo kwa mujibu wa baadhi ya maoni ya wachangiaji inaonyesha wazi umeongea vitu vya msingi Sana, hivyo kwa heshima na tahadhima natanguliza heshima zangu nyingi kwako na kongole kem kemu Bila kujari udini, kabila, rangi au jinsia ya kwamba tutashirikiana vzr kutoa maoni na kuunga Hoja! Ahsante sana
 
Nakumbusha kuwa Shekhe Ponda kajiunga rasmi ACT- Wazalendo, naye ni miongoni mwa Wazee wa kuchezesha antena kila nyakati za uchaguzi.

Kiongozi Mkuu huyo wa ACT, kasema nafasi iko wazi kwa wapenda haki na demokrasia kujiunga huko.

Uwezekano wa Gwaji kujikita ACT upo wazi.
 
Agenda Setting Theory umeiva vizuri
 
Unabisha nini unajua mfumo ni mpana sana kiufupi kuna mfumo wa ndani na kuna mfumo wa nje na yote ni mifumo
Vijana wa 2010 huyo, hata kubalehe anyone anaonekana bado hajabalehe. So ni vigumu sana kuyajua mambo ya mifumo. Kikubwa anachofahamu ni kupelekwa kwa Gwajima kumpigia makofi na kumshangilia tu kila J2.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…