Hivi haya matukio ya namna hii hupangwa na CCM, serikali au wavaa kaunda suit?

Ya ni kweli nakubaliana na wewe mkuu. Ndomaana kama ulisoma thread yote huko juu kuna sema nimesema nakubaliana na kile alichoongea Gwajima kuhusu utekaji na mauaji. Lkn sasa haya mambo yalianza muda mrefu sana toka 2017 Enzi za Lisu kupigwa risasi, Ben saa8 kupotea nk. Kama kweli alikuwa na nia ya dhati ya kutetea matendo hayo kwanini hakuwahi kujitokeza hata siku moja huko nyuma kutetea unyama huu?

Alikuwa haoni kinachoendelea au alikuwa hayupo nchini?

Inamaana waliokuwa wanatekwa na kuuwawa miaka yote hawakuwa na umuhimu kwake mpaka akae kimya miaka yote hiyo?

Au pengine safari hii kuna ndugu yake, au mtoto wake ametekwa ndomaana amejifanya kujitokeza na kulikemea swala hili? Ni nini siri au sababu ya yeye kukaa kimya muda wote hadi aibuke leo?
 
Shukran sana mkuu kwa kila aya na hoja uliyoandika hapa. Ubarikiwe wewe na uzao wako wote ndugu yangu 🙏🙏
 
Sheikh Ponda ni miongoni mwao mkuu ndomaana watu hawakushangazwa kwa yeye kuenda huko.
 
Gwajima alijieleza kwanini alikaa kimya muda wote huo.
Hatuwezi kupigia mstari katika point zako kuwa ni sahihi uliyoyaongea kwa 100%!
Hapo inaweza kuwa plani zake binafsi pia.
Kwa wanasiasa lolote laweza kuwa sahihi.
 
Gwajima alijieleza kwanini alikaa kimya muda wote huo.
Sishangai yeye kukimbilia kujitetea vile mapema, maana alikuwa ashajipanga lkn kwa mtu mwenye akili timamu kamwe hauwezi kukubaliana na utetezi wake. Toka 2017 ujitokeze leo 2025? Yani kama ulizaa mtoto miaka hiyo sasa ivi anakaribia kubalehe.
Hatuwezi kupigia mstari katika point zako kuwa ni sahihi uliyoyaongea kwa 100%!
Hapo inaweza kuwa plani zake binafsi pia.
Kwa wanasiasa lolote laweza kuwa sahihi.
Hapa nakubaliana na wewe mkuu.
 
Wavaa kaunda suit,

Wakihakikisha Gwajima anakuwa Mkuu 2025,

Itakuwa mission Bora kuwahi kutokea tangu nchi kupata uhuru.
Sidhani kama wanaweza kuwa na mpango huo. Kinachofanyika hapa ni kuhamisha magoli kuhusu kesi ya Lisu, badala ya watu kutumia muda mwingi kujadili, na kuongelea kesi ya Lisu, watumie muda mwingi kujadili, na kuongelea ishu ya Gwajima. Ukiweka mawazo yako huru utaligundua hili.

Hata zile kelele za watu kuwazungumzia wanaharakati wa Kenya nk zimepungua kwa kiasi kikubwa. Kila mtu anatega sikio kusikia Gwajima atakuja na neno gani, na raisi au viongozi wa chama watamjibu na neno gani.

Kingine wanaangalia chama ambacho wataweza kumpachika huko, ili akawavuruge na uchaguzi ufanyike kama walivyopanga wao.
 
Wewe ni mjinga unayefikiria kijinga sana. Unafikiria mtoto aliyezaliwa miaka ya 1990 atakuwa anawaza huo ujinga unaowaza wewe?
 
Nakuelewa mkuu. I appreciate your thinking.

Kinachonisikitisha ni kuwa nchi imefikia hatua ya ovyo sana na safari yakuelekea "jehanam" inazidi kushika kasi. Hii yote ni kwa sababu watu wengi wenye uelewa na nafasi kubwa ndani ya dola wamegubikwa na giza la tamaa (greed), hofu na ujinga kiasi cha kuwa SPINELESS and GUTLESS.

Hakuna mwenye akili ya kuona mbele tena. Wanafumbia macho giza nene la maafa linalozidi kujongea karibu. Kwao, the country can go to hell as long as I survive and continue receiving my daily trickle of crumbs!

Inapofikia hatua hiyo, hata sauti ya mwendawazimu inakuwa na maana sana kuliko jigonga gonga za wenye akili. Kufikia hapo chambuzi za kisomi (analysis) na busara za "wenye akili" zinakuwa anasa isiyokuwa na maana yoyote kwa nchi na kwa wananchi. Haitashangaza mtu kama Gwajima akipata mileage kubwa mitaani.

Hivi hivi, kwa mfano, Marekani haikustahili kuongozwa na mtu erratic kama Donald Trump ambaye anajulikana kama mbabaishaji na tapeli katika biashara aliyorithishwa na baba yake. Mtu anayetaka kupindua na kuvuruga mfumo mzima ulioifikisha Marekani kuwa taifa kubwa na lenye nguvu na ushawishi mkubwa (wa heri au wa shari) kuliko yote duniani.

Hii yote ni sababu watu wenye uelewa mkubwa (intellectuals) wa mifumo ya nchi walijisahau wakaacha kushughulikia mambo ya msingi na kuanza kuendekeza ujinga mwingi kiasi cha kuwakatisha tamaa wananchi wa kawaida. Wananchi hao wakaona ni bora safari hii wamjaribu huyu "mwendawazimu" ambaye angalau kauli zake wanazielewa na wanachukuana nazo - hata kama yeye na maneno yake yanatia shaka!
 
Mbona inafahamika gwajima ni mwanamikakati! Hapa anaweza kuzuga ana ugomvi na serikali ya chama chake mradi tu wananchi waone ni kweli! Wamelifunga kanisa lake halafu wanatoa offer akate rufaa walifungue. Hapa kuna kundi la vyama 14 vinasema vitaungana vipate mgombea mmoja wa kushindana na ccm! Who know? Huyo mgombea anaweza kuwa gwajima machachari wa kuchangamsha uchaguzi. Maana lissu mpinzani wa kweli yuko ndani na haijulikani watamuachia lini, yule ndiye angeleta vibe kubwa kwenye uchaguzi ila kawekwa ndani hadi muda huu. Kaibuka gwajima na hoja za kina lissu kwa sasa trending ni yeye na mama anampa makavu kila akipata jukwa gwajima anakula za uso. Huenda ukawa ni mkakati wa kucheza na akili za wananchi, hebu tusubiri muda tutaona picha kamili!
 
Swadakta mkuu kwa kutoa hoja yenye mashiko. Kifupi umeandika maneno ya msingi sana.
 
Mtumishi huko alipo akisoma hizi comment zetu anachukia sana kuona tumemgundua mapema kabla ya kuianza mission yake.
 
Nadhani mleta uzi ni kama amekariri maisha na historia

Kuna kitu kinaitwa “ Wakati wa Bwana” 😁
Hahaha brother G na mabosi wake wametumia mbinu za kijinga sana. Ukute kafichwa kwa Amos Makala alaf watu wanaacha kujadili kesi ya Lisu na wanaharakati wa Kenya. Wanabaki kujadili alipojificha mtumishi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…