Hivi haya matukio ya namna hii hupangwa na CCM, serikali au wavaa kaunda suit?

Gwajima aliuanbia umma kumwombea Lissu na kuhudhuria Mahakamani,

Sasa amezima nn na anaongelea utekaji ambao Kila kukicha CDM wanaiongelea majukwaani.

Tujadili hoja ya utekaji, habari za ambition za Gwajima mwachie mwenyewe kama zipo.
 
Gwajima aliuanbia umma kumwombea Lissu na kuhudhuria Mahakamani,

Sasa amezima nn na anaongelea utekaji ambao Kila kukicha CDM wanaiongelea majukwaani.

Tujadili hoja ya utekaji, habari za ambition za Gwajima mwachie mwenyewe kama zipo.
Kama ulisoma vizuri huko juu toka mwanzo wa thread hii nilionesha kukubaliana nae kwenye swala la utekaji na mauji. Lakini mkakati huu wa kutetea mbona hakuufanya kipindi kile Lissu anapigwa risasi?
Mbona hakuufanya kipindi kile Ben saa8 na wengine walipotekwa na kupotea?

Unajua toka 2017 hadi 2020 ni watu wangapi walikuwa wamepotea, je kwanini hakuona umuhimu wa kutetea kipindi chote kile, na watu wote wale waliopotea?

Kuanzia 2021 hadi mwaka huu mwez wa kwanza unajua ni watu wangapi waliopotea, kutekwa na kuuwawa?

Je alikuwa wapi kukemea miaka yote hiyo hadi asubiri kipindi hiki ambacho kuna heka heka za uchaguzi, Lisu kukamatwa nk ndo ajitokeze?

Obvious anaweza kumzungumzia Lisu katika mission zake ili kuwafunga macho watu aina yako, lkn moyoni akawa na mipango yake, au target zake nyingine kabisa ambazo amepewa kuzifanya.
 
1.Aliyemdokeza Lisu kuahirisha kwenda Dodoma sababu alipata tetesi juu ya kushambuliwa kwake wamjua?

2.Na Utekaji wa watu kituo Cha clouds Fm na vita yake na kijana yule ilikuwa juu ya nn kama SI utekaji na matumizi ya nguvu?

Yote hayo hapo juu wayajua na unajichomoa betri.

Kiufupi huna hoja!
 
Unataka kutuaminisha kwamba Mtumishi naye atakuja na kauli ya "Narudi nyumbani?"
Kwa sababu kwenye nchi zetu hizi masikini ni ngumu sana kuwa mpambanaji, mtafuta hela kama gwajima halafu uakishi na kufanikiwa nje ya chama tawala. Ni ngumu mno unless upoteze vingi sana au Chama tawala kishindwe. atarudi tu hata kama sasa yuko serious. Watu wanamlaumu mbowe hata yeye kafinywa sana aisee...

Baada ya uchaguzi vijana wengi walio CDM watanunuliwa ama wataenda kutumikia chama chao halali (ya kina silinde, nassari nk) trend inaonesha hivyo.
 
1.Aliyemdokeza Lisu kuahirisha kwenda Dodoma sababu alipata tetesi juu ya kushambuliwa kwake wamjua?
Hizi ni siasa tu. Umdokeze mtu alaf akishambuliwa ushindwe kukemea na kuongelea swala la kushambuliwa kwake!
2.Na Utekaji wa watu kituo Cha clouds Fm na vita yake na kijana yule ilikuwa juu ya nn kama SI utekaji na matumizi ya nguvu?
Ndo maana nasema hii unayoongelea hapa ni siasa. Jamaa alijifanya kuongea kwa sababu kijana tayari alikuwa ashamhusisha ktk ile vita yake ya madawa ya kulevya. Na ndomaana na yeye akawa anapambana na kijana. Je baada ya lile zogo la madawa kuisha uliona tena anaendelea kupambana na kijana hadi leo?
Yote hayo hapo juu wayajua na unajichomoa betri.

Kiufupi huna hoja!
Wewe hili swala umeliweka kiutetezi zaidi badala ya kiuhalisia, ndomaana unapinga bila kujua unachokipinga.
 
Unajitekenya na kucheka mwenyewe! Kwamba Lowassa ulikuwa mpango wa system? Kwa taarifa yako Lowassa angetendewa haki ndo angekuwa wa awamu ya 5 na aliitikisa CCM vilivyo. Kwa Gwajima tujadili kwanza hoja zake, je watu hawatekwi? Hawapotei? Hawalawitiwi? Kwanini mkemea maovu aonekane mkosaji na wakosaji halisi wakumbatiwe!?
 
Kuna wajinga hauwambii kitu. Wao wanaamini kuwa mchungaji ni mkombozi wa watanzania.
Jibuni hoja za mchungaji kwanza, naona nguvu kubwa mmeelekeza kumshambulia yeye binafsi! Kwanza ni mwana CCM mwenzenu na M-NEC so aliyozungumza kayatoa jikoni kabisa, jibuni hoja
 
Ni bora yeye ameweza kuongea hata kwa kuchelewa. Maccm wwnzio nani kathubutu kuongea na anaona kabisa wananchi wanarekwa, kubakwa na kuuawa!? Si bora huyo aliyethubutu kufungua mdomo?
 
Mkuu thread yangu au hoja yangu ulitakiwa uijibu mchana ukiwa haujalewa. Saa hizi hata hatuwezi kuelewana, maana umeuliza maswali ambayo nimeshayajibu hapo hapo kwenye thread. So bora nikuache kwanza ulale pombe ziishe kichwani na hasira ipungue akilini.

Usiku mwema.
 
Yetu macho
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…