Hivi hii tabia kwamba ukila dagaa au bamia wewe ni maskini inatoka wapi?

Hivi hii tabia kwamba ukila dagaa au bamia wewe ni maskini inatoka wapi?

Hii tabia inakuja kwa sababu kule ulaya fresh food kama matunda na mboga zinaliwa na matajiri wakati masikini wanakula junk food kama mikate na madude the likes of pizza au na supermarket.
Huku nchi za Africa, matajiri wanakula mavitu ya KFC huku masikini wanakula bamia na mnavu mixer dagaa.
Kwahiyo shida ni mindset.
Hii kitu ilinishangaza baada ya kutembelea nchi za wenzetu kwa mara ya kwanza. Unachokieleza ndicho nilichokutana nacho
 
Wakati kilo ya nyama iko chini kuliko dagaa tena wale wa Zanzibar kilo ni 14000
Dagaa unakula milo mingapi na nyama unakula milo mingapi. Wewe uliona wapi familia ya watu wengi na kipato cha chini inaopt kilo ya nyama badala ya dagaa kisa wana bei. Au uliona wapi nyama ya kupima elfu moja kama mafungu ya dagaa.

Mimi huwa najilazimisha kula dagaa nyama wa buku kwa mlo mmoja, mara nyingi dagaa wa buku nakula milo miwili na kwa ugali tu. Ila nyama robo naweza kula kama mboga kwa mlo mmoja.
Kwahiyo kwenye kilo moja ya nyama naweza kulazimisha kula hata milo mitano ila mara nyingi ni nane. Ila kwenye dagaa nyama siwezi kula chini ya mara 16 kwa kilo moja.

Kitimoto nakula nusu, kilo simalizi. Sato na sangara kilo namaliza. Samaki wa baharini kilo simalizi. Kuku mzima simalizi.

Kuna namna dagaa zilivyo, dagaa kidogo inaenda na chakula kingi. Huwezi sikia mtu kala kilo ya dagaa kama ambavyo anakula paja la mbuzi.
 
Ukiishi kwa kusikiliza wanadamu wanasemaje kuhusu maisha yako,utateseka sana,
Ishi upendavyo,maisha ni yako,wala sio yao,life is very short,enjoy it before it's too late,

Love the life u live
Live the life u love.
 
Kilo ya dagaa eneo nililopo ni elfu 12,wakti nyama kilo ni elfu 9,so kipi chakula cha kimasikini hapo?
 
Wengi wetu maamuzi ya kupikwa dagaa au bamia hupitishwa baada ya bajeti kuwa tight hivyo watu wanatakiwa kula kutokana hela iliyopo mezani........

Dagaa na bamia inatazamika kama mboga ya wanyonge kutokana upatikanaji kuanzia kwa bei ya chini....kama huku mtaani dagaa fungu linaanzia mia tatu mpaka mia tano na bamia kuanzia mia mbili.....bei ambazo wanyonge tunazimudu....
 
Dagaa mixer bamia halfu ziwekewee karanga ....
Mtaniita maskini sana aiseee
 
Sa Si Ndio....
Dagaa waandaliwe vzr tuu,

OSHA hata mara tano maji ya vuguvugu mix ya baridii, wakaangwe na mafuta waivie vzr, tia mboga mboga hizo nyanya karoti hoho mix masala ya samaki, kama una kitunguu swaumu tia mix tangawizi, tia ndimu mix chumvi na pilipili wapenda nazi mix karanga au korosho wewe tuu,,
 
Write your reply...nguruka wa kuchoma unawajua wewe upate na maharage na figiri kwa ugali hatari au dagaa mchele
 
Imetoka kwa masikini waliopata pesa. Pesa au utajiri huwa havifuti umasikini bali umasikini hufutwa na ukarimu, upendo,kujitoa kwaajiri ya wengine,kujali wengine na kutokuwa mvivu.

Nilijifunza hili somo one time too many. Nitakupa kisa kimoja cha mzee pale Moshi. Yeye alikuwa ni mkarimu kupita maelezo. Yaani ni wale wazee wa bush ila tulipokwenda kumtembelea tukiwa na mjukuu wake. Tulifika pale alikuwa ana hangaika kutuandalia chakula, mara mbege mara atuletee ndizi.

Muda tunaondoka alitufungia maziwa mtindi na mahindi akatupatia na buku buku eti ya nauli.

Aiseee unajua kuna watu ni wakarimu hata kama hana kitu ila atakupa chochote mradi ujue umekarimiwa na yeye.

Umasikini ukikushika hata ukiwa billionaire kama hawa viongozi wa ccm bado utataka kunyang'anya michango ya harambee na utataka kugawana kodi na masikini.
 
Wakuu habari,

Kuna hili jambo linanitatiza na kunikasirisha sana, hivi hii dhana ya kwamba ukila bamia au dagaa wewe ni Masikini ilianzia wapi na inatokea wapi?

Yaani mimi niangaike kutafuta hela ninunue mboga ninyoipenda alafu mtu mwingine na fikra zake duni ahoji uwezo wangu wa maisha

Kwanza kuna dagaa nyama, dagaa mchele, dagaa wa Kigoma yaani unapika utakavyo iwe roast, kavu au mchuzi na kiafya dagaa ni chakula kinachosaidia kuongeza madini ya chuma aina ya kalsiamu na protini

Bamia pia ni mboga nzuri sana yenye virutubisho nyingi kwa Afya, sasa endeleeni kula pizzza na kubeza hivi vyakula

Dagaa na bamia unaweza kulia vyakula vingi tu hata ukiandaa roast yake mix

we acha utani na wasukuma bhana😁.....dagaa wa kwetu kigoma kilo "alufusitinangapi" unajua? naskia huko "dasalama" wanakula wadosi na watu fulani wenye kipato cha juu😁
sema mimi nadhani dagaa fulani na bamia ni kwa sababu ya upatikanaji na gharama zake za chini na kutojua faida za kiafya ndio inapelekea zionekane mboga za kimasikini, na ile kasumba ya chochote cha garama anatumia mwenye nazo🙏
 
Waambie tu kilo ya dagaa ni 12k, wakati kilo ya nyama ni 10k. Dagaa lipikwe na bamia/ngogwe upate na ugali+glass ya mtindi, afya tele kabisa.
 
Back
Top Bottom