Hivi hii tabia kwamba ukila dagaa au bamia wewe ni maskini inatoka wapi?

Dagaa nawapenda sana asee hasa wabichi. Binafisi Kwa kitu ninachopenda hata usemeje siwezi acha maadam hakuna madhara.

Nikiwa out nisipokula mkuu wa meza basi ni samaki hizo chips pizza nk nimeshawaachia ninyi maboss
 
Nachojua vyakula vinavyojenga mwili huwa vinadhauriliwa sana na masikini.

Masikini tunaamini kula vizuri ni kula Chips , soda , pilau nyama n.k na sio dagaa wala maharage japo kuna ukweli Fulani Kati ya umasikini na dagaa
Kama vinajenga mwili kwanini hatuendelei kama nchi?
 
Dagaa wa mwanza ukila kma upo dar wewe ni high class ila kanda ya ziwa wanaita misumaria 🤣🤣🤣
 
Issue ni bei ndg, hivyo vt ni vya bei ya chini, price discrimination. Ila kiukweli ni mboga za watu wenye uwezo mdg kwa kuwa ndio mboga wanayoweza kununua. Na msipambe umaskini, ungewekewa samaki na dagaa wangapi watachagua dagaa? Au uwekewe beaf, nyama ya kuku au ya kitimoto utachagua bamia kweli? Bamia na mboga za majani ni mboga za ziad pembeni mwa nyama au samaki. Huo ndio ukweli.
 
Kilo ya dagaa eneo nililopo ni elfu 12,wakti nyama kilo ni elfu 9,so kipi chakula cha kimasikini hapo?
Nyama Kg moja wanamaliza watu wawili au watatu Ila dagaa kg 1 hiyo ni mboga ya wiki nzima.

So hoja ya bei haina mashiko hapo Ila ungeangilia virutubisho n.k

Masikini Dagaa kwake inasaidia kuweka budget yake vizuri .
 
Mambo ya sizitaki mbichi hayo mkuu
 
Hii kitu ilinishangaza baada ya kutembelea nchi za wenzetu kwa mara ya kwanza. Unachokieleza ndicho nilichokutana nacho
Naam, hali hii inasababishwa na uchumi, Demand and Supply; nchi za Ulaya fresh food ni ghali sana kwa sababu hazipatikani kwa urahisi ndio maana masikini hawamudu kula. Huku kwetu, dagaa, mchicha, matembele, bamia ni bei ya bure kwa hiyo ndicho masikini wanamudu kuvipata.
Ulaya mkate ni bei kitonga kuliko bei ya bamia wala dagaa. Mfano, parachichi linalotoka Africa London linauzwa £2 (Pound 2) ambazo ni zaidi ya elfu 5 ya bongo, na mkate bei ni hiyo hiyo. Kwa mtu masikini heri anunue mkate akale kuliko kununua parachichi moja.
Kwetu Dar es Salaam parachichi lipo hadi la jero.
 
yaani ule dagaa za mafungu ya mia mia ulete stori za nikuone tajiri hapana aseeh
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…