Aise hujakosea kabisa na mtazamo wako, kuna kasinema nilitazama, kulikuwa na wakinamama wanaharakiti, walidai Mungu ni mwanamke!
Kwa kweli sikuona ajabu kabisa, bado siamini kama Mungu ni mwanaume, yawezekana sababu ya mabavu yetu na kujikakamuwa..
Ila mwanamke ndio kila kitu, hii lazima tukubali, kweli mbegu za kiume zahitajika, zaidi ya hapo sidhani kama sisi wanaume tuna la zaidi la kumshinda mwanamke, hili swala tuliangalie kwa makini sana, kukaa na mimba miezi tisa si mchezo (mwanaume hawezi), kuzaa ni kazi ngumu zaidi (nina imani sisi wanaume hatuwezi kabisa ule uchungu), kulea mpaka mtoto anajitegemea ni balaa, haya yote kwa upande wangu naamini mwanamke ni jabali zaidi, na sisi wanaume tulitakiwa kuongozwa naye..
Tuje kwenye ukatili, wanaume siyo wakatili, hata kidogo, mwanamke mkuu! Acha kabisa na ukatili wa mwanamke, akiamuwa kukufanyizia huponi!
Utafutaji, hapa mwanaume kapigwa ngwala ya kufa mtu, 100% wametushinda kwenye hili, hasa kama ana watoto...
Tabia nzuri, ustaarabu, upole, heshima na mapenzi, tena tumepigwa bao, wanaume tuko very selfish, tuko sana na "mimi mimi mimi)..mwanamke yuko selfish sawa, ila kwa familia yake, kwa zao lake, kuna ule usemi nyoka akiingia kwenye boma lenu na kutaka kudhuru mtoto, mwanaume atafanya nini? atatafuta silaha yoyote kwanza, mwanamke atamfuata nyoka bila silaha yoyote, amini usiamini atakayekufa pale ni nyoka!