Hivi hizi kampuni za kukopesha zinaruhusiwa kukamata mali za wadaiwa wao? Akina mama wanalia kila kona ya Tanzania.

Hivi hizi kampuni za kukopesha zinaruhusiwa kukamata mali za wadaiwa wao? Akina mama wanalia kila kona ya Tanzania.

Wamama wajasiriamali wanalia kila kona.

Wanapokwa mali za ndani kwa kutolipa madeni.

Je huu ni utaratibu?
Tanzania ni nchi ya wajinga inayotaliwa na kikundi cha wahuni (CCM). Kuna wengine nimeona jana wanalia kwa sababu kuna mtu anaitwa eti Mr Manguruwe kawatapeli fedha zao. Yaani huyo tapeli anajiita ni mfugaji wa nguruwe na unampa fedha zako ili ''akufugie'' nguruwe na faida anakulipa kila wiki tena fedha nyingi tu. Ni ule ule mchezo wa Mr Kuku au Ukulima wa Vanila. Narudia, Tanzania ni nchi ya mazoba kweli kweli.
 
Kwa sasa ukiwa na vijipesa kidogo na uthubutu basi unaweza vunja sheria yeyote ya nchi.

Anaepaswa kukemea hata hajui kinachoendelea as long as yake yanamnyookea. Yeye kauli yake moja tu, 'na hili mkalishughulikie'.

Kwa dalili zilizopo hizi taasisi zote za mikopo ya kausha damu zina baraka ya walioshika hatamu, hivyo hakuna chochote watachofanywa hao wanaovunja sheria.

Suluhisho ni dogo tu, usikope kwenye hizo taasisi kinyume na hapo kubali kuweka maisha yako rehani. Maana jamaa wakija kudai wana mpaka mamlaka ya kuua achilia mbali kuchukua samani zako.
 
Wamama wajasiriamali wanalia kila kona.

Wanapokwa mali za ndani kwa kutolipa madeni.

Je huu ni utaratibu?
Mkopeshaji kisheria anatakiwa kuchukua dhamana iliyotumika kuchukulia mkopo tu na si kitu kingine,hairuhusiwi kuchukua samani za mtu,ni kinyume Cha Sheria
 
Back
Top Bottom