Hivi hizi pesa za magoli ya Simba na Yanga zilipitishwa kwenye bajeti ipi?

Hivi hizi pesa za magoli ya Simba na Yanga zilipitishwa kwenye bajeti ipi?

Yanga kaitangaza nchi kwalipi ukilinganisha na ujumbe wa Visit Rwanda kwenye jezi za Arsenal,uoni kama ni vitu viwili tofauti? Sisi tunavivutio vingi kipi ambacho kimetangazwa kuputia Yanga.
Nchi ambayo hata watu hawajui ipo wapi kwenye Ramani Inatangazwa kwa Namna nyingi tu, Asilimia Kubwa ya Watu duniani hawajui kama Kuna Nchi inaitwa Tanzania, ni Rahisi hata Kenya kusema Mlima Kilimanjaro upo kwao sababu hatujulikani.

Kucheza fainali automatic umeitangaza nchi kwa mabilioni ya watu

Reuters

Unaweza ukakaa miezi hata hujaandikwa vyombo vya habari kama hivyo ila opportunity kama hii inakuongezea umaarufu
 
Hassan mwakinyo na vijana wengine wamekuwa wakipiga Game zao Ulaya na ktk mataifa mengine zaidi tena maarufu sana Duniani. Sijawahi ona wanapewa vitita vinene kama hvo au hata kutengenezewa tension kubwa kiasi hicho. Tunakwama wap?????
 
Acha maswali ambayo hata mtoto hawezi kuuliza.unafahamu Rais wetu alianza lini utumishi wa umma? Unafahamu amefanya kazi Taasisi ngapi? Amekuwa Waziri na mbunge kwa muda gani? Kwa hiyo kwa akili zako unafikiri hela hiyo anayoitoa mh Rais wetu mpendwa kutoa hamasa na kuleta morali kwa club na wachezaji wetu inaweza kumshinda? Unafikiri Hana hela hiyo? Kwani akitoa na kuwazawadia wachezaji na club zetu inazuia vipi yeye na serikali Yake kututumikia na kutupatia huduma watanzania? Lini ulisikia kuwa hospitali na shule zimefungwa kwa kukosa watumishi kwa kuwa Rais amewapa yanga au Simba zawadi?

Hujuwi kuwa michezo inachochewa secta ya utalii na biashara hapa nchini? Pesa na mabillioni mangapi yamewekezwa na wawekezaji katika michezo? Unafahamu Kodi kiasi gani inayokusanywa kutoka katika michezo? Unafahamu mabillioni mangapi yataingia katika benki za ndani ya nchi yetu pale club zetu zitakapo fanya vyema kimataifa? Hujuwi pesa ikiwepo ya kutosha benki Ina faida katika uchumi wetu? Hujuwi watu watakopa kupitia benki na kuongeza mzunguko wa fedha mitaani? Hujuwi watu watafungua biashara na kuongeza wigo wa Kodi? Hujuwi serikali utapata Kodi? Hujuwi fursa za ajira zitaongezeka kwa vijana kupitia michezo?

Hujuwi club zikifanya vyema zitapelekea biashara ya jezi kufanya vyema mitaani? Je hujuwi biashara hizi zitaongeza mapato ya kikodi?

Acha umbumbumbu wewe na kuandika tu mambo yasiyo ya msingi.mwache Rais wetu mzalendo na mchapa kazi aendelee kututumikia watanzania,Tunamuunga mkono na tupo tayari kumpa ushirikiano wetu

umeandika Pumba nyiiingiiiii


jibu ni moja tu.

Ofisi binafsi ya Raisi inatengewa fedha ambayo haijadiliwi kokote kwa sababu za usalama wa Taifa nfo huko kuna mavazi ya raisi, vyakula, Perdiem,Mshahara yeye na maposho ya mume na familia yake
 
Mbona matumizi hayo ya ghafla yapo mengi, leo nimesoma mahali ndege imetolewa bure kupeleka hao washindi Mbeya eti wanamalizia mafuta yaliyobaki ya ndege iliyowapeleka Algeria
 
Hii nchi tayari ccm wamejua udhaifu wa hao mashabiki wa simba na yanga na wao wamejipenyeza na wamekubalika sasa ni kujichotea tu pesa wanavyotaka huku wajinga wakiendelea kufurahia
 
Mbona matumizi hayo ya ghafla yapo mengi, leo nimesoma mahali ndege imetolewa bure kupeleka hao washindi Mbeya eti wanamalizia mafuta yaliyobaki ya ndege iliyowapeleka Algeria
😆😆😆
 
Ofisi ya rais haijatengewa pesa za matumizi mbalimbali? Kama hujawai kuwa hata monitor darasani huez elewa hii mambo
 
Je, tuseme Tanzania tuna pesa nyingi ambazo hazina matumizi yoyote ?
Sioni baya kweny support ya michezo pamoja na hayo ukipiga hesabu ni pesa ndogo san, jus'imagine zile Trillion hazikuidhinishwa na bunge bas walau tujue zilitumikaje lkn wap!!!
 
Nchi hii inaitaji Katiba Mpya. Hili kuondoa matumizi ya hovyo ya Kodi zetu.
 
Back
Top Bottom