Hivi hizi R na L zimetukosea nini?

Hivi hizi R na L zimetukosea nini?

Mara nyingi hizo R na L husababishwa na asili ya watu! Mfano watu wa Kanda ya Ziwa, kimsingi hawana L! Badala yake wana R tu!! Niretee ugari, Niretee Gwajima, nk.

Ukienda Dodoma, Iringa, nk huko hawana R! Badala yake wana L tu! Badala ya kutamka Iringa , wenyeji hutamka Ilinga! Dodoma nako kila neno lenye R, hugeuzwa na kuwa L! 'Napeleka malejesho', nk.

Mifano ni mingi, muda ni mchache.
Hatuna tatizo, hata uwe unatoka kwa wa Hadzabe. Kwenye kuongea tutaelewa ni lafudhi....tatizo linakuja kwenye KUANDIKA.
 
Hii imekuwa kama jadi yetu watanzania. Kupenda kubisha tunaposahihishwa. Mwanzisha thread ana point nzuri sana. Haya maneno uliyosahihisha mara nyingi yanaweza kuvumilika lakini siyo hili kosa la R na L.
Kwani mkuu, umeishia kidato cha ngapi![emoji848]
 
Yapo makosa yanayovumika kwenye kiswahili. Hivi unajua Zanzibar wanaandika ''mwengine'' na sisi tunaandika ''mwingine''?
Nafikiri hili ni swala(nimeambiwa ni suala eti) la lahaja za kiswahili. Hili sio tatizo, ila ni kwamba lahaja ziko tofauti kutokana na sehemu.

Kuna wengine humu wamenisahihisha mambo ambayo sio makosa, nikaamua kupotezea.... ni kama kiingereza unaweza ukasema "center" au "centre"

Ila huko kwenye R na L....hili hapana. Ndio maana tunatwangwa matozo kila kukicha.
 
Aibu yako mkuu, tena watu mnaokosea kwa mtindo huu, IQ zenu huwa ziko chini sana na mara nyingi huwa ni waropokaji pia mnajifanya wajuaji hasa kwenye masuala ya siasa na maendeleo uchwara
Natumai utakuwa umepata unafuu kwa kujipa moyo kuhusu IQ yangu kuwa ndogo. Sasa kwa IQ yako ya juu, nikukute unabomoa R na L zako.
 
Hili limekuwa tatizo haswa. Sijui kama nahitaji kubadilisha mtazamo wangu juu ya hili ila watu wengi wanaochanganya herufi R na L huwa nawachukulia kama vilaza fulani hivi.

Kuna mwandishi unakuta ndani ya andiko kuna sehemu kaandika, say, mnara na mbele kidogo kwenye andika hilo hilo unakuta kaandika mnala. Sasa unajiuliza huyu anatutega wasomaji wake au?

Na kuna maneno mengi yanatumika siku hizi, baada ya kuuliza nikajua wanachomaanisha

Mfano,

ko == kwa hiyo
Make == maana yake
Waga == huwa(ga)

Kuna kijana nilikuta kaandika teachel badala ya teacher, nikachoka kabisa.
 
Vilaza tupu.
 
Kwenye lugha ya kingereza, kitendo cha kukosea matumizi ya L na R kinaleta ukakasi. Mfano; Tly badala ya Try

Lakini kwenye kiswahili hakuna shida, mambo ni yaleyale tu, tusikaze mafuvu, lugha yenyewe ni ya kwetu, acheni tuichalange tuwezavyo
Mfano: Madhala ~ madhara, kwani hapo kipi hakijaeleweka?
 
Hembu chukulia mtu aseme Karamu badala ya kalamu,

Mkuu...ivi unajielewa kweli?
 
Inategemea na nature ya watuuuu! Kuna makabila huchanganya sana L na R na kuchanganya H inayoambatana na alfabeti
 
Back
Top Bottom