Hivi huku Mbweni wanaishi Watanzania? Haya majengo sio poa

Mkuu unajua bei za viwanja kweli? Kule kwa Mama viwanja vingi vikubwa vinakaribia ekari moja ,anzia kona ya Mama pale hadi kona ya kwenda baharini ,lile eneo la bara bara ya kwanza hadi ya 6 viwanja ni vikubwa sana ,si chini ya 500m.
Jamaa alisema kiwanja ukubwa wa 35kwa 40 jkt,kiwanja cha 500m hakuna labda kiwe eka,kule kwa mama vile ni special kesi hata tasisi zinazunguka na lazima uwe mzito
 
K.koo kuna nyumba tulikuwa tunaishi iliuzwa 23 million.....ilikuwa mwaka 2003
 
Mbweni ipi uswahilini? Mie siamini wallah.
Haha mdogo wangu jaza mafuta uje utembee ujionee au kama hauna gari funga safari nenda Makumbusho au Simu 2000, chukua daladala za Mbweni shuka kituo kinaitwa Miti Mitatu ingia ndani ndani halafu urudi hapa ulete mrejesho, kwanza kuanzia tu pale barabarani utakaposhuka mandhari yake yatakuonesha ni uswahilini
 
Hebu fanya mpango kajenge mavurunza. Hapo paache paongezeke thamani uuze.
 
Watu wengi wanapita ile njia ya chini hadi wanaenda kutokea city center ile huwa haina foleni sana
 
Kuna jamaa angu anajilaumu hadi leo hii kushindwa kununua Kiwanja Kariakoo miaka ya 98, anasema alipata mtu anataka kumuuzia bei nzuri lakini alikataa.

Leo hii 2024 huwezi kumudu gharama ya Kiwanja Kariakoo πŸ™Œ
Mkuu kariakoo kuna viwanja!? Nijuavyo mimi unanunua jengo la zamani unavunja na kujenga jipya la kwako!
 
Ni upuuzi tu wa mamlaka zenu ila nchi za wenzetu wenye utimamu wapo watu wanaishi moro na wanafanya kazi Dar na kila siku wanawahi makazini in minutes.
 
Pale mtaa wa malindi estate (Mbweni),Mwenyekiti wa mtaa Ni yule mkurugenzi mstaafu wa TBC Clement Mshana.

Unaweza ukapata picha halisi.
 
Mbweni ina Mitaa mitano tu, Mbweni (wengi wanapaita Geza), Malindi (ndio huko wengi wanapaita JKT), Mpiji, Teta na Maputo basi, hakuna sehemu inaitwa Mbweni Kijijini, Mtaa wa Mbweni mostly ni uswahilini

Mbweni Kijijini ni pale center wanapogeuzia magari ya Makumbusho-Mbweni ,Pale walipojazana wapemba/Mamwinyi ukienda Mbele kuna kamto kamepakana na kambi ya Jeshi - Kiembeni ,Pale hapajapimwa ni slum.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…