Hivi huyu dada Joyce Kiria ana shida gani?

Hivi huyu dada Joyce Kiria ana shida gani?

Mimi kama nimemuelewa tofauti Joyce anisamehe. Lakini akili yangu inanituma kuamini kuwa baada ya Joyce kuanika sakata hili kwenye media na shutuma alizopata toka kwa wachangiaji, sasa ameamua kuja na episode 2 ili watu wajue chanzo cha ugomvi wao ni ubahili/ubinafsi Wa mumewe na hii anadhani itamsaidia ku atract public sympathy. Lakini ukisoma vizuri maelezo yake unamwonea huruma kwa sababu between lines ameficha tabia yake na anachotaka kiuhalisia toka kwa mumewe. Lakini pia angalau ameeleza chanzo cha kupigwa kwake kuwa ni yeye kwenda "kujirusha" peke yake kama anavyofanya mumewe ili ngoma iwe droo, na anataka jamii ione kuwa kipigo toka kwa mumewe hakikuwa sahihi kwa vile alimkuta sehemu anayoifahamu na hakuwa akifanya zinaa kama yalivyokuwa mawazo ya mumewe. Tatizo la pili la Joyce ni kutofanywa Second signatory kwenye akaunti za mumewe wakati yeye amemfanya signatory kwenye akaunti zake. Katika hili Hoja ya Joy ni ya msingi lakini siyo nzito. Anakiri wakati hili linafanyika hakuona tatizo kwa sababu alikuwa na mapenzi thabiti kwa mumewe. Kwa maana nyingine kinachomfanya ahoji sasa hivi ni kupungua kwa hayo mapenzi thabiti ya awali. Sasa ni kipi kimeyapunguza hayo mapenzi? Ni pale Kilewo alipoacha kumjali na kumthamini, yaani kutoka out peke yake bila mkewe.
Je, haya ni ya kuanika hadharani hata kama kweli yapo? Jibu rahisi ni no, tena big NO! Kinachofanya ayaanike haya kwa sasa ni dhamira yake anayosema alimwambia mumewe tangu mwanzoni mwa mwaka huu, hajataja ni lini, kuwa "MWAKA HUU 2018 NI MWAKA WA KUACHANA".
Huwezi kudumu katika mahusiano kama akili yako umeshaiset kuachana. Ukilala unaota kuachana, ukiamka unawaza kuachana. Siku zote mawazo yanaumba dhamira na mwisho wa siku "UTEKELEZAJI". Joyce unatekekeza ulichokiwaza siku nyingi na sababu ulizotoa ni catalyst. Yaani ulitegesha kama wimbo mmoja Wa Mrisho Mpoto anaposema; "UKINIKANYAGA TU.....!"
Lakini Joy hujachelewa, la kwanza nakusihi acha kutumia njia hii ya kishamba kumdhalilisha mwanaume unayemuita baba Wa watoto wako, na sehemu nyingine umemuita "KILEWO WANGU". Tafuta wenye busara wakusaidie ama KUACHIKA kwa amani au KUREJESHA ndoa yako katika line.
Wasalaam;
Bila bin Bila!!
Ushauri mzuri sana huu, nataman nimtag akusome...!
 
Pamoja na yote mwanamke kaumbwa na roho ndogo sana so ilitakiwa huyu bwana amsaidie namna ya kutunza watoto sasa anakimbia na hawezi kutoa fedha popote bila sign yake kwenye biashara zao sasa huyo mwanaume amkomoa mkewe au watoto? Hapo ndipo usemi wa RIA MMBE unaposhika kasi kwa wachagga
 
Halafu huyo ndo anajiita mtetezi wa wanawakwe
Mungu nusuru aina ya wanawake hawa [emoji119][emoji119][emoji119]
 
Najaribu kutafakari aina ya wanawake tunaoishi nao sasa ni shida!Kilewo huyo si mkeo kwasasa!Mwanamke mwenye hekima hawezi ongea mambo ya chumbani hadharani hayo wanayafanya akina Giggy na Tunda!
Si ajabu siku kadhaa zijazo tukamwona yuko na Serengeti boy!
 
Bila kumumunya maneno, Huyo mwanamke hafai, tena hafai.

Sio hekima wala busara kwa mwanandoa kuja hadharani kuanika udhaifu wa mwenza wake au udhaifu wa ndoa yake. Ni sawa na golikipa kuamua kujifunga kisa anataka kumkomoa kocha wake.

Hakuna ndoa isiyopitia changamoto nzito nzito za kimaisha, ndoa iliyofanikiwa ni ndoa iliyoweza kutatua changamoto zake za ndani. Katika hili Joyce Kiria anapaswa kupambana kimya kimya ndani ya ndoa yake na akiona hayawezekani, basi anakaa zake kimya au anaachana na mwenzake kimya kimya tena kwa hekima.

Hivi nini kitatokea ikitokea kwa madai hayo kama ni kweli halafu Kileo amuendee mkewe na kumwomba msahama na kuamua kujirekebisha. Joyce Kiria ataweza kuyafuta hayo maneno kwenye jamii? Ujasiri wa mumewe(kama mwanaume) utatokea wapi tena?

Hichi kilichoandikwa hapa ni shutuma za upande mmoja tu, sio sahihi kuamini kila kitu mpaka kwanza tusikie na upande wa pili.

Ukichunguza vizuri, malalamiko yote msingi ni pesa tu. Joyce Kiria anasema alikuwa anamvumilia Kileo wakati Kileo akiwa hana pesa, ila hayuko tayari kuendelea kumvumilia Kileo wakati kwa sasa Kileo inaonekana ana pesa kisiri!!!
 
Mimi kama nimemuelewa tofauti Joyce anisamehe. Lakini akili yangu inanituma kuamini kuwa baada ya Joyce kuanika sakata hili kwenye media na shutuma alizopata toka kwa wachangiaji, sasa ameamua kuja na episode 2 ili watu wajue chanzo cha ugomvi wao ni ubahili/ubinafsi Wa mumewe na hii anadhani itamsaidia ku atract public sympathy. Lakini ukisoma vizuri maelezo yake unamwonea huruma kwa sababu between lines ameficha tabia yake na anachotaka kiuhalisia toka kwa mumewe. Lakini pia angalau ameeleza chanzo cha kupigwa kwake kuwa ni yeye kwenda "kujirusha" peke yake kama anavyofanya mumewe ili ngoma iwe droo, na anataka jamii ione kuwa kipigo toka kwa mumewe hakikuwa sahihi kwa vile alimkuta sehemu anayoifahamu na hakuwa akifanya zinaa kama yalivyokuwa mawazo ya mumewe. Tatizo la pili la Joyce ni kutofanywa Second signatory kwenye akaunti za mumewe wakati yeye amemfanya signatory kwenye akaunti zake. Katika hili Hoja ya Joy ni ya msingi lakini siyo nzito. Anakiri wakati hili linafanyika hakuona tatizo kwa sababu alikuwa na mapenzi thabiti kwa mumewe. Kwa maana nyingine kinachomfanya ahoji sasa hivi ni kupungua kwa hayo mapenzi thabiti ya awali. Sasa ni kipi kimeyapunguza hayo mapenzi? Ni pale Kilewo alipoacha kumjali na kumthamini, yaani kutoka out peke yake bila mkewe.
Je, haya ni ya kuanika hadharani hata kama kweli yapo? Jibu rahisi ni no, tena big NO! Kinachofanya ayaanike haya kwa sasa ni dhamira yake anayosema alimwambia mumewe tangu mwanzoni mwa mwaka huu, hajataja ni lini, kuwa "MWAKA HUU 2018 NI MWAKA WA KUACHANA".
Huwezi kudumu katika mahusiano kama akili yako umeshaiset kuachana. Ukilala unaota kuachana, ukiamka unawaza kuachana. Siku zote mawazo yanaumba dhamira na mwisho wa siku "UTEKELEZAJI". Joyce unatekekeza ulichokiwaza siku nyingi na sababu ulizotoa ni catalyst. Yaani ulitegesha kama wimbo mmoja Wa Mrisho Mpoto anaposema; "UKINIKANYAGA TU.....!"
Lakini Joy hujachelewa, la kwanza nakusihi acha kutumia njia hii ya kishamba kumdhalilisha mwanaume unayemuita baba Wa watoto wako, na sehemu nyingine umemuita "KILEWO WANGU". Tafuta wenye busara wakusaidie ama KUACHIKA kwa amani au KUREJESHA ndoa yako katika line.
Wasalaam;
Bila bin Bila!!
Ushauri mzuri sana, natamani uendelee kutiririka ili wengine wajifunze
 
Mtazima fegi zenu pale watakapoyamaliza na kuanza kupost picha ig za mahaba niue!!
 
Hana usuperwoman wowote wa kumfuga mwanaume.
Dem alijua siku zote ni mteremko jamaa atakua nazo. Kibao kilipogeuka kamanda alipokosa ubunge
kwa hiyo kama amekosa ubunge ndio amtegemee mkewe mpaka ela ya kununua boxer apewe na mke?.....huyu kilewo anapenda kulelewa sana
 
Mkuu mbona hawa sio wamachame?I mean Kilewo ni mpare na Kiria ni mkibosho au unataka kutuambia pia ni wahaya wote wanata
Sisi wahaya huwa tukifikisha umri wa kuoa wazazi hasa mama zetu huwa wanatukalisha chini na kutuhasa kamwe tusioe mwanamke mchagga au mmachame uwa wanatwambia mabaya na madhaifu yao mengi kwenye ndoa ikiwemo hayo yanatokea kwenye familia ya kileo ndo maana ni Nadra sana kumuona muhaya achana na hawa wahaya wasiopajua bukoba,huwezi kukuta kamuoa mtu wa makabila haya....those people are too selfish..!!
 
Ila jamani nimemponda sana huyu mwanadada post zangu za nyuma. Ila Ukiangalia maisha ya sasa wanaume wengi wamekua team kitonga. Alafu mbaya zaidi hawajui kujiongeza. Hapa kamanda alifeli kumuoa mwanamke aliyeachika kwa kuomba taraka kwa mwanaume wake wa kwanza. Ila swali linakuja kwa nn kamanda anapenda kitonga aka Ilula.
 
Kuoa Mwanamke wa Kichagga ni sawasawa na Kulikaribisha Kundi zima la Al Qaeda au Al Shabaab au ISIS nyumbani Kwako. Ngoja tu nibaki na hawa hawa Mademu zangu wa Kingoni, Kisukuma na Kinyiramba ambao hawana roho mbaya zilizotukuka na Unafiki wa Kiwango cha Kimataifa kama Mwanadada Joyce Kiria.
 
Mdogomdogo mpaka ataanika ya kaLemutuz [emoji23]
Wanawake tunawapenda sana na kuwaheshimu ni Mama zetu, ila omba sana usikutane na aliyefyatuka!
 
cd9720b7d829c8988a6fe36fc4c3c566.jpg

Nawaza tu alipomfuma Kilewo akidraw pesa Joyce alivyoangalia...

Pesa pesa mi nishaizila,siitaki kuiona.
 
Tatizo Joyce anakosea..awaite shilawadu..ajilize kama wastara..kesho mkulu bilanga lazima amtumie mnikulu...
 
Back
Top Bottom