Kiasi fulani nina hii hulka, licha ya kwamba sisikilizi radio/muziki nyumbani, ni nikiwa katika shughuli nje tu.Me naweza kukaa ndani kutwa nzima kila siku
Alafu muziki una hisia sana kama akili yako imetulia na kuusikiliza muziki vizuri utaenjoy sana unaweza kusikiliza tu beat na usizingatie yale maneno au kusikiliza tu maneno ukaachana na beat au pia ukawa unasikiliza feature mbalimbali zilizotengeneza hiyo beat na jinsi zilivyo unganishwa na kuwa beat kamili
Sent from my TECNO KC8 using JamiiForums mobile app
Boss we ni mtu WA kusini,iringa,songea au mbeya?Nadhani hii inamuadhiri zaidi mtu anayataka mawazo yake yawe yanakubalika tu kila mara, mimi uwa napenda kuwa free pale tunapojadili mada furani yani kama ntatoa mchango wangu na watu wakaukataa ni sawa, kama ntakuwa na ushahidi juu ya kile nikiongeacho basi ntawaonesha wakikataa tena sina muda wakuendelea kubishana nao na maisha yanaendelea siwezi kaa mbali na watu kisa wanapinga mitazamo yangu
Yaani uyo ni Mimi kabisa ,jamii Bado haijajua aina za watu aswa introvert,na hawajui hauwezi mbadilisha mtu kutoka introvert kuwa extrovert,Watu hatufanani mkuu Kuna watu tunapenda kua peke yetu haitusumbui Ila Mara nyingi inawasumbua wanaotuzunguka nakumbuka nikiwa primary Sina hili Wala like mama akaja akaniuliza eti una shida gani? Nikamwambia sina shida yoyote akaniambia mwalimu Fulani kaja kamuambia nitakua na tatizo la kisaikolojia kwa sababu ni mkimya Sana na sishirikiani na wenzangu kwa hiyo wanipeleke kwa mtaalam wa saikolojia nilishangaa maana Mimi nilikua najiona naongea tu vizuri na nacheza na wenzangu vizuri, hatukuongelea Tena Hilo suala mpaka nilivyojua mkubwa Ila mpaka Sasa hivi kila hatua ya maisha niliyopita comment huwa Ni zile zile utasikia we mpole,. we mkimya, mwingine anakuuliza hivi huwa unaongea kweli? Mbona unapenda kujifungia fungia, Kuna siku kazini mtu aliniambia watu wa aina yako ndio huwa wanajinyonga bila taarifa nikashangaa Sana maana sijawahi kwa na mawazo hayo hata.
Inabidi watu mjifunze kua binadamu hatufanani kitabia na Mara nyingi huwa mnaproject hisia zenu yaani Kama wewe ukikaa ndani muda mwingi unakua na stress unahisi kila anayekaa ndani ana stress hapana sio wote wako hivyo.
Yaani Kuna kipindi nikiwa chuo nilianza Hadi kujifunza tabia ambazo Sina ili tu nisiambiwe mpole sijui mkimya sijui nini baadae nikashindwa nikajua tu this is who I am kwa hiyo siku hizi naishi tu Kama mimi.Mtu alikiniuliza mbona mkimya Sana , mbona huongei namwambia naongea sana hujanifahamu tu vizuri.
Hata mimi, kama sina ratiba inayonitoa, naweza kuingia ndani ijumaa nikatoka alfajiri ya juma tatu.Ndio lifestyle nayopenda, siku nikiamua kutulia home simu naweka no distance nabaki mimi na mimi, mimi na Mungu
Mkuu Kiranga. Neno Haki mnalitumia vibaya saana.Ukishasema ni haki, hilo linatosha.
Huko kwenye usahihi utaanza ku debate sahihi kwa mtazamo wa nani?
Haina maana hawasiliani na watu, ila siyo mkaaji wa vijiweni, hana pa kwenda hushinda ndani kwake.Mtu unawezaje kuishi katika mfumo huu ?? mimi kwa kweli sipendi mtu anayejitenga tenga bila sababu za msingi hii tabia siyo nzuri maana vingi vitakupita usipokuwa makini
Kuna moment tu inatokeaga baadhi ya watu tunakua hivi.. Hapa ni kama unanizungumzia mimi wa kipindi flani hivi ila sikuizi najitahidi kujichanganya kiasi.Habari zenu wakuu?? Natumaini mpo salama kabisa. Okay mimi siyo muanzisha mada humu mara kwa mara ila mara nyingi nimekuwa napenda sana kusoma tu mada, story hata visa mbalimbali viinavyolweta na baadhi ya wadau wenzetu na kama itatokea nikaguswa sanaa basi mara moja moja huwa natupia comment ili mambo yawe swadakta kabisaa.
Sasa bwana mimi mwenzenu nina rafiki yangu (mwanaume ) ambaye huwa tunapeana michongo ya hapa na pale ili maisha yasonge, japo urafiki wetu una muda kidogo lakini mimi mwenzenu kuna kitu huwa sikielewi juu ya huyu mtu, huyu jamaa kama hamna mishe yeye ni mtu wakuchill sanaa ndani mpaka kuna muda huwa namuuliza " we jamaa hivi kukaa ndani peke yako huchoki??" .. yeye atakujibu mbona kawaida tu mkuu .( Hanywi pombe, hashabikii mpira kabisaaaa hata draft siyo mchezaji ni mimo ndiyo huwa namvuta twende kijiweni tukapige danari maana nipo vizuri mno kwenye huu upande basi atakuja tu na kuwa mtazamaji )
Sasa tisa kumi kilichonifanya mpaka nije humu kuwauliza ni hili, ukiachilia mbali kukaa ndani muda mrefu pekee yake. Ana tabia ya kupenda sana kusikiliza muziki, ila sasa yeye usikilizaji wake ndiyo unaonishangaza sana na nakaona nije niwaulizeni . Yaani anaweza kuplay wimbo mmoja tu huo huo akausikiliza hata kwa masaa matano mfano kuna wimbo wa costa titch unaitwa big flexa hapa naandika nimemuacha ameuplay huu wimbo, lakini nje na hapo ni mwezi sasa amekuwa akiusikiliza huu huu non -stop hata kwenye simu yake kama utaangalia most played song ni huu huu nilioutaja hapa, kabla ya hapo alikuwa anausikiliza wimbo unaitwa Dwala lam msaanii anaitwa Dj ksb . Tisa kumi namjua vizuri tu lugha anayoifahamu vizuri ni kiswahili na kiingereza cha tia tia maji ila sasa hizi nyimbo anazozisikiliza ni za kizulu hivyo najua kabisa haelewi kiimbwacho humo ... Miaka yake ni 27 kwa sasa.
Sasa je hii hali ni kawaida??. Maana mimi najua humu kuna watu mbali mbali ambao pengine mmeweza kukutana na watu wa namna hii na mkaweza kuwaelewa bila shida, naombeni na mimi mnisaidie maana kuna wakati nahisi mwenzangu anapitia wakati mgumu lakini nimeshindwa kujua, lengo ni kujaribu kumsaidia huyu ndugu yangu.. au ili niweze kumuelewa.
Asanteni
Boss we ni mtu WA kusini,iringa,songea au mbeya?
Wewe kama Watanzania wengi huwezi kunielewa kwa sababu hata serikali yako inakupa haki ya kupigiwa kura uchaguliwe kuwa mbunge au rais kuongoza nchi, halafu inakuwekea vikwazo kwenye kuitumia haki hiyo kwa kukuambia huwezi kuitumia mpaka uwe mwanachama wa chama cha siasa.
Mkuu kama uliachana na mtindo huu wa maisha nikupongeze sanaa huu mfumo wa kujifungia ndani kwa sisis unga unga mwana hautufai , mtu kama unataka kuishi hivi ni bora akahakikisha kweli anajiweza nje na hapo ndyo hawa tunaowasikia kila siku wamejinyonga ..Kuna moment tu inatokeaga baadhi ya watu tunakua hivi.. Hapa ni kama unanizungumzia mimi wa kipindi flani hivi ila sikuizi najitahidi kujichanganya kiasi.
Sawa lakin ushawahi kuwa karibu na watu wa namna hii ??... Ukweli siku jaribu ukae na mtu ana -play wimbo hauna mbele wa nyuma hata kwa dk 10 tu lazima kuna kijikero fulani kitakujia . Sasa hivi ndyo nijisikiavyo napokuwa karibu na huyu rafiki yangu .Kwanza jua mziki hauna Lugha, uimbwe kwa lugha yeyote, akina Ntombi walikua wanaimba kizuru, Makiadi na wenzie kilingara ila nyimbo zao zilipendwa sana Tanzania.
Bongo na nchi nyingi sana za kimaskini zinazofanana na sisi huwa kuna pressure kubwa ya social conformity. Ukienda tofauti na matarajio au mfumo wa maisha uliozoeleka na jamii husika unaonekana ni kituko, tofauti kabisa na maeneo yaliyoendelea ambayo kila mtu yupo busy na shughuli zake.Wabongo wengine wanapenda kulazimishana wote tuishi sawa.
Yani kama yeye anapenda kushinda bar, anataka na wewe lazima upende kushinda bar.
Ukiwa tofauti naye anakuona wewe si wa kawaida, anataka kukubadilisha uwe kama yeye.
Huyo rafiki yako mwambie au mshawiishi muende kwa wataalamu wa afya ya akili au wanasihi. Huko ndo atapewa tiba. Usidanganyike kuwa ni hali ya kawaida shida ipo hapo.Sawa lakin ushawahi kuwa karibu na watu wa namna hii ??... Ukweli siku jaribu ukae na mtu ana -play wimbo hauna mbele wa nyuma hata kwa dk 10 tu lazima kuna kijikero fulani kitakujia . Sasa hivi ndyo nijisikiavyo napokuwa karibu na huyu rafiki yangu .
Hili jambo linaua sana diversity na creativity na hatimaye kufanya watu wazidi kuwa masikini.Bongo na nchi nyingi sana za kimaskini zinazofanana na sisi huwa kuna pressure kubwa ya social conformity. Ukienda tofauti na matarajio au mfumo wa maisha uliozoeleka na jamii husika unaonekana ni kituko, tofauti kabisa na maeneo yaliyoendelea ambayo kila mtu yupo busy na shughuli zake.
Ni kweli mimi ni wa mziki mzee, ila siyo hizi nyimbo zenu ni zile akina Muhina Panduka, Fredy Mwalasha kurudi nyumaSawa lakin ushawahi kuwa karibu na watu wa namna hii ??... Ukweli siku jaribu ukae na mtu ana -play wimbo hauna mbele wa nyuma hata kwa dk 10 tu lazima kuna kijikero fulani kitakujia . Sasa hivi ndyo nijisikiavyo napokuwa karibu na huyu rafiki yangu .