Hivi huyu rafiki yangu anaweza kuwa mtu wa aina gani?

Sure Jombaa. Sorry OP for hijacking your thread.

Changamoto alizopita mwanzilishi wa NALA kampuni ya kutuma pesa kutoka nchi moja kwenda nchi nyingine ilimpelekea mpaka kupeleka makao makuu kuhamishia Kenya. Huu ni mfano halisi wa jambo ulilozungumza hapo juu.

Angalia kituko kuhusu BoT kuna vibali vya aina moja inachukua benki kuu ya Uingereza siku moja kuvipata hivyo hivyo kwa benki kuu ya Marekani, Kenya na Uganda vinachukua siku 10 za kazi pekee. Kwa upande Rwanda na Burudi ni siku 14 ila kwa Tanzania ni miezi 6.
 
Dah, hatari sana mkuu.

Asante kwa kuweka wazi haya mambo kwa takwimu.

Inawezekana watu wengi wasione muunganiko wa mambo yote haya, lakini kuna uhusiano mkubwa.

Mimi naona hatuja hijack thread ya OP, tumepanua mazungumzo na kwenda kwa kina kuonesha pembe nyingine za jambo alilolianzisha OP.

Inabidi tu normalize watu kuwa tofauti, si lazima wote tufikiri na kuishi sawa.
 
Huyu nini mimi kabisa kila kitu ulichokitaja kinanihusu kasoro hapo hapo kwenye draft,mimi ni mchezaji mzuri wa hilo dubwasha
Mchezaji mzuri wa draft na chess .. ..anakuwa mzuri Sana up stairs!
 
Mapenzi na muziki Hayana Lugha ,Haitaji kujua lugha yeyote kuelewa na kuupenda mziki au kumpenda mtu ,Sababu mziki ni Hisia na mapenzi pia nayo hisia ..Kwahiyo mtu kupenda mziki asiojua maana yake si sababu ,Na hivyo hivyo kwenye upendo hakuhitaji Lugha kumwelewa mtu anayekupenda au kumwelezea mtu unampenda
 
🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣 Nimekuelewa vizuro sana nashukuru sana ila hawa introvert basi wanazingua yani akikaa na sisi washikaji zake kwa dk kadhaa tu eti mipango yake itaferi hii dharau hii . Kwanza huyu jamaa yangu sidhani kama ata anahii mipango mimi najua dharau tu imemjaa ili aonekane yeye special kumbe hamna kitu
 
Sio dharau ndio nature yao iko hivyo pia ni wa siri wa mambo yao ukitaka kujua hilo wewe muhesabie miaka 5 mbele kuanzia sasa atakuja kukushangaza kitu hutoamini na utajiuliza maswali mengi sana halafu utamlaumu dah inakuwaje mshikaji katusua bila hata kunishirikisha mimi mshikaji wake wa karibu sasa alimshirikisha nani mipango yake.

Sent from my SM-C7000 using JamiiForums mobile app
 
Ni tabia ambayo hata mimi ninayo ngoja nisome nione kama ni tatizo au siyo tatizo nisije nikalea maradhi bila kujua.

Ila mimi nina tofauti kidogo,ikitokea verse fulani imenigusa sana nitai-rewind zaidi hata ya mara 20 then nikichoka nauacha wimbo huo huo baada ya muda nafanya tena vile vile ku-riwind.
 
Mkuu,

Jaribu kujisoma ili ujielewe.

Ila kibongobongo hata kama unatumia mkono wa kushoto na jamii imezoea kutumia mkono wa kulia utaambiwa una majini.

Hatupendi watu kuwa tofauti.
 
Mkuu,

Jaribu kujisoma ili ujielewe.

Ila kibongobongo hata kama unatumia mkono wa kushoto na jamii imezoea kutumia mkono wa kulia utaambiwa una majini.

Hatupendi watu kuwa tofauti.
Hakika umenena.

Napitia post moja baada ya nyingine naweza nikatoka na kitu.
 

Hatumii Username na Avatar yako [emoji848]
 
Nje ya mada hapa tunazungumzia kwa upande wa Tanzania sio dunia nzima.
 
Mkuu huyo jamaa ni kama Mimi tu, wimbo uki-catch feeling zangu naweza sikiliza hata siku mbili Yenyewe tu.. nafeel comfortable sana kuwa alone sometime. Naweza kushinda ndani hadi jioni. Mfano mzuri Leo. Nimeamka saa 10 kwenda kutafuta Msosi tu
 
Unatoa siri za kambini wewe, mwenzio yuko kwenye kozi ya CHAPUTA afu unataka akuoneshe mbinu zinazompagawisha hadi ashinde ndani pekeyake kutwa nzima kama Mwali?

Sent from my CPH2387 using JamiiForums mobile app
 
Kwa watu tunaopenda kusoma mtu kukaa ndani peke yako si ajabu.

We are comfortable in our own company, maybe with a book to engage our minds.

Nakumbuka darasa la nne niliazimwa kitabu cha Willy Gamba cha Njama.

Sasa mtaani kwetu watu walikuwa wanaoenda dana kusoma riwaya za Aristablus Elvis Musiba za jasusi Willy Gamba, halafu vitabu vichache vinatembea nyumba hadi nyumba.

Basi niliazimwa kitabu nikaambiwa nikisome kwa siku moja tu nikirudishe.

Aliyeniazima alijua siku moja maana yake kaniazima leo asubuhi nitamrudishia kesho.

Nilikisoma kile kitabu siku ile kuanzia asubuhi mpaka jioni, jioni yake nikamrudishia nishamaliza kusoma.

Jamaa hakuamini speed yangu ya kusoma.

Sasa mtu hapa napiga piano, hapa naangalia movie, hapa nina games, hapa nina gym ina mazagazaga yote, hapa nina computer network with servers, laptops, desktops, including a Plex server, movies za Netflix na Prime just to mention a few, hapa nina library ina vitabu zaidi ya 10,000, hapa nina bar ina vinywaji vya kila aina, hapa nina music systems ambazo zinatosha kufungua nightclubs kadhaa, complete with DJ sets, all tye way to the garage, hapo natoka nje kufanya nini bila mpango maalum?

Na hata nikiamua kutoka nje natoka nyuma kwenye kwenye deck nina grill nyama choma ninavyotaka, nikitaka kuongea na watu nina simu ina unlimited internet, ambayo hata siitumii kwa sababu nina Wifi, hapo natoka kwenda wapi bila shughuli maalum?
 
Hiyo ni kawaida sana tena huyo jamaa tunaendanda sana mm ndivyo nilivyo, siyo nyimbo tu mm hata beat naweza nkasikiliza hata week nzima
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…