Hivi ilikuwaje Rais wa nchi akaenda kuigiza akiwa bado madarakani?

Championship

JF-Expert Member
Joined
Aug 7, 2019
Posts
5,500
Reaction score
10,616
Hiki kitu bado kinanipa ukakasi sana. Nimeona post muda huu linkedin ya yule Peter kamshika mkono Rais nikakereka sana. Japo ni post ya mwezi uliopita ila imeniumiza.

Pengine ni ushamba wangu lakini dah, kila nikiangalia naona kama Rais wetu ameonekana wa kawaida sana. Ni kama vile urais ni kazi cheap kabisa. Nafasi ya urais imedhalilika sana.

Movie ingeweza kutengenezwa kwa kutafuta mtu anayefahamika duniani kwenye hiyo tasnia.
 
Mkuu kwani rais siyo wa kawaida......kujikweza inategemea na hulka ya mtu alivyo, ulibahatika kumwona Mwl. Nyerere namna alivyoishi? alikuwa hadi anacheza bao kijiweni na kupanga foleni ya kununua sukari.
 
Ninyi kizazi cha nyoka, lini mtaweza kuziona fursa mnazotayarishiwa?
 
Mkuu kwani rais siyo wa kawaida......kujikweza inategemea na hulka ya mtu alivyo, ulibahatika kumwona Mwl. Nyerere namna alivyoishi? alikuwa hadi anacheza bao kijiweni na kupanga foleni ya kununua sukari.
Sukuma gang hao, wamezoea yale mambo ya Mwendakuzimu alivyokuwa akijifanya 'mungu mtu'.
 
Mkuu kwani rais siyo wa kawaida......kujikweza inategemea na hulka ya mtu alivyo, ulibahatika kumwona Mwl. Nyerere namna alivyoishi? alikuwa hadi anacheza bao kijiweni na kupanga foleni ya kununua sukari.
Mazingira ni ya tofauti sana kipindi cha Nyerere na sasa. Halafu mwalimu hakufanya hizo kama official activities. Alikuwa anajichanganya na watu wake.

Unaweza kufikiria umuone rais wa marekani au urusi anaigiza movie?
 
Sukuma gang hao wamezoea yale mambo ya Mwendakuzimu alivyokuwa akijifanya 'mungu mtu'.
Mkuu hii haihusiani kabisa na hayo ya sukuma gang. Mimi nimempinga magufuli siku zote na udikteta wake.

Ila bado sijaweza kuelewa rais anaanzaje kuigiza akiwa madarakani.

Unaweza kufikiria siku umuone raisi wa ufaransa au waziri mkuu wa japan au UK anaigiza movie akiwa madarakani?
 
Hiki kitu bado kinanipa ukakasi sana. Nimeona post muda huu linkedin ya yule Peter kamshika mkono Rais nikakereka sana. Japo ni post ya mwezi uliopita ila imeniumiza.

Pengine ni ushamba wangu lakini dah, kila nikiangalia naona kama Rais wetu ameonekana wa kawaida sana. Ni kama vile urais ni kazi cheap kabisa. Nafasi ya urais imedhalilika sana.

Movie ingeweza kutengenezwa kwa kutafuta mtu anayefahamika duniani kwenye hiyo tasnia.
Ondoa tongotongo machoni
 
What's your take kuhusu Nyerere kujichanganya na kucheza bao na 'majobless'? Au utaitafutia excuse kwa kuwa target yako ni Samia?
 
kabla ya kuhoji hayo kwanza ulitakiwa kujuwa maana ya royal tour kaka ukishaijuwa maana yake baaasi hutakuwa na maswali tena alu omba uelimishwe kuhusu royal tour siyo kila mtu anafanya
 
Hiyo ndio sawa na kuigiza muvi?
 
kabla ya kuhoji hayo kwanza ulitakiwa kujuwa maana ya royal tour kaka ukishaijuwa maana yake baaasi hutakuwa na maswali tena alu omba uelimishwe kuhusu royal tour siyo kila mtu anafanya
Hilo ni jina tu, lingeweza kutafutwa lingine.
 
Mazingira ni ya tofauti sana kipindi cha Nyerere na sasa. Halafu mwalimu hakufanya hizo kama official activities. Alikuwa anajichanganya na watu wake.

Unaweza kufikiria umuone rais wa marekani au urusi anaigiza movie?
Unasema alikuwa anaigiza wakati alikuwa kwenye mazingira halisi akishiriki kwenye matukio ambayo ni halisi kabisa ya kuitangaza nchi kiutalii....
 
Hilo ni jina tu, lingeweza kutafutwa lingine.
hata kama lingetafutwa lingine lakini maudhui yake ndiyo yanamfanya rais ashiriki unakumbuka hii kitu hata kagame alishafanya? au huna hiyo historia
 
Unasema alikuwa anaigiza wakati alikuwa kwenye mazingira halisi akishiriki kwenye matukio ambayo ni halisi kabisa ya kuitangaza nchi kiutalii....
Sina tatizo na kuutangaza utalii wetu, ni wazo jema. Ukakasi upo kwa raisi kuigiza.

Ingekuwa documentary ni sawa na ushiriki wake ungekuwa official lakini sio vile kwenye uigizaji.
 
hata kama lingetafutwa lingine lakini maudhui yake ndiyo yanamfanya rais ashiriki unakumbuka hii kitu hata kagame alishafanya? au huna hiyo historia
Kagame aliigiza au alishiriki kwenye documentary?
 
Wakati Rais Paul Kagame anafanya Royal tour alikuwa shamba boy wako?
 
Back
Top Bottom