Kudhalilishwa rais wetu ni fursa!! Tafadhali!! Hiyo pesa inayopatikana kwa kumdhalilisha rais wetu ni pesa chafu!! Heshima ni bora kuliko pesa!! Rais ni nembo ya nchi, watu wamekereka mpaka basi!!
Simlaumu rais binafsi lakini ninalaumu sana Rais kama taasisi!! Hii taasisi ina wasaidizi lukuki, kwa nini hawa wasaidizi hawakuliona hili? Ina maana hawa wasaidizi hawakuwahi kuiona hii filamu hadi ilipozinduliwa?? kama waliiona ina maana walilidhia huo udhalilishaji? Hata rais wetu wa awamu ya tano amepigwa kijembe na hilo li-Peter na wao hadi leo kimyaa!!
Ninachofahamu, kabla ya kurekodi filamu huwa kuna mazoezi/rehersal! Ina maana mazoezi ya jinsi watakavyoshikana mikono yalifanyika?