Hivi inakuaje mwanaume mzima unapata GPA below 4.5 chuoni?

 
Kwa elimu yetu Watu wenye uwezo mkubwa wa kukariri na hawana misheni zingine za kufanya lazima upate GPA kubwa
Yeah gpa kubwa inafaida zake kama mtu ataweza kuitumia kufika mbali zaidi kielimu , ninao mfano wa Dr mmoja mtanzania gpa kubwa ilimfanya kapata chuo kizuri US, kafanya kazi huko , na sasa kuna kipindi anaenda mhimbili kufundisha radiology.
 
Kuwa na GPA kubwa ni vizuri maana ni added advantage kwenye baadhi ya kazi.
Ukiwa na GPA ndogo kuna baadhi ya kazi huwezi ruhusiwa kuomba.
Nakumbuka wakati nimemaliza chuo sina mchongo wa kazi .Crdb wakatangaza nafasi za Graduate training programme GPA ilikuwa wanataka above 3.5 ndio ilinifanya nikapata ile opportunity.
Baada ya hapo ajira yangu ya sasa kwa mfaransa sikuombwa hata cheti.
 
We ume
 
Utoto raha sana joined 2025.

GPA za chuoni hazikuandai kuwa mwanaume kamili, mwanaume hupimwa kwa vision, kazi, na uwezo wa kusimama kwa miguu yake na sio GPA tu kama ulivyokalili kijana.

Halafu utuambie hiyo GPA yako umapata chuo gani na kozi gani.
 

Attachments

  • Screenshot_20250908_164222_Chrome.jpg
    11.2 KB · Views: 18
EACOP walitiki mkuu hongera sana.
 
Na cha kushangaza zaidi pamoja na Wewe kuitambia hii GPA yako ya 4.5 bado una Dhiki nyingi za Kimaisha (namaanisha Maisha yamekupiga sana) huku wenye GPA za 2 Gentleman / Pass na za 3 Lower Second Class wakiwa wana Maisha mazuri kiasi kwamba wanawaze hata Kukuajiri uwe unafanya Usafi katika Vyoo vyao.
 
Hauwezi kunishauri wewe mwenye 4.3 unahisi kupata above 4.5 GPA muhimbili na kazi ndogo? Nitokee hapa
 
Elimu bora yenye mabadiliko chanya ni ile inayomfanya mhitimu kuweza kutatua changamoto zake na jamii inayomzunguka.
 
Swadaktaaaaaaa!! Umemaliza kila kitu.
 
GPA kubwa ina faida sana, ni wewe tu kushindwa kuitumia ndio utaangukia kwenye kubeba zege. Ila watu wanaojua kutafuta fursa GPA zimewasaidia sana

Tatizo hapa mleta mada amehusisha GPA na uanaume, vitu ambavyo havina uhusiano kabisa, inaonekana hakuwa na mpango wa kuelimisha watu kuhusu GPA bali alitaka kudhihaki watu ambao hawakupata GPA kubwa ili wajisikie vibaya, na yeye ndio ajisikie vizuri.
mkunga wa jadi sio vizuri kuandika maneno kama hayo, wewe kama ni msomi jaribu na mada zako kuziandika kisomi
 
Kozi achana nayo, nilikua pale COET, 4yrs.
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ Sasa mm nikijua kozi kuna shida gani lakini. Ila hongera inaonekana ulisoma kozi za Uhandisi na ww ni mwanamke. Kuna mtu hapo juu kasema Uhandisi ni kozi ya kiume, muelimishe kuwa hata nyie mnasoma
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…