Kuna waliojibu sahihi lakini naona kama wameeleza sana.
Jinsi ilivyo ni hivi, Kuna lugha ya kiarabu, ya kitaifa official,
Alafu kuna lugha ya kiarabu iliotumika katika dini ya kiislam, ambayo haitokuja badilika ata shetani akija duniani habadilishi.
Hivyo basi nchi yeyote ya kiarabu katika hii dunia, haiwezi kusoma Qur'an kama haijasoma lugha ya Qur'an,
Watanzania wengi hatuwez soma lugha ya gazeti la kiarabu sababu wengi wao tunasoma lugha ya dini, Qur'an, ambayo ndo muhim katika dini
Ni mashkh wachache ndo wana weza kwa sababu wao walienda kusoma nje ya nchi.
Mimi binafsi mswahili, hata ukiniletea muarabu kutoka wapi au profesa wa lugha ya kiarabu kama hajasoma lugha ya dini (iliotumika katika Qur'an) hanifikii hata hafanyaje hawez nifikia sababu hajasoma.