Serikali imeweka mafao makubwa serikalini, bungeni na mahakamani kwa viongozi wakubwa inakuwaje pamoja na kuwa wana uhakika wa kupaa mapato makubwa sasa na maisha yao yote bado wanakuwa vibaka wa kula kwa urefu wa kamba zao?
Mwenyezi Mungu atusaidie kwenye hili wanataka nini hasa?
Nature ya wanadamu ni kuwa na ego/umimi/ mimi na familia yangu. Au sisi watu wa daraja hili tunastahili hiki.
Actually Kenya pamoja na kuwa na katiba mpya malipo yao na stahiki zao za wabunge, magavana na wengineo kwenye mifumo ni za "kufa mtu" ukizingatia wamegatua madaraka na wana mabunge mawili.
Wazungu hawa ambao wametutawala na kutuibia kwa miaka mingi na wana uchumi mkubwa kabisa, bado wanakuja kwetu huku na kuwaivisha watia sahihi mikataba ili waendelee kukomba mboga kwenye vyungu vyetu.
Pengine tupata malaika ndio waje watutawale na wasimamie mgawanyo wa rasilimali zetu, hapo tunaweza kuwa na suluhu.
Hao wa vyama shindani wanaodai katiba mpya, ukichunguza kwa juu juu namna uendeshaji wa ofisi, ukodishwaji na umiliki wa zile double cabin, ukodishwaji wa chopper, ukiomba accountability report, haitatolewa kirahisi kwa maana vitabu vya hesabu ya ngawira sio safi.
Baadhi yetu tunakumbuka ZZK pamoja na "usanii wake", akuwa mkiti wa PAC alitaka CAG akachunguze ruzuku wanayopewa CDM inafanya nini. Walimnunia sana na akaishia kutimliwa.
Na kuna wakati bilionea Sabodo aliwapa mtonyo wa 100mil wajenge ofisi yenye hadhi wahame pale ufipa; misallocation ya hiyo 100mil hajawahi kuwa wazi. 100 mil sio hela nyingi walau uwazi na ukweli ungekuwepo.
Well, tukomaeni na katiba mpya tukitegemea discretion ya mtawala kama atapata hiyo bajeti ya kuwezesha michakato. Na hivi with time madam SSH kapata wapambe wengi ambao wanajiita "chawa" kinyume ahadi za mwana-TANU na baadae CCM. Binadamu wote ni sawa, yet kuna wanadamu graduate wa vyuo vikuu wanathbutu kwa ujasiri kujiita mimi ni chawa wa fulani. Na fulani nae hatujaona akikemea watu kujiita chawa wake.
Ili kuondoa kelele, katiba mpya na ije tuone kama tutakuwa na mabadiliko significant.
Nihitimishe kwa mfano mdogo tu, tulipigwa kwa escrow, kuna watu walivuta mgao wa kufanikisha rada kununuliwa. Ila hao majemedari waliovuta sana, wapo mtaani na hawagusiki na inajulikana "walitupiga". Juzi hapa kuna traffic amekamatwa na viji-hela nyuma ya gari na mapicha-picha yanasambaa. Si ajabu "akapugwa", ila jamii anajua huyu amekutwa na "ngozi" tu, ila huo mchezo upo sana tu.
Je sheria ya sasa inahalalisha wizi? La hasha. Kwa wanadamu hawa hawa, ikija katiba mpya kuna jipya sana litafanyika??