Hivi inakuwaje mtu anatunzwa na Serikali maisha yake yote halafu bado anataka kula kwa urefu wa kamba yake

Serikali imeweka mafao makubwa serikalini, bungeni na mahakamani kwa viongozi wakubwa inakuwaje pamoja na kuwa wana uhakika wa kupaa mapato makubwa sasa na maisha yao yote bado wanakuwa vibaka wa kula kwa urefu wa kamba zao?

Mwenyezi Mungu atusaidie kwenye hili wanataka nini hasa?
Matatizo ya aina hii yangeweza kupunguzwa sana kwa kuwa na serikali za majimbo zinazosimamia mapato na matumizi kwenye majimbo yao. Pesa zinazokusanywa Namtumbo kupita kwenye mikono ya watu wengi nalo ni tatizo kubwa.
 
Urefu wa kamba ni ukubwa wa mshahara. Ni matumizi ya lugha za mafumbo tu.
Usimlishe mabeno ambayo hakusema hotuba yake ilikuwa clea bila chenga kueleweka kwa kila mtu kwa kiswahili rahisi na cha wazi
 
Katiba hata ya sasa hairuhusu hayo onyesha kifungu kinachoruhusu kula kwa urefu wa kamba
Elewa kwamba katiba ya sasa hivi inampa Raisi mamlaka na nguvu nyingi hawezi kihojiwa kwa kauli zake kama hizo ndo manaake, Raisi haogope lolote anaongea na kufanya kwa utashi wake bila uoga katiba ya sasa inamsapoti sana,..... waziri mkuu wa wingereza anaombwa kujiuzuru kwa kufanya kosa dogo tu la kukusanyika na kunywa pombe kipindi cha korona tu, imagine katiba yao ina nguvu
 
Serikali imeweka mafao makubwa serikalini, bungeni na mahakamani kwa viongozi wakubwa inakuwaje pamoja na kuwa wana uhakika wa kupaa mapato makubwa sasa na maisha yao yote bado wanakuwa vibaka wa kula kwa urefu wa kamba zao?

Mwenyezi Mungu atusaidie kwenye hili wanataka nini hasa?
Muulize bwana yuleeeeee, anayetaka kujipimia kwa wachina kwenye kivuko cha mabaga ya moyoni...........
 
Serikali imeweka mafao makubwa serikalini, bungeni na mahakamani kwa viongozi wakubwa inakuwaje pamoja na kuwa wana uhakika wa kupaa mapato makubwa sasa na maisha yao yote bado wanakuwa vibaka wa kula kwa urefu wa kamba zao?

Mwenyezi Mungu atusaidie kwenye hili wanataka nini hasa?
Nature ya wanadamu ni kuwa na ego/umimi/ mimi na familia yangu. Au sisi watu wa daraja hili tunastahili hiki.

Actually Kenya pamoja na kuwa na katiba mpya malipo yao na stahiki zao za wabunge, magavana na wengineo kwenye mifumo ni za "kufa mtu" ukizingatia wamegatua madaraka na wana mabunge mawili.

Wazungu hawa ambao wametutawala na kutuibia kwa miaka mingi na wana uchumi mkubwa kabisa, bado wanakuja kwetu huku na kuwaivisha watia sahihi mikataba ili waendelee kukomba mboga kwenye vyungu vyetu.

Pengine tupata malaika ndio waje watutawale na wasimamie mgawanyo wa rasilimali zetu, hapo tunaweza kuwa na suluhu.

Hao wa vyama shindani wanaodai katiba mpya, ukichunguza kwa juu juu namna uendeshaji wa ofisi, ukodishwaji na umiliki wa zile double cabin, ukodishwaji wa chopper, ukiomba accountability report, haitatolewa kirahisi kwa maana vitabu vya hesabu ya ngawira sio safi.
Baadhi yetu tunakumbuka ZZK pamoja na "usanii wake", akuwa mkiti wa PAC alitaka CAG akachunguze ruzuku wanayopewa CDM inafanya nini. Walimnunia sana na akaishia kutimliwa.
Na kuna wakati bilionea Sabodo aliwapa mtonyo wa 100mil wajenge ofisi yenye hadhi wahame pale ufipa; misallocation ya hiyo 100mil hajawahi kuwa wazi. 100 mil sio hela nyingi walau uwazi na ukweli ungekuwepo.

Well, tukomaeni na katiba mpya tukitegemea discretion ya mtawala kama atapata hiyo bajeti ya kuwezesha michakato. Na hivi with time madam SSH kapata wapambe wengi ambao wanajiita "chawa" kinyume ahadi za mwana-TANU na baadae CCM. Binadamu wote ni sawa, yet kuna wanadamu graduate wa vyuo vikuu wanathbutu kwa ujasiri kujiita mimi ni chawa wa fulani. Na fulani nae hatujaona akikemea watu kujiita chawa wake.

Ili kuondoa kelele, katiba mpya na ije tuone kama tutakuwa na mabadiliko significant.

Nihitimishe kwa mfano mdogo tu, tulipigwa kwa escrow, kuna watu walivuta mgao wa kufanikisha rada kununuliwa. Ila hao majemedari waliovuta sana, wapo mtaani na hawagusiki na inajulikana "walitupiga". Juzi hapa kuna traffic amekamatwa na viji-hela nyuma ya gari na mapicha-picha yanasambaa. Si ajabu "akapugwa", ila jamii anajua huyu amekutwa na "ngozi" tu, ila huo mchezo upo sana tu.
Je sheria ya sasa inahalalisha wizi? La hasha. Kwa wanadamu hawa hawa, ikija katiba mpya kuna jipya sana litafanyika??
 
Kwani katiba ya sasa ina ruhusu hayo? Ni wapi hapo?
Katiba inayompa Rais mamlaka ya kuwa mkuu wa nchi & Serikali.

Katiba inayompa Rais nafasi ya kumteua CDF&IGP..

Katiba inayompa Rais kuteua RC's & DC's.

Katiba inayompa Rais mamlala kuteua Wakurugenzi.

Katiba inayompa Rais mamlaka kuteua Mkurugenzi wa Tume ya uchaguzi (NEC ) halafu wanaenda kusimamia uchaguzi wa aliyewateua😂😂.

Katiba inayompa Rais mamlaka ya kumteua katibu mkuu ,mawaziri, manaibu waziri bila merit yoyote(haulizwi kwa chochote)

Katiba inayompa Rais mamlaka ya kuteua wabunge 10 bila sababu yoyote(hapa hata wapenzi wa zamani wanaweza kwenda mjengoni kugonga meza).

Katiba inayokataza matokeo ya Rais kupingwa mahakamani.

Katiba inayozuia Rais kuburuzwa Kortini hata kama amekosea awapo au akitoka madarakani.

Katiba inayoruhusu Rais mstaafu licha ya kulipiwa gharama zote bado anaendelea kuvuta 80% ya mshahara wa Rais aliyepo madarakani.

Katiba inayosema mbunge akiwa na elimu ya darasa la 7 na anajua kusoma na kuandika ruksa kwenda kugonga meza na kusema ndio hata kama hajui kilichomo kwenye mkataba.

Hayo ni machache tu!
 
Serikali imeweka mafao makubwa serikalini, bungeni na mahakamani kwa viongozi wakubwa inakuwaje pamoja na kuwa wana uhakika wa kupaa mapato makubwa sasa na maisha yao yote bado wanakuwa vibaka wa kula kwa urefu wa kamba zao?
Tatizo viongozi wetu wengi ndani ya ccm wizi, ukwapuaji, 'udalali' na utapeli umeshakuwa ndio dira yao na taaluma yao.
 
Nature ya wanadamu ni kuwa na ego/umimi/ mimi na familia yangu. Au sisi watu wa daraja hili tunastahili hiki.

Actually Kenya pamoja na kuwa na katiba mpya malipo yao na stahiki zao za wabunge, magavana na wengineo kwenye mifumo ni za "kufa mtu" ukizingatia wamegatua madaraka na wana mabunge mawili.

Wazungu hawa ambao wametutawala na kutuibia kwa miaka mingi na wana uchumi mkubwa kabisa, bado wanakuja kwetu huku na kuwaivisha watia sahihi mikataba ili waendelee kukomba mboga kwenye vyungu vyetu.

Pengine tupata malaika ndio waje watutawale na wasimamie mgawanyo wa rasilimali zetu, hapo tunaweza kuwa na suluhu.

Hao wa vyama shindani wanaodai katiba mpya, ukichunguza kwa juu juu namna uendeshaji wa ofisi, ukodishwaji na umiliki wa zile double cabin, ukodishwaji wa chopper, ukiomba accountability report, haitatolewa kirahisi kwa maana vitabu vya hesabu ya ngawira sio safi.
Baadhi yetu tunakumbuka ZZK pamoja na "usanii wake", akuwa mkiti wa PAC alitaka CAG akachunguze ruzuku wanayopewa CDM inafanya nini. Walimnunia sana na akaishia kutimliwa.
Na kuna wakati bilionea Sabodo aliwapa mtonyo wa 100mil wajenge ofisi yenye hadhi wahame pale ufipa; misallocation ya hiyo 100mil hajawahi kuwa wazi. 100 mil sio hela nyingi walau uwazi na ukweli ungekuwepo.

Well, tukomaeni na katiba mpya tukitegemea discretion ya mtawala kama atapata hiyo bajeti ya kuwezesha michakato. Na hivi with time madam SSH kapata wapambe wengi ambao wanajiita "chawa" kinyume ahadi za mwana-TANU na baadae CCM. Binadamu wote ni sawa, yet kuna wanadamu graduate wa vyuo vikuu wanathbutu kwa ujasiri kujiita mimi ni chawa wa fulani. Na fulani nae hatujaona akikemea watu kujiita chawa wake.

Ili kuondoa kelele, katiba mpya na ije tuone kama tutakuwa na mabadiliko significant.

Nihitimishe kwa mfano mdogo tu, tulipigwa kwa escrow, kuna watu walivuta mgao wa kufanikisha rada kununuliwa. Ila hao majemedari waliovuta sana, wapo mtaani na hawagusiki na inajulikana "walitupiga". Juzi hapa kuna traffic amekamatwa na viji-hela nyuma ya gari na mapicha-picha yanasambaa. Si ajabu "akapugwa", ila jamii anajua huyu amekutwa na "ngozi" tu, ila huo mchezo upo sana tu.
Je sheria ya sasa inahalalisha wizi? La hasha. Kwa wanadamu hawa hawa, ikija katiba mpya kuna jipya sana litafanyika??
Mkuu uneongea point nyingi sana za uhakika zilizoenda shule nakubaliana na wewe kwa asilimia 99
 
Katiba mpya lazima iwe na vipengele katili. Kuna viongozi wengi sana wa kunyonga
 
Tatizo viongozi wetu wengi ndani ya ccm wizi, ukwapuaji, 'udalali' na utapeli umeshakuwa ndio dira yao na taaluma yao.
You are right hundred percent ume wa define vizuri in one sentence una akili za uhakika za kufa MTU

Sentence moja uliyoandika inebeba kila kitu kuwahusu asante
 
Back
Top Bottom