Hivi inakuwaje mtu anatunzwa na Serikali maisha yake yote halafu bado anataka kula kwa urefu wa kamba yake

Hivi inakuwaje mtu anatunzwa na Serikali maisha yake yote halafu bado anataka kula kwa urefu wa kamba yake

Binadamu hasa Mwafrika ni ngumu sana kutosheka....
 
Urefu wa kamba ni ukubwa wa mshahara. Ni matumizi ya lugha za mafumbo tu.
Mkuu, kwa hiyo hapa unamaanisha kuwa hao mawaziri wanajiamulia wenyewe kiasi cha mishahara yao?! Samia anapowashutumu kuwa '.......lakini mbona mnakula sana......mtavimbiwa' anamaanisha wanakula sana mishahara yao?!
Uongo na unafiki ni tabia za shaitwani.....mkatae shaitwani.
 
Katiba hata ya sasa hairuhusu hayo onyesha kifungu kinachoruhusu kula kwa urefu wa kamba
Kifungu cha kutokushtakiwa baadae ndicho kinaruhusu kuwa wezi hawa watu.
Umeshausikia wizi wa mwendazake & Company ulivyo wa kutisha?
 
Lazima kamba nayo itunzwe la sivyo itakatika
Ila Mungu huingilia kati huikata ndio chain huwa inaishia hapo
Wengi hao wezi wala kwa urefu wa kamba zao Mungu alishawashughulikia sana tu hawali vyakula vyenye chumvi wala mafita wala sukari waba mimaradhi kibao hawa enjoy hizo pesa wabazoibia walalahoi wakati mlalahoi anakula chumvi,mafuta na sujari kibao na nyama choma kibao na haumwi

Yenyewe kutwa inahangaika dawa na mazoezi na kukwepa vitu vitamu kama nyama,chakula chenye mafuta ,sukari na vitabu kibao

Mungu kawadhibiti vibaka hao kuwa mtaiba mabilioni lakini hamtayafaidi afya zao lazima ziwe mgogoro

Tafuta fisadi lolote lisilo na maradhi makubwa liwe jike au dune utapata moja kati ya mia moja mengi miradhi kibao
 
Back
Top Bottom